Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
BINADAMU NI WANYAMA. NI BINADAMU WACHACHE AMBAO NI WATU. HAYA NDIO MAMBO YANAYOKUONYESHA WEWE NI MTU AU MNYAMA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Kuna dhana zinazochanganya wengi.
Je Binadamu ni Mnyama au Mtu? Au vyote viwili.
2. Ili binadamu awe MTU itampasa awe na mambo Makuu yafuatayo;
I) Mwenye Akili
Akili ni uwezo wa kuweza kukusanya taarifa kwa kutumia mifumo ya fahamu, kuzichakata na kuzichambua, kuzihifadhi na kuweza kuzitumia katika kutatua matatizo yanayomzunguka binadamu. Hasahasa kumrahisishia maisha. Kuyafanya maisha yawe rahisi.
Na hili ili litokee ndipo elimu, tafiti, maarifa hutokea.
b) Upendo.
Nguvu ya kuvutia vitu, mambo, watu na kuweza kuwajali, kuwathamini, kuwllinda, kuwatunza na kuijenga future. Hakuna Future Bora bila Akili na upendo.
Kujipenda na kupenda wanaokuhusu. Kupenda mazingira ultimo.
c) HAKI.
Ili binadamu awe mtu lazima haki iwepo. Haki ni nini?
Haki ni wajibu, majukumu, na malipo anayostahili mtu.
Zipo haki za wote zinazounganisha watu wenye level moja. Zipo haki za makundi kulingana na tofauti za watu kama rika, jinsia, cheo, maumbile n.k.
d) Ukweli.
Hapa tunazungumzia uhalisia, tunazungumzia sayansi.
Binadamu ili awe mtu lazima aishi kwakutafuta Ukweli ili asiwe mtumwa wa vitu, mambo au watu wengine.
Huo ndio utibeli wenyewe, yaani UTU.
3. Binadamu hazaliwo akiwa MTU.
4. Kama inavyochukua miezi zaidi ya sita au Saba kwa mtoto tumboni mwa mama yake ili azaliwe binadamu. Vivyohivyo. Binadamu humchukua miaka na miaka ili awe MTU.
5. Ni binadamu wachache waliowahi kufika level ya kuwa WATU.
6. Wapo binadamu wanazaliwa na kukua na wao kwa utashi wao, kupenda kutafuta ukweli na kuwa huru wanajikuta wakiwa WATU.
7. Wapo ambao hufundishwa na kupewa elimu na ufahamu ya jinsi ya kuwa watu na matokeo yake hugeuka kuwa WATU.
8. Binadamu kama wanyama wengine hawana haki sawa na WATU. Hilo wengi hawalijui.
9. Mimi Robert Mtibeli, kama nitakuwa sijitambui, sina maarifa, sielewi, system ya dunia, nature ita react kwangu kwa namna hiyohiyo. Haitanichukulia kama MTU isipokuwa itanichukulia kama Mnyama.
10. Na Nature inaponichukulia kama mnyana basi Watu watanitumia kama Mnyama na sio kama MTU.
11. Natoa Mfano halisi kwa Wanawake ambao ni Mama, Dada, shangazi na Bibi na binti zetu.
Wanawake zamani hawakuwa watu. Walikuwa wanyama hivi.
12. Mfumo wa zamani uliwatengeneza wanawake kama wanyama wanaofugwa na wanaume. Ingawaje wengi wanakataa ukweli huu lakini ndivyo ilivyokuwa.
13. Ndio Maana ipo mifumo ya Kununua wanawake kama unavyonunua ng'ombe, mbuzi, farasi. Na zamani ungeweza kununua wanawake hata ishirini wawe watumwa wako hapo ambapo sasa hivi wanaitwa MKE.
14. Mwanamke mwenye UTU hawezi kukubali kutolewa mahari(kununuliwa) hilo ni Moja. Pili, Mwanamke mwenye UTU hawezi kukubali kuolewa WAKE wengi kimafungu.
