Binafsi naona hii ndiyo faida kubwa ambayo Tanganyika inapata kupitia Muungano

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Faida ya kupata sehemu ya bahari, yaani exclusive economic zone(EEZ). Kisheria mile 200 kutoka pwani ya nchi ni eneo la kiuchumi la nchi husika. Hapo inamaana kilomita kama 320 kutoka pwani ya Tanzania bara kuingia bahari ya Hindi ni eneo letu la kiuchumi. Mafuta na uvuvi wa eneo hilo ni wetu peke yetu.

Sasa hakuna tatizo kwa sababu tuneungana, lakini kama tungekuwa hatujaungana, eneo ilipo Zanzibar ingezuia muendelezo wa eneo hili. Umbali wa kutoka Pemba hadi Unguja, kuelekea mashariki baharini Km 320 za eneo la bahari tungepoteza.

Binafsi naona hiyo ndiyo faida ya Muungano kwa Tanganyika, faida kubwa sana.
 
Kwa nini unaamini Zanzibar ingeizuia bara na si Tanganyika kuizuia Zanzibar?
 
Kinachotakiwa ni kujadili kuondoa umasikini Tanzania ila kila kukicha tukiamka na hoja za Muungano tutaendelea kuwa masikini na rasilimali tunazo. Umoja ni Nguvu Utengano ni Udhaifu.
 
Hio ni faida Kubwa sana, ukitumia rasilimali ktk hilo eneo nchi inakua Tajiri.
 
Kinachotakiwa ni kujadili kuondoa umasikini Tanzania ila kila kukicha tukiamka na hoja za Muungano tutaendelea kuwa masikini na rasilimali tunazo...Umoja ni Nguvu Utengano ni Udhaifu.
Kama vipi Wazanzibar wajiamini tu.

Twende serikali moja.
 
Eneo la bahari la Tanganyika nilaimeza mpaka Zanzibar yenyewe

Hatishitwi mtu apa
 
Imagine Rwanda ingekuwa ndani ya Tanzania kama ilivyo Zanzibar, genocide ya 1994 ingetokea?
 
Faida ya kupata sehemu ya bahari, yaani exclusive economic zone(EEZ). Kisheria mile 200 kutoka pwani ya nchi ni eneo la kiuchumi la nchi husika. Hapo inamaana kilomita kama 320 kutoka pwani ya Tanzania bara kuingia bahari ya Hindi ni eneo letu la kiuchumi. Mafuta na uvuvi wa eneo hilo ni wetu peke yetu.
Sasa hakuna tatizo kwa sababu tuneungana, lakini kama tungekuwa hatujaungana, eneo ilipo Zanzibar ingezuia muendelezo wa eneo hili. Umbali wa kutoka Pemba hadi Unguja, kuelekea mashariki baharini Km 320 za eneo la bahari tungepoteza.

Binafsi naona hiyo ndiyo faida ya Muungano kwa Tanganyika, faida kubwa sana.
Tanganyika haitishiki na Zanzibar

Ukianza kuhesabu eneo la maji la Tanganyika, kwa upande wa kaskazini wa Tanganyika, ka Zanzibar kanamezwa kote
 
Faida ya kupata sehemu ya bahari, yaani exclusive economic zone(EEZ). Kisheria mile 200 kutoka pwani ya nchi ni eneo la kiuchumi la nchi husika. Hapo inamaana kilomita kama 320 kutoka pwani ya Tanzania bara kuingia bahari ya Hindi ni eneo letu la kiuchumi. Mafuta na uvuvi wa eneo hilo ni wetu peke yetu.

Sasa hakuna tatizo kwa sababu tuneungana, lakini kama tungekuwa hatujaungana, eneo ilipo Zanzibar ingezuia muendelezo wa eneo hili. Umbali wa kutoka Pemba hadi Unguja, kuelekea mashariki baharini Km 320 za eneo la bahari tungepoteza.

Binafsi naona hiyo ndiyo faida ya Muungano kwa Tanganyika, faida kubwa sana.
Acha uwongo huo bado tutakuepo na eneo kubwa tuu bila hiyo Zanzibar . Coast ya Tanzania ina km nyingi za mraba tuna visiwa vingi Sana ikiwepo kikubwa ni mafia Island
 
Kama vipi Wazanzibar wajiamini tu.

Twende serikali moja.
Serikali mbili tu mnawabana hiyo serikali moja si itakua hatari hapo wenzetu wazanzibar wanaamini katika maisha bora kupata mahitaji muhimu na vitu vya matumizi kwa bei rafiki maana Kodi yao ni rafiki pia wakati bara wanaamini katika kukomoana yaani tv tuu ni starehe...
 
Mbona huku bara wapo wanaishi tu kama sisi.

Matatizo yapo na hayaepukiki.

Tuwe serikali moja, tuchanganye, kila kilichopop tupambanie hivyo hivyo.

Huu muungano wenye lawama, mzanzibar yeye chake chake, lakini mtanganyika yeye chake ni cha wote
 
Sasa hivi Zanzibar Ni Kama mkoa wa Tanzania, ingekua sio muungano halafu ukawa mkoa wa Somalia/ au nchi ya kibeberu, huoni kwamba tungekua hatuna amani tuliyo nayo?
 
Unakaririshwa kanisani
 
Back
Top Bottom