Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 422
- 489
Kufunga maana yake ni nini?!Maandiko yapo mengi mno, haya ni baadhi tu;
Kutoka 8
8 Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni Bwana, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee Bwana dhabihu.
Zekaria 10
1 Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.
Mathayo 17
21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
Mathayo 7
7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
Andiko gani linasema mfungue saa 12 za jioni?!
Kumbuka saa 12 jioni kwa mikoa ya Kigoma , Kagera na Rukwa hadi Mbeya na Ruvuma bado ni mchana kabisa, halafu mnasema sisi waislamu ndio walafi wakati nyinyi mnafungua mchana bado jua linawaka?! Ni andiko gani linawaambia mfungue saa 12?! Na ni andiko gani linakataza watu kula usiku ?! Kwani nyinyi Yesu aliwakataza kula DAKU?!
Kama kawakataza tuonyesheni andiko!