UTU ni uungu. Uungu unahusisha Wivu mapenzi ya MUNGU MMOJA, mke mmoja, mume mmoja.
15. Mfumo wowote unaowafanya wanawake watolewe mahari na kuolewa kimafungu ni mfumo usiomtambua mwanamke kama MTU isipokuwa Mnyama Fulani hivi.
Wengine wanasema wanawake ni chombo cha starehe.
Hii ni tofauti na falsafa za kitibeli.
16. Mnyama kama Kondoo au Bata, unaweza mkamata hivi Leo hapo bandani, ukamchinja, ukamla nyama au ukamuuza. Alafu bata na kondoo wenzake wasifanye chochote kile.
Baba bata, mama bata, ndugu zake bata wakasahau au wakatafuta kisingizio chochote wasifanye chochote.
17. Wanyama kiasili hawanaga Kisasi. Sio kwa sababu wanasahau tuu Bali ni kwa sababu hawana upendo wa kweli, wanajua watazaa watoto wengine.
Ndio maana ya kuitwa Mnyama.
18. Binadamu wengi ambao ni wanyama kama bata, au paka huyo wa hapo nyumbani. Unaweza kuwafanya chochote ikiwezekana kuwauua, kuwafanyia ukatili.
Wataishia kulia tuu, kupiga mayowe. Na mwishowe watafanya nini zaidi kuacha ndugu au mtoto wao apotee hivyohivyo bila kutafuta haki ya ndugu yao kivyovyote.
19. Huwezi muua Mtu alafu ndugu na wazazi wake watu wenzake wakakuacha hivihivi. Lazima ulipwe. Lazima ulipwe.
20. Miungu huwaona Binadamu kama Wanyama. Ndio maana wakati mwingine huhitaji kafara ya ng'ombe, mbuzi, kondoo, na wakati mwingine huomba kafara za binadamu kwa sababu binadamu asiye mtu ni mnyama tuu.
21. Kauli ya ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga. Inahusu kuua WATU sio kuua binadamu.
Ndio maana wengi hujiuliza mbona Kila uchwao binadamu wanauawa lakini wauaji wanadunda tuu. Jibu ni moja. Kuua binadamu asiye mtu hakuna madhara labda upate madhara ya kiserikali na ni mpaka serikali ifuatilie, ione huo umuhimu.
Sasa vipi kama Serikali ndio inahusika? Nani atafuatilia?
Hapo ndipo Binadamu anabaki kuwa Mnyama tuu. Hakuna kisasi cha mnyama. Hakuna.
22. Mtibeli unajaribu kusema nini, Ndugu zangu ninachokisema mnakijua.
Upendo, haki, akili, na ukweli. Yaani Utibeli.
23. Swali linakuja, je kuna wanyama wenye utu zaidi ya binadamu. Jibu la haraka Sana ni hapana. Binadamu kwa hapa duniani ndiye Mnyama aliyepewa fursa ya kuwa MTU.
24. Jipende.
Ipende familia yako.
Mpende mkeo/Mumeo.
Penda watoto wako.
Penda wazazi wako.
Watu huwezi kuwaona wanachukia familia zao.
Usipoopenda familia yako unatofauti gani na Wanyama?
Kama unampenda utamlinda na utajilinda.
25. Familia za Watawala. Hawajawa Watawala kibahati bahati. Na moja ya mambo ambayo ukitaka wakupoteze bila kikao bila kujali Sheria za nchi au dunia basi ingilia Familia zao.
Jaribu hata kidogo tuu utaona response yao itakuwaje.
Bila kujali huyo mwanafamilia wao anamakosa au hana.
Na spirit hii haiji baada ya kupata madaraka bali ni spirit waliyonayo tangu hawajawa hapo walipo.
26. MTU ni Kutawala mazingira.
Na huwezi kutawala mazingira kama utaishi kama Mnyama.
Nimemaliza. Mwenye swali anaweza kuuliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam