Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Ninavyojua mimi wakristu hawatakiwi kufunga kama wanavyofanya waislam.Wakristu huwa wanatakiwa kujinyima ili kusaidia watu maskini au wenye uhitaji.Kwa mfano,kama mtu huwa anakunywa bia nne kwa siku anaweza kunywa mbili na pesa ya zile mbili aliyookoa anapeleka kwa maskini.
Funga ina kusudio moja ila kwa sasa show off ni tatizo sana...Hizo futari nyingi ni batili maana wanafuturisha kama kukuza urafiki ,walengwa ni watu maskini kabisa...


Kiufupi wanaopiga klele huko mitandaoni hata dini hawajui ni ule ushabiki maandazi. Hiyo mialiko ilitakiwa pasiwe na camera wala kuchukua video...Msaa ni kimya kimya na pia Mwezi unapoisha iwe ni tamaduni endelevu kuwakumbuka watu maskini.
 
Kwani kufuturu ni nini mkuu? Huoni hiyo ni kwa ajili ya kudumisha mahusiano mema japo haifuti ukweli mu waroho na waoga wa njaa na pia sio.kama mnafunga bali mnabadilisha muda wa kula. Baada ya kula mchana, mnakula usiku kucha mkuu huku mchana mnatunukisha midomo. 🤣🤣🤣

Usimind jamaa yangu. Nakutania tu kaka. Nyie mnafunga bwana.
Kufuturu ni kufungua baada ya kufunga!
Sasa kati yetu tunaowaalika makafiri kufuturu pamoja na nyinyi mnapenda kufakamia futari za waislamu wakati hamfungi hivi sisi tunaolika ndio waroho au nyinyi mnaokwenda kula vyakula vya waislamu ndio waroho?!
Sisi tunafunga Ramadhani siku 30 au 29 na tunakula tangu jua likizama na tunaanza kufunga alfajiri ikichomoza!
Nyinyi inasemekana mnafunga siku 40 na mkishafungua jioni hamli tena hadi kesho jioni , HIVI KATI YETU NA NYINYI NI WEPI WANAONUKA MIDOMO!.
Bila shaka NYINYI MNAOFUNGA MUDA MREFU ZAIDI NDIO MNAONUKA MIDOMO!.
 
Mtumishi wa Mungu Samson Ernest kuna huyu umat wa allah anauliza kama mnaweza vumilia njaa hata dakika 3? Najua FPCT hapo Singida Mjini mna mifungo mingi. Kuna ule wa kitaifa wa siku 21 kama ambao sisi TAG tunao wa kitaifa kwa siku 21 kila mwanzo wa Mwaka. Pia kuna mifungo ya kawaida ya kutaniko la mahali pamoja.

Ndugu yangu Lucha binafsi sasa nipo CBC hapa miuji Dodoma na nina funga kila wiki siku 3 kavu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili jioni. Hata nikiwa natumia TAG kule GEITA huwa nafunga kavu 3 days lakini pia kuna mifungo ya masaa 12 na masaa 24.

Kufunga kwa mkristu ni kitu cha kawaida pale anapoamua kumnyenyekea na kumtafuta Mungu wake na mara nyingi hatujitangazi kama tumefunga. Kuanzia nikiwa kazini nilikuwa nafunga na kama wenzangu wanakula kazini mi nawaacha na kujitenga wakimaliza kula tunaendelea na kazi otherwise umeandika hii comment kwa mzaha tu mkuu.
Acha kujitesa na njaa funga ya mkristo haina malipo
 
Mtoa mada anasumbuliwa na wivu na chuki dhizi ya uthabiti wa waislam juu ya dini yao.

Huu mwezi wa ramadhani ni wa kipekee ipo hivyo ilikua hivyo na itakua hivyo miaka yote hata nyie makafiri mkichukizwa nao.

Baadhi ya wakristo ni wapuuzi sana hivi hata mnatafakari mnayoyaandika kuna muda mpaka unajiuliza mtu kama mtoa mada kama yuko na akili timamu.
 
Mimi najiuliza sasa kama unafunga usiku usiku unaamka kushindilia Ugali ya Nini?

Alafu Unashinda unajisifu Umefunga kweli?

Alafu najiuliza kwa Nini bei za vitu zinapanda kipindi cha mfungo wa ramadhani?

Utagundua wafanyabiashara waligundua kwamba bidhaa za vyakula utumika sana kipindi hicho.

Sasa kama tunafunga kwa Nini jioni misufuria machakula kibao ya Nini kama sio ulafitu. Yaani jioni ukakula na unafidia chai ya Asubui + CHAKULA cha mchana = hakuna funga hapo.

Mtume Alikua mwadilifu sana na Aliweka vizuri sana maana ya funga, unajinyima ili sehemu ya fedha uwasaidie waitaji.
 
