Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Hii ni kwa Kiranga na mshamba_hachekwi , naomba maoni yenu 🤔
Dini lengo lake kuu ni kuwaunganisha watu kuwa katika udugu mmoja kwa ufunuo wa chanzo kimoja cha asili, lakini dini imekuwa tofauti imekuwa uwanja wa ubishani nani yupo sahihi?
Lengo la jumla la dini halipo ila lipo lengo la kumfanya binadamu kuwa bidhaa katika mafundisho yao. Anayo kheri binadamu asiye na dini lakini ndani upo upendo wenye utu kuliko binadamu aliye na dini lakini ndani upo upendo wa utengano na dhihaka.Upendo ulio na unyama ndani
Dini zimeruhusu Mungu kufa, kwakua kila dini imeunda Mungu wa kumtumikia mwenye sifa tofauti kabisa, ulimwengu wenye dini zaidi ya Elfu kumi umepoteza maana muhimu ya dini kwa kutojibu swali hili "Kwa nini ninaishi, na ni nini mtazamo wangu kwa ulimwengu usio na kikomo ambao unanizunguka?"
Dini zinaingia sana katika mijadala ya nje na kusahau ndani kwenye msingi halisi, hii huonesha jinsi dini zenyewe zisivyo jitambua katika "Upendo" unao enezwa
Binadamu mwenye hekima huutafuta ustaarabu nje ya dini, ustaarabu upatikanao katika dini huua asili ya binadamu na kumvisha asili bandia. Dini zimewekwa katika kumchachisha binadamu ufahamu wake
"Wale wanao jitambulisha katika ubinadamu wao wana upendo kuliko wale wajitambulishao katika dini zao. Wale wajitambulishao katika dini zao hujihesabia Kweli na haki na wale wajitambulishao katika ubinadamu wao huhesabiwa watu wa ulimwengu potevu"
Tujiulize binafsi, tujiulize tukiwa nafsi huru, tujiulize kabla ya kujazwa maarifa ya nje, tujiulize kwa maarifa ya ndani Je tunafanya jambo sahihi? Matendo yetu yanaendana
sawa na nguvu iliyotutuma ulimwenguni?
Kusudi la maisha halipatikani katika dini,ikiwa tutalitafuta katika dini maisha yatakuwa katili sana juu yetu,ila kusudi linapatika katika "Utambuzi"