Binti ameugua ugonjwa ambao umeshindwa kutambulika

Kama hajulikani anaumwa nini muulizeni vizuri huyo binti,akidanganya anadanja kweli

Allah amfanyie wepesi apone.
 
Mpeleke oshenroad haraka sana.
 
Wahi hospitali kubwa, Ni magonjwa ya ngono
 
Saw tutajaribu kumuuliza japo mchakato uliopo kwa sasa ni kumpeleka hospitali
 
calitho sikikiza ushauri muhimu, mpelekeni kijana hospitali ya rufaa acheni kucheza na afya.

Pili ikishindikana huko kwenye rufaa ndipo uje hapa jukwaani kuwa imeshindikana.

Duniani kuna magonjwa mengine siyo ya hospitali, nitakupa tiba yake hadi utoke kwenye rufaa na ionekane mme_ failure!.
 
Asante chief nitareta mrejesho baada ya kutoka hospitali
 
iyo ya waume za watu naskia ina wakuta sana wasichana unapigwa juju ni mwendo wa period non stop nasikia ilimkuta demu mmoja tulikuwa tunapiga naye job ,mtaalamu alimuokoa
 
Kila Mara nmewaambia humu Ndani, Magonjwa yahusuyo NGOZI na sehem zake, Huwa yanahitaji Kuonwa.

Unapoomba Msaada Mitandaoni ya Kijamii, bila kuambatanisha picha, ni vema Ushauriwe tu kwenda HOSPITAL .


Huyo Binti anasumbuliwa na Condylomata acuminata , inayosababishwa na Human Papilloma Virus ( HPV) ambayo pia hupelekea Wanawake kupata UGONJWA WA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI.


Kwa mbali kwakua sijayaona hayo mapele, inaweza kua ana Condylomata Lata inayosababishwa na Syphilis stage 3 , lkn hii lazima tayari iwe imesambaa sehem nyingine za Mwili, mfano, Kinywani, Mwili mzm hasa mapaja, mgongo, viganja kubwa na mapele yanayowasha na kuacha makovu meusi, pia matatizo ya macho .



ITOSHE KUSEMA MPELEKE HOSPITAL KUBWA ANGALAU KUANZIA NGAZI YA WILAYA, MKOA , huko chini utakutana na wahuni tu wale Hela.

Na Binti asione Aibu, mficha Maradhi Kwa Aibu, Kifo humuumbua
 
hakika condoms zitumike tu,, magonjwa mengi mnoooo m mwenyewe sikuwahi waza wala fikiria,,yaani kam mimi mwanzo tu sehem zilkua vile yeye je,,kama ni huo huo lakini kama ni tofauti na nlopata mimi mmmh sjui
Wewe ulipata ugonjwa gani, tiba gani ulitumia, dalili zilikuwaje, funguka Ms R
 
Pole sana
 
Afanye vipimo hivi
1. Infections za Fungus (Candida): Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri yanaweza kusababisha vipele na maumivu, pamoja na kutoa majimaji ambayo yanaweza kuonekana kama jasho au ufanano wa maji ya hedhi. Hii ni moja ya matatizo ya kawaida kwa wanawake, hasa kwenye maeneo ya nyeti.


2. Herpes (HSV - Herpes Simplex Virus): Herpes genitalia inaweza kusababisha vipele na maumivu makali kwenye sehemu za siri. Wakati mwingine, vipele hivi huonekana kama visivyo vya kawaida na vinapoendelea, vinaweza kuumiza sana.

3. Sifilis (Syphilis): Ugonjwa huu ni maambukizi ya bakteria ambayo yanaweza kuathiri sehemu za siri na kuleta vipele. Inashauriwa kupimwa kwa uangalifu kwa ajili ya maambukizi ya Sifilis, hasa ikiwa kuna mabadiliko ya vipele kwenye nyeti.


4. Magonjwa mengine ya ngozi (sifafungus, dermatitis, eczema): Hizi zinaweza pia kuhusisha vipele kwenye maeneo ya siri, ingawa mara nyingi huwa na maumivu ya kupungua na hupungua baada ya matibabu ya kuzuia maambukizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…