Binadamu wenye uthubutu duniani

Binadamu wenye uthubutu duniani

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Kama ulidhani umemaliza kusikia kuhusu Binadamu wenye uthubutu duniani basi nikwambie hujaona kitu bado 😃, hii ni baada ya Watu watano kukamatwa na Polisi nchini India kwa tuhuma za kutengeneza kituo bandia cha Polisi na kuendesha shughuli zote za Jeshi la Polisi kwa miezi nane bila kugundulika.

Genge hilo la Wahalifu lilikuwa likifanya kazi zake katika mji wa Banka Mashariki mwa Jimbo la Bihar ambapo pia wamekuwa wakiwatoza Watu mamilioni ya pesa ili kushughulikia kesi zao.

Baadhi ya mitandao ya India iliripoti kwamba moja ya vilivyowachomesha na kusababisha kushtukiwa ni bendera feki ikipepea nje ya kituo hicho ambacho walikijenga umbali wa mita mia tano tu kutoka Kituo halisi cha Polisi.
 
Back
Top Bottom