Binti amenichanganya mpaka nimeshukia njiani

Binti amenichanganya mpaka nimeshukia njiani

Hahahahahahaa polee

Nafasi yako ilikuwa ndani ya basi ucheze karata zote ili binti asishuke Iringa uende nae hadi Dar angekuwa keshamuacha jamaa yake. Hehehehee polee.

Nakumbuka nilipokuwa kigori **** mkaka alishuka kwenye daladala kituo sio chake na alinisindikiza hadi nyumbani hehehe. Kote huko sijamjibu hata kimoja alichokuwa ananiongelesha. Nilipokaribia nyumbani nikamwambia skiza nipe namba ya simu ya kazini kwako na anuani ili mimi nikutafute maana enzi hizo geti kali na sikutaka apajue nyumbani. Nikimuacha anisindikize kutoka kituo cha daladala hadi karibu na nyumbani maana kigiza cha saa kumi na mbili jioni kilikuwa kimetanda hivo nilikuwa na woga wa kutembea mwenyewe.
Hahahaha nilikuwa nashangaa wanaume unaanzaje kumfatilia mschana hata humjui tena alinilipia nauli, simjibu chochote aniongeleshacho mie natembea tuu hahahah

Kwenye daladala sasa akishakulipua nauli utaona konda anauliza sheli. ... kimya.... kwa mpemba.... kimya... jamaa anasubiria binti aseme shusha ili naye ashuke.

Siku ingune nilikutana na jamaa wa hivi na nilimuuza maana nilikuwa natoka kawe naenda posta, baada ya kunilipia nauli nikasema leo atakoma maana ukimuangalia usoni anakutazama kwa macho ya kukutongoza tuu.
Kufika mbuyuni konda kuuliza mbuyuni nikasema shusha, yeye akatangulia kusimama na kushuka mie nikajichelewesha nilisimama kisha nilipoona kushuka nikainama na kurudi kukaa. Konda kuuliza mwingine kimyaa.... akaruhusu gari iondoke heheheheh nilichungulia nje jamaa macho yanamtoka maana mda ule kupata usafiri wa posta maeneo yale ni shida.

Poleni ila nilifanya yale kwakuwa ilikuwa utoto tuu hahahaha kweli wanaume mmeumbiwa mateso.

Wakati nasoma sekondari kuna mvulana flani alishanisindikiza toka tumeshuka kwwnye daladala hadi eneo la tuition wakati huo na yeye anasoma tuition ila kwingine. Siku hiyo alinisubiri hadi mie nimetoka tuition na tunarudi tumepanda daladala moja. Akanilipia nauli, sikutaka apajue nyumbani hivyo niliposhuka mwisho wa kituo nikamwambia nipe address ya shule unayosoma na jina tuandikiane barua si unajua home kuna mbwa wakali? Akanielewa ndo nikamtoa kihivyo daah.

Yaani mleta mada nimekuelewa sanaa. Pole kwa yaliyokusibu sio pekeyako ni wanaume wengi tuu huwakuta haya.
Kasie utakuwa mtamu sana machoni .

I wish uje pm unizingue kama hizo "crush" zako[emoji3]
 
Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
Yaani hujatengeneza mchongo ukiwa kwa basi haf ume dro ndo unaaza kunyatia. pole aise
 
Kasie utakuwa mtamu sana machoni .

I wish uje pm unizingue kama hizo "crush" zako[emoji3]

Kawaida sana sema haya mambo hayafanani machoni pa watu, we unaweza kuangalia tunda ukasema limeiva kwa kuliwa mwingine akasema hapana limeiva sana siliwezi mwingine akasema tunda raha ulile bichi na chumvi.

Waweza jikuta unasema huyu nae, mbona anajipromo wa kawaida sanaa ila kuna vinasaba ambavyo kila mwanaume kwa nyakati tofauti akiviona huona Kasie ni bonge ya totoz hehehehe hata hivyo sikuhizi nshazeeka si kama nilivokuwa kigori.
 
We jamaa bwege Kweli... Sikuhizi whatsup inapiga sound kuliko ulivofanya
 
Nimesoma comments mpaka page hii ya 5. Nimecheka mno. Ndivyo tulivyo
 
Nimesoma comments mpaka page hii ya 5. Nimecheka mno. Ndivyo tulivyo

Mmmh kweli umecheka ssna hadi 3 kwako imekuwa 5 hehehhee hongera kwa kufurahi na kuongeza maisha.
 
Mambo kasie?

Kumbe roho mbaya ulikuwa nayo kitambo tu na siyo kwa binamu yako.

Mambo poa,

Hahahah hujanielewa tuu Kasie hana roho mbaya yuko peace tuu sema nj mkali akiona mizengwe na ndivyo sivyo.

Binamu kwakweli alinikosea adabu na kama ni roho mbaya kwa binamu acha niwe nayo asee tena akithubutu kurudia namnunia mazima.
 
Mambo poa,

Hahahah hujanielewa tuu Kasie hana roho mbaya yuko peace tuu sema nj mkali akiona mizengwe na ndivyo sivyo.

Binamu kwakweli alinikosea adabu na kama ni roho mbaya kwa binamu acha niwe nayo asee tena akithubutu kurudia namnunia mazima.
Hahahahah!

Siyo vizuri hivyo..kasie
 
Ni kujichanganya na ujinga tu ambao asilimia ya humans upitia ... I blv next time utakuwa umesha learn a lesson
 
Ha haa! Mkuu iyo huwa inatokeaga... Hata mie nilishafanya kama wewe kwenye hizi dala dala...
 
Back
Top Bottom