Binti amenichanganya mpaka nimeshukia njiani

Binti amenichanganya mpaka nimeshukia njiani

Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kama umenifanya nicheke sana , umenifanya leo nikumbuke story kama hiyo ambayo niliificha kwa washikaji, ni kama miaka miwili imepita nilikuwa natoka dzm naenda Arusha kwenye harusi ya rafiki yetu, sasa washikaji wangu wawili waliniomba n9je na nguo zao watakazoo vaa harusini, nakutana na mtoto mkaliii vibaya mno ndani ya basi, yule mtoto alikuwa anashukia njia panda ya kwenda himo alikuwa anaenda marangu baada ya kukosa chansi ya kuongea nae kwenye basi ilibidi na mimi nishuke hapo njia panda huku ni nguo za washikaji na harusi ni kesho yake ilikuwa mida ya saa kumi jioni.Kweli wanawake sometimes hutufanya tuchizike yule mtoto nilimfuatilia mpaka marangu jinsi nilivyopiga sound ni siri yangu, mtoto ilibidi adanganye huko aendapo kuwa basi limeharibika njiani huku washikaji wananiuliza nipo wapi nawaambia gari limeharibika, nikafanya yangu kuja kushtuka mda umeenda nikashawishi binti tukalala kabisa nikasahau nina mzigo wa watu.Nafika arusha kesho yake saa saba, nakuta watu wamenuna hawajaenda kanisani sababu yangu, ila siri nilibakiwa nayo mimi[emoji2] [emoji2] [emoji2] POWER OF PAPUCH
 
Inaonesha we domo zege na limbukeni kabisa. Sa uliona kumsemesha ndani ya siti tena karibu kabisa hata jirani hakusikii ni shida. Huko nje ya basi si ngoma nzito zaidi?? Umebaki kumkodolea mimacho mpaka mwenye nacho akaja kuchukua mzigo wake. Hata namba ya sm ukashindwa kumtoa!! Jamani, hata chembe ya huruma kwa mtu ka wewe miye sina. Pambafuuuu halaf unathubutu kuja aibisha warume hapa JF??? Liwe fundisho kwako na wengine domo zege ka weye.
 
Dah sijui hata mara ya mwisho nimetongoza mwanamke live ni lini ,Teknolojia imefanya mambo kuwa marahisi sana

Eroo natumia Whatsapp ya moto au baridi ,muhudumu letea cup
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kama umenifanya nicheke sana , umenifanya leo nikumbuke story kama hiyo ambayo niliificha kwa washikaji, ni kama miaka miwili imepita nilikuwa natoka dzm naenda Arusha kwenye harusi ya rafiki yetu, sasa washikaji wangu wawili waliniomba n9je na nguo zao watakazoo vaa harusini, nakutana na mtoto mkaliii vibaya mno ndani ya basi, yule mtoto alikuwa anashukia njia panda ya kwenda himo alikuwa anaenda marangu baada ya kukosa chansi ya kuongea nae kwenye basi ilibidi na mimi nishuke hapo njia panda huku ni nguo za washikaji na harusi ni kesho yake ilikuwa mida ya saa kumi jioni.Kweli wanawake sometimes hutufanya tuchizike yule mtoto nilimfuatilia mpaka marangu jinsi nilivyopiga sound ni siri yangu, mtoto ilibidi adanganye huko aendapo kuwa basi limeharibika njiani huku washikaji wananiuliza nipo wapi nawaambia gari limeharibika, nikafanya yangu kuja kushtuka mda umeenda nikashawishi binti tukalala kabisa nikasahau nina mzigo wa watu.Nafika arusha kesho yake saa saba, nakuta watu wamenuna hawajaenda kanisani sababu yangu, ila siri nilibakiwa nayo mimi[emoji2] [emoji2] [emoji2] POWER OF PAPUCH
haha mkuu umetishaaaa, eeh bt hapo ulipiga na papushina eeeh i surrender you
 
Hahahaa. Sikuwahi kuwajaza mkuu. Niko makini kwa hilo. After all mimi wa kawaida mno.
nimeoteshwa kua nawe nimoja ya kiumbe mwenye haiba,ewe kiumbe uliezaliwa kipindi cha mavuno hakika umependelewa na kujaaliwa....... najua kunamijamaa nimeipa verses for free hapa
 
nimeoteshwa kua nawe nimoja ya kiumbe mwenye haiba,ewe kiumbe uliezaliwa kipindi cha mavuno hakika umependelewa na kujaaliwa....... najua kunamijamaa nimeipa verses for free hapa
Mhhhh hayaaaaa. Usiku mwema
 
Hahahahahahaa polee

Nafasi yako ilikuwa ndani ya basi ucheze karata zote ili binti asishuke Iringa uende nae hadi Dar angekuwa keshamuacha jamaa yake. Hehehehee polee.

Nakumbuka nilipokuwa kigori **** mkaka alishuka kwenye daladala kituo sio chake na alinisindikiza hadi nyumbani hehehe. Kote huko sijamjibu hata kimoja alichokuwa ananiongelesha. Nilipokaribia nyumbani nikamwambia skiza nipe namba ya simu ya kazini kwako na anuani ili mimi nikutafute maana enzi hizo geti kali na sikutaka apajue nyumbani. Nikimuacha anisindikize kutoka kituo cha daladala hadi karibu na nyumbani maana kigiza cha saa kumi na mbili jioni kilikuwa kimetanda hivo nilikuwa na woga wa kutembea mwenyewe.
Hahahaha nilikuwa nashangaa wanaume unaanzaje kumfatilia mschana hata humjui tena alinilipia nauli, simjibu chochote aniongeleshacho mie natembea tuu hahahah

Kwenye daladala sasa akishakulipua nauli utaona konda anauliza sheli. ... kimya.... kwa mpemba.... kimya... jamaa anasubiria binti aseme shusha ili naye ashuke.

Siku ingune nilikutana na jamaa wa hivi na nilimuuza maana nilikuwa natoka kawe naenda posta, baada ya kunilipia nauli nikasema leo atakoma maana ukimuangalia usoni anakutazama kwa macho ya kukutongoza tuu.
Kufika mbuyuni konda kuuliza mbuyuni nikasema shusha, yeye akatangulia kusimama na kushuka mie nikajichelewesha nilisimama kisha nilipoona kushuka nikainama na kurudi kukaa. Konda kuuliza mwingine kimyaa.... akaruhusu gari iondoke heheheheh nilichungulia nje jamaa macho yanamtoka maana mda ule kupata usafiri wa posta maeneo yale ni shida.

Poleni ila nilifanya yale kwakuwa ilikuwa utoto tuu hahahaha kweli wanaume mmeumbiwa mateso.

Wakati nasoma sekondari kuna mvulana flani alishanisindikiza toka tumeshuka kwwnye daladala hadi eneo la tuition wakati huo na yeye anasoma tuition ila kwingine. Siku hiyo alinisubiri hadi mie nimetoka tuition na tunarudi tumepanda daladala moja. Akanilipia nauli, sikutaka apajue nyumbani hivyo niliposhuka mwisho wa kituo nikamwambia nipe address ya shule unayosoma na jina tuandikiane barua si unajua home kuna mbwa wakali? Akanielewa ndo nikamtoa kihivyo daah.

Yaani mleta mada nimekuelewa sanaa. Pole kwa yaliyokusibu sio pekeyako ni wanaume wengi tuu huwakuta haya.
MUNGU anakuona.
 
Back
Top Bottom