Binti afanyiwa uonevu na anyimwa haki ya kuitwa kwenye usaili

Binti afanyiwa uonevu na anyimwa haki ya kuitwa kwenye usaili

Mimi sijasoma ila naweza kuwa na uelewa kidogo ila haya mambo ni magumu sana, hii inaitwa watu kujuana kwa vilemba
 
Ni jambo la ajabu lakini la kweli.
Mojawapo ya tangazo lililowekwa katika tovuti ya ajira portal na mara zote kabla hujaweza ku apply system inakuambia ama kukukumbusha uhakikishe ume attach barua ya maombi ya kazi.

Binti huyu alikua na sifa zote kama kazi ilivotaka na pia system ilimuwezesha kuomba hio kazi, sababu sifa anazo, na zaidi profile ama wasifu wake amejaza taarifa kwa usahihi kabisa na kuambatanisha viambata vyote muhimu,

Cha ajabu tarehe na ratiba ikatolewa ya usaili kwenye tovuti,ila ajabu kwenye application yake kaandikiwa hajawa shortlisted sababu haja attach transcript ya chuo kikuu( in which kipo). Na kama tume ya ajira ingetaka kujiridhisha kuangalia academic transcript ya mtahiniwa huyu walishindwa nini ku view profile yake na kuiangalia?

Je huu sio uonevu na kunyimwa haki ya kufanyiwa usaili kwa wazi kabisa ? Au ndio njia ya kuwasafishia wengine njia ya kupata ajira kiulaini?

Mana ni kama waliangalia kila namna watafute sababu wakakosa na wakaamua kupachika sababu hio isiyo na mashiko
Uzi wako umekosa mashiko kwasababu ya kutanguliza mfumo jike "binti"
 
Ulifanyaje boss?
Mimi nimeapa hii kitu lazima ifike hadi kwa waziri husika. Haiwezekani mtu ufanyiwe uonevu na kukosa haki kwenye nchi yako
Wasiliana nao hiyo ni system error hutokea sana acha kuwatisha watu! Wasiliana nao kama unayoyasema ni kweli ataongezwa kwenye usaili!
 
Back
Top Bottom