Binti ameugua ugonjwa ambao umeshindwa kutambulika

Binti ameugua ugonjwa ambao umeshindwa kutambulika

Afanye vipimo hivi
1. Infections za Fungus (Candida): Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri yanaweza kusababisha vipele na maumivu, pamoja na kutoa majimaji ambayo yanaweza kuonekana kama jasho au ufanano wa maji ya hedhi. Hii ni moja ya matatizo ya kawaida kwa wanawake, hasa kwenye maeneo ya nyeti.


2. Herpes (HSV - Herpes Simplex Virus): Herpes genitalia inaweza kusababisha vipele na maumivu makali kwenye sehemu za siri. Wakati mwingine, vipele hivi huonekana kama visivyo vya kawaida na vinapoendelea, vinaweza kuumiza sana.

3. Sifilis (Syphilis): Ugonjwa huu ni maambukizi ya bakteria ambayo yanaweza kuathiri sehemu za siri na kuleta vipele. Inashauriwa kupimwa kwa uangalifu kwa ajili ya maambukizi ya Sifilis, hasa ikiwa kuna mabadiliko ya vipele kwenye nyeti.


4. Magonjwa mengine ya ngozi (sifafungus, dermatitis, eczema): Hizi zinaweza pia kuhusisha vipele kwenye maeneo ya siri, ingawa mara nyingi huwa na maumivu ya kupungua na hupungua baada ya matibabu ya kuzuia maambukizi.
🙏
 
Ngono zembe zitatuua hakika safari hii,ukiachana na ukimwi magonjwa mengi sana ya ngono ya kutisha,,io shida nmenusurika karibuni tu,sema mm niliwahi,nyama ya uchi ya ndani inakua ngumu inachomoza nje,na hayo yanayoota wanaita masundosundo sjui aaah,,na hauna dawa rasmi hospital naskia pia,,niljitibia kienyeji nyumbani tu,kam nayeye ni ivo imefika stage kubwaaa....
Muelekeze ulitumia dawa gani
 
Habari wana jamii.

Nahitaji msaada wa ugonjwa ambao umempata binti ambaye ni mtoto wa rafiki yangu mwenye umri wa miaka 18.

Binti huyu ameugua ugonjwa ambao umeshindwa kutambulika ni ugonjwa gani. Alianza kwa kuugua tu kawaida alipoenda kupima afya akagundulika ana U.T.I na malaria. Baada ya tiba hali ilibadilika akapata upele mfano wa vipele vya tetekuwanga hali ikabadilika akawa ni mtu ambaye analia kwa kuugulia maumivu

Mabadiliko yakazidi kuwa makubwa mpaka sehemu za siri ambapo binti kwenye nyeti zake katokwa na mapele makubwa mfano wa yale mapele yanayopatikana ukiwa umenyoa nyeti kwa wembe kibaya zaidi nyama ya ndani ya uke imechomoza kutoka nje na anatokwa na maji mengi mfano ya jasho hayatoki kwa wingi kama period ila yanatoka kwa taratibu yeye mwenyewe anadai kusikia maumivu anayoyapata ni kama anaungua moto kwenye uke tumejaribu kumpeleka kituo cha afya wameshindwa kuutambua ni ugonjwa gani kwa sasa yupo zahanati japo mpaka sasa hatujui ni ugonjwa gani ana unasababishwa na nini na tiba yake ni ipi kwa yoyote mwenye kuufaham ugonjwa huu atupe mrejesho na muongozo wa matibabu ya binti huyu .

Asanteni.
Mtu anaimwa hivyo unampeleka kwenye zahanati. Labda ungejitahidi umpeleke hospital kubwa kabisa apate matibabu sahihi
 
Mkuu poleni sana kwa kuuguliwa na bint yenu. Jaribu kumuuliza katika pitapita zake hajawahi kumangamanga na mume wa mtu? Usije na jibu kwamba bint ni mdogo.
Hapo ni kipengere si unajua mambo ya gizani chief
 
Inasikitisha sana kusikia kuhusu ha Kutokana na maelezo uliyoyatoa, dalili hizo zinashabihiana na baadhi ya magonjwa ya zinaa (STD), ingawa inaweza kuwa kitu kingine pia.
Hali hiyo ya kuwa na malengelenge au vipele vikubwa, na ile hali ya nyama ya ndani ya uke kuchomoza, na maumivu makali kama ya kuungua moto, pamoja na kutoka majimaji, ni dalili zinazoweza kuhusishwa na:
* Kaswende (Syphilis): Ingawa dalili za awali za kaswende ni vidonda vidogo visivyo na maumivu, katika hatua za baadaye, inaweza kusababisha vidonda vikubwa na vya kutisha.
* Malengelenge ya sehemu za siri (Genital Herpes): Hii husababisha vipele au malengelenge yanayojaa maji ambayo hupasuka na kuacha vidonda vyenye maumivu makali, na mara nyingi husababisha hisia ya kuungua au kuwasha.
* Chancroid: Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria ambao husababisha vidonda vikubwa, vyenye maumivu kwenye sehemu za siri.
Ushauri wa Kitaalamu
Kwa kuwa kituo cha afya na zahanati wameshindwa kutambua ugonjwa, ni muhimu sana kumpeleka binti huyo hospitali kubwa ya rufaa au kwa daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi (Dermatologist) au magonjwa ya wanawake (Gynecologist) haraka iwezekanavyo. Katika hospitali hizo, wanaweza kufanya vipimo maalum vya maabara kama vile vipimo vya damu na kuchunguza majimaji kutoka kwenye vidonda ili kubaini chanzo cha tatizo.
Kujua jina halisi la ugonjwa ni hatua ya kwanza muhimu sana. Baada ya kujua ni ugonjwa gani, ndipo matibabu sahihi yataweza kutolewa, ambayo yataondoa maumivu na hatimaye kumponya kabisa.
Usipoteze muda, tafadhali msaidie apate rufaa au umpeleke hospitali kubwa ambapo atapata utambuzi sahihi na matibabu stahiki.
Chatgpt ni zaidi ya doctor ukiitumia vizur ...... asante mkuu pia? Ndo uzuri wa chat gpt kusaidia watu
 
iyo ya waume za watu naskia ina wakuta sana wasichana unapigwa juju ni mwendo wa period non stop nasikia ilimkuta demu mmoja tulikuwa tunapiga naye job ,mtaalamu alimuokoa
Ni kweli ht me ukiingia anga zangu nakunyoosha ,mi SI shei dudu 😂sicjeki na wowowte
 
Ugonjwa huo unatibika vizuri kabisa.
Mpeleke hospitali kubwa siyo hivi vizahanati au vituo vya Afya!
Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Kna sehemu nyingine sijui watu wanaishije. Zahanati ni sehemu sahihi ya kupeleka mtu kama huyu? Si ajabu hata hayo madawa ya UTI aliyopewa ndiyo yamemfanya augue. Apelekwe hospital kubwa haraka.
 
Mpelekeni fasta, pia ugonjwa kwa yoyote ambao mnaona clinic au hospital ndogo haiwezi tatua muhimu sana kupeleka hospital kubwa. Awape barua kuonyesha amekuwa anatibiwa tayari n.k.

Mola amponye upesi
Somesha mwanao apate elimu sahihi kama una uwezo. Mtu anatibiwa zahanati halafu anashangaa wameshindwa kujua ugonjwa? Magonywa mengine unapita hata hospital kubwa tatu ndiyo yanagundulika.
 
Habari wana jamii.

Nahitaji msaada wa ugonjwa ambao umempata binti ambaye ni mtoto wa rafiki yangu mwenye umri wa miaka 18.

Binti huyu ameugua ugonjwa ambao umeshindwa kutambulika ni ugonjwa gani. Alianza kwa kuugua tu kawaida alipoenda kupima afya akagundulika ana U.T.I na malaria. Baada ya tiba hali ilibadilika akapata upele mfano wa vipele vya tetekuwanga hali ikabadilika akawa ni mtu ambaye analia kwa kuugulia maumivu

Mabadiliko yakazidi kuwa makubwa mpaka sehemu za siri ambapo binti kwenye nyeti zake katokwa na mapele makubwa mfano wa yale mapele yanayopatikana ukiwa umenyoa nyeti kwa wembe kibaya zaidi nyama ya ndani ya uke imechomoza kutoka nje na anatokwa na maji mengi mfano ya jasho hayatoki kwa wingi kama period ila yanatoka kwa taratibu yeye mwenyewe anadai kusikia maumivu anayoyapata ni kama anaungua moto kwenye uke tumejaribu kumpeleka kituo cha afya wameshindwa kuutambua ni ugonjwa gani kwa sasa yupo zahanati japo mpaka sasa hatujui ni ugonjwa gani ana unasababishwa na nini na tiba yake ni ipi kwa yoyote mwenye kuufaham ugonjwa huu atupe mrejesho na muongozo wa matibabu ya binti huyu .

Asanteni.
Habari, Kuna mtaalamu kaniomba nitoe ushauri kuhusiana na hili swala, " ampeleke mtoto huyo hospital achunguzwe bakteria wa mafua watakuwa wameingia kwenye cell nyeupe za damu, hilo limekuwa tatizo kubwa la watoto wengi wa umri huo na mara nyingi hospital huwa zinashindwa kulitambua hiyo Hali kwenye sehemu za siri ni hao wadudu wanashambulia,
Kama atakuta ni hao bakteria utamwambia anicheck nimwandikie dawa maana wengi huwa wanapewa dawa ambayo haimalizi tatizo hilo"
Mimi niongezee kwa kusema kwa yote hayo uliyoshauriwa, yatekeleze kwa kwenda hospitali kubwa yenye uhakika wa vipimo vyote na upime hili pia. Pole kwa changamoto
 
Back
Top Bottom