Binti kamaliza form 6 na ndoto za kusomea udaktari kwa matokeo ya Division 1 ya 9; Physics C, Chemistry C, Biology C, Maths C, amekosa mkopo

Nimetumia akili ndio maana nikaja kwa wenye ujuzi zaidi yangu maana hakuna anayejua kila kitu duniani

Asante kwa kunipa jibu kwamba hawezi kupata Muhas

Ila na wewe wakati mwingine utumie akili kujua kwamba kile unachokijua wewe sio kila mtu anakijua

Barikiwa BUKOBA LAND 🤝
Mwambie aombe chuo ambacho ni Cha Serikali
Ambacho kitaendana na ufaulu wake
Then akamilishe taratibu zote za uombaji mkopo 2022/2023

Ikitokea kwa bahati kakosa mkopo ndo utupatie Bandiko maana hapa wengi tunazo namba za watu wa Helsb hope atasaidiwa
 
Habari za jioni wakuu mabibi na mabwana

Huyu binti namfahamu tangu akiwa mtoto. Anatoka kwenye mazingira magumu kuliko ngumu wenyewe.

Hamjui baba yake mzazi, hajawahi kumsikia wala kumuona.

Mazingira ambayo mama yake hawezi kumiliki hata simu ya elfu20, hawezi lipa kodi vyumba2 vya elfu 60 uswahilini kwetu huku, hana uhakika wa kulisha watoto wake milo miwili kwa siku lakini amepambana hadi binti kafika kidato cha sita kwa msaada wa serikali na amepata hayo matokeo hapo.

Alipofaulu kidato cha nne kwenda kidato cha tano mkoani hata nauli wachana na Ile ada ya elfu70 ya Magufuli ilikua shughuli kubwa. Wakati wa kufunga shule ndio ilikua hadi walimu wapige simu kwa namba atakazowapa za ndugu na jamaa ndio arudi njiani. Yaani kwa kifupi amekua kwenye mazingira magumu nyakati zote shuleni na nyumbani

Pamoja na kuwa amesoma shule zetu za serikali tangu chekechea hadi kidato cha sita na matokeo yake ni hayo hapo, amejitahidi kadri ya uwezo wake kwa lengo la kuja kusomea masomo ya utabibu kama udaktari au maana ya lakini leo nimeumia kidogo baada ya kumkuta kajikunyata kwa huzuni baada ya kukosa ufadhili au mkopo wa serikali kwa kozi hizo ambazo ada zake zipo juu

Nimewaza nikaona nije hapa jukwaani kwa wajuzi wa mambo maana najua hapa kuna wazoefu, walimu, wasomi, washauri, wazazi wenye mapenzi mema labda Huyu binti anaweza saidika

Mtoto wa mwenzio no mtoto wako, natanguliza shukrani

Nawasilisha[emoji1666]

Cc Dada Ummy Wizara ya Afya Tanzania

Hiyo ilikuwa combination gani yenye Maths C? Manake Maths alisoma BAM sasa inakuwaje BAM iwe na credit badala ya S au F? Huyu kawaingiza chaka jamani, mpuuzeni.
 
Mwambie aombe chuo ambacho ni Cha Serikali
Ambacho kitaendana na ufaulu wake
Then akamilishe taratibu zote za uombaji mkopo 2022/2023

Ikitokea kwa bahati kakosa mkopo ndo utupatie Bandiko maana hapa wengi tunazo namba za watu wa Helsb hope atasaidiwa

Kwa maana hiyo nimwambie aachane na mambo ya ufamasia au udaktari. Niko sawa!?
 
Ada ya kairuki unajua ni sh ngapi hivi Kama unasema Ni mtoto wa maskini then unataka asome kairuki I guess unata ku-bury dreams za huyo dogo

Kujua wewe nipe ushauri kadri ya maelezo niliyotoa. Kusema ukweli Mimi mambo ya helb siyajuagi kabisaaa
 
Nimesoma chuo lakini mambo ya mkopo siyajuagi sikuwahi