Kristo anataka ukifunga ufanye kwa siri
Kafie mbali na kristo wenu?! Unataka na sisi tumfuate kristo ?! Sisi ni waislamu na funga zetu zinafuata misingi mitukufu ya Quran na Sunna za Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Sisi ni wafuasi watiifu wa mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Na kwetu sisi funga zimegawanyika sehemu mbili.
Kuna funga za FARADHI ( funga za lazima ) ambazo ni kama vile funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani .
Hii ni funga ya lazima kwa kila muislamu isipokuwa watoto, wendawazimu, wagonjwa , wazee walioisha nguvu na wasafiri.
Halafu kuna funga za sunna ( funga za khiyari anayetaka anafunga asiyetaka halazimishwi ) .
Funga hizi zipo mwaka mzima na waislamu wanafunga swaumu hizo kila mmoja kwa nafasi yake na nguvu ya Imani yake.
Waislamu huwa wanafunga funga hizi huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku na wagalatia huwa hamjui kuwa wahusika wamefunga kwa sababu hizo ni funga za khiyari hivyo huwa hakuna haja ya wao kujulikana kuwa wamefunga.
Mfano wa funga hizi ni kama vile :
A. Funga ya siku sita baada ya kumaliza mwezi wa ramadhani.
B . Funga ya kila jumatatu na kila alkhamisi.
C. Funga ya siku tati kila mwezi .
Hii huitwa funga ya masiku mweupe ambayo ni kila tarehe 13, 14,na 15 tarehe ya mwezi mwandamo siyo miezi hii ya kirumi.
D. Kuna funga ya siku ya arafa ( tarehe 9 ya mwezi wa 12 wa kiislamu unaojulikana kama Dhul hijja au mfungo TATU.
E. Funga ya siku ya Ashura ambayo ni tarehe 10 ya mwezi wa kwanza wa kiislamu unaojulikana kama Muharramu au mfungo nne.
Kwahiyo waislamu tunafunga mwaka mzima kwa tarehe tafautitafauti na masiku tafautitafauti lakini hatutangazi kwakuwa hizo ni funga za khiyari kwa kila anayetafuta thawabu kwa mwenyezimungu.
Funga hizi anayefunga anapata thawabu na asiyefunga hapati dhambi tafauti na mwezi wa Ramadhani ambao anayefunga anapata thawabu na asiyefunga bila udhuru wa kisheria anapata dhambi.
Kulingana na maelezo yenu KWARESMA KWENU SIYO FUNGA YA LAZIMA KWA WAKRISTO WOTE.
Anayetaka anafunga KWARESMA na asiyaka hafungi na hakuna wa kumuuliza kwanini hafungi.
Sasa msitake kufananisha Ramadhani na kwaresma.
Mwezi wa Ramadhani ni lazima kwa waislamu wote wasiokuwa na dharura za kisheria kufunga siku 30 au 29 kama Allaah alovyoamrisha kufunga pale aliposema katika Suuratul Baqara Aya ya 183 ya kwamba :
"{ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ }
"Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, ( mumefaradhishiwa kufunga )
kama waliyo andikiwa (walivyofaradhishiwa ) walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamungu.

Na katika Aya ya 185 Allaah akasema:

" { شَهۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهۡرَ فَلۡيَصُمۡهُۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُكۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ }

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo (ndani yake ) Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.
 
Wewe ulishawahi kupigwa kisa umekula hadharani au unaleta hadithi za Abunuasi?!
Mimi nipo Moshi mjini na ninafunga mimi na waislamu wengine, na hapa mama ntilie na migahawa kutwa nzima watu wanakula hadharani wala sisi hatuoni shida yoyote kwasababu dini yao inawaruhusu kula mchana kama watakavyo!
Sio migahawa tu bali hata vilabu vya walevi na bucha za nguruwe zinafanya kazi mchana wa Ramadhani wala hakuna muislamu anayelalamika wala kunung'unika!.
Sasa habari za kwamba sisi tukiona mtu anakula mchana tunaumia naona kama HADITHI ZA PAUKA PAKAWA!.
Huko zenj je
 
Mimi najiuliza sasa kama unafunga usiku usiku unaamka kushindilia Ugali ya Nini?

Alafu Unashinda unajisifu Umefunga kweli?

Alafu najiuliza kwa Nini bei za vitu zinapanda kipindi cha mfungo wa ramadhani?

Utagundua wafanyabiashara waligundua kwamba bidhaa za vyakula utumika sana kipindi hicho.

Sasa kama tunafunga kwa Nini jioni misufuria machakula kibao ya Nini kama sio ulafitu. Yaani jioni ukakula na unafidia chai ya Asubui + CHAKULA cha mchana = hakuna funga hapo.

Mtume Alikua mwadilifu sana na Aliweka vizuri sana maana ya funga, unajinyima ili sehemu ya fedha uwasaidie waitaji.
Wanabadilisha ratiba tu ya kula eti mtu anajidai kuwa akafunga. Aisee hakuna kirusi kibaya tulipandikiziwa waafrika Kama hizi dini za kuja na mashua
 
Asante sana.sifa na utukufu ni Kwa Mungu.

Tena aliyekwambua sie mwisho kula sa tano usiku kakudanganya, hakuna mkristo anaefunga anakula usiku huo
Tukishafungua sa kumi na mbili wachache wanakula sa mbili kidogo basi mpk kesho tena
Kwa maandiko gani katika Bible mmeamrishwa mfunge hivyo?
 
Je, huu ni uungwana? La hasha,huu si uungwana hata kidogo
Mimi sina dini lakini nawakubali wakristo japo wana mapungufu yao lakini yanavumilika. Wakristo wamevuka stage ya unyani kidogo ndio wanausogelea ubinadamu.
Wengine hawa wa alahu akbaru wameachwa mbali kiasi cha kukatisha tamaa.
Nimeangalia huko Syria alahu kwa alahu wanauana kikatili sana kitu ambacho hata nyani hawafanyi.
Mfano mwingine ukienda hepo Zanzibar alahu kafunga lakini akiona mtu mwingine akila anaona wivu hadi anaanzisha fujo. Huu sii uungwana hata kidogo
 
Mimi naongelea ustaarabu siongelei vitabu vya dini
Dini ndio ilio leta swala la kumfunga Acha kijitia utahira usio zaliwa nao.
Waislam wanafunga sababu wameamrishwa katika Dini yao hawakurupuki tu.
Wewe unafunga kwa andiko lipi
 
Tatizo unafananisha chaki na chizi, huenda vikafanana kimuonekano (zote zinaitwa ni funga) lakini ni vitu viwili tofauti.
Naomba kupata muongozo wa funga ya Kwaresma, kwani funga ya waislamu ni kutokula na kutokunywa na kujizuia na matamanio ya nafsi kuanzia Alfajiri mpaka kwa kuzama kwa jua.
Acha uvivu wa kusoma maandiko
We umefunga lakini au ndio mbwembwe tu..?
Funga ni Siri ya mfungaji na MUNGU mwenyewe
 
Asante sana.sifa na utukufu ni Kwa Mungu.

Tena aliyekwambua sie mwisho kula sa tano usiku kakudanganya, hakuna mkristo anaefunga anakula usiku huo
Tukishafungua sa kumi na mbili wachache wanakula sa mbili kidogo basi mpk kesho tena
Barikiwa sana mkuu
 
Siku hizi post za maana zimeisha, lengo la post yako ni kushindanisha funga au!!! Wakubwa sasa nyie, haya mambo ya kiuchizi hayafai, kama kweli umefunga kwaresma au yoyote Ile, ajuaye ni Mungu wako, sasa unafunga halafu unawasema wenzako kuwa hawana kitu, huo ni ujinga.
Na wewe umekuja kuchangia kitu kwenye ujinga huu
 
Huko zenj je
Kwani wewe uko zenji?
Mambo ya zenji waachie wazenji kila nchi ina utaratibu wake, mila na desturi zake. Lakini Mimi ninavyofahamu hata huko zenji wakristo hawakatazwi kula.
Ila muislamu akila hadharani lazima achukuliwe hatua za kinidhamu kwa sababu Moja ya misingi muhimu ya dini yetu ni kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Allaah kalieleza hili ndani ya Suurat Aalu Imrani Aya ya 104 pale aliposema:
{ وَلۡتَكُن مِّنكُمۡ أُمَّةٞ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلۡخَيۡرِ وَيَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ }
Na liwepo miongoni mwenu kundi (ambalo) linalingania katika kheri na linaamrisha mema na linakataza mabaya.
Na hao ndio walio fanikiwa.

Na katika sura hiyohiyo aya ya 110 Allaah akasema:

{ كُنتُمۡ خَيۡرَ أُمَّةٍ أُخۡرِجَتۡ لِلنَّاسِ تَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَتَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِۗ
Nyinyi mmekuwa umma bora walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.

Na mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
anasema katika hadithi aliyoipokea Imamu Muslim kutoka kwa swahaba Abuu Sai'yd Al khudry
رضي الله عنه.
Mtume amesema:

" مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ ".
Atakayeona miongoni mwenu jambo ovu na alizuie kwa mkono wake, kama hawezi basi ( alikataze ) kwa ulimi wake , na kama hawezi basi ( alichukie ) kwa moyo wake na huyo ni mdhaifu mno wa imani"

Kwa sababu kufunga Ramadhani ni jambo jema na ni amri ya Allaah
سبحانه وتعالى
Na kula mchana wa Ramadhani bila dharura ya kisheria ni jambo baya la kumuasi Allaah ndio maana mwislamu anayekula mchana wa Ramadhani bila dharura ya kisheria katika jamii ya waislamu wengi humchukulia hatua za kinidhamu!.
 
We ni kichwa maji Sasa huoni hizi ni dini mbili tofauti? Zingekua sawa c ingekua dini Moja
Dini ipi na ipi?Mimi nimezungumzia wakristo,wewe unazungumzia watu wa dini gani nyingine?
 
Back
Top Bottom