Binti aua mwanaye kwa kumtumbukiza kwenye ndoo ya maji

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Siku moja tangu Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 aitwae Johari Twaha, Mkazi wa mtaa wa Kigamboni Mkoani Iringa akamatwe na Polisi kwa tuhuma za kumtumbukiza kwenye ndoo ya maji ya lita ishirini na kumuua Mtoto wake mwenye umri wa miezi saba, Polisi wamesema Johari aliua Mtoto ili aende Dar es salaam kutafuta maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo amesema Johari alimuua Mtoto kwasababu alikuwa anataka kwenda Dar es salaam kwa Baba yake kwa ajili ya kutafuta maisha.

"Huyu Binti alimuua Mtoto kwasababu Baba yake huyu Binti (Babu wa Mtoto) yupo Dar es salaam kwahiyo aliitwa na Baba yake kwenda Dar es salaam kwa ajili ya kuhangaika na maisha yeye anasema Iringa maisha ni magumu yamemshinda kwahiyo Baba yake alimpa masharti kuwa aende Dar es salaam bila Mtoto”

Johari alitekeleza mauaji hayo November 19,2023 saa tano katika eneo la Mawelewele Mkoani Iringa kwa kumtumbukiza mwanaye kwenye ndoo iliyopo chooni kichwa chini miguu juu na kusababisha kifo chake.
 
Binti miaka 19,babu anawezakuwa ana 38 kwa akili hizo.

Sasa mwanao ana mtoto wa miezi 7 unasema asije naye,amwachie nani!!!au alikuwa na ratiba ya kuja kumkaza!!!
 
Kila siku nawambia kuweni makini na mimba zisizo tarajiwa,acheni kuzini hovyohovyo,baba kama angewajibika kumlea mtoto wake haya yasingetokea
Inauma mtoto kudhulumiwa uhai wake
 
Sasa kama aliambiwa asiende na mtoto ndio amuue siangefanya kama wenzie wanawatelekeza hata kwenye nyumba za watu au nyumba za ibada 😪
 
Polisi wamesema Johari aliua Mtoto ili aende Dar es salaam kutafuta maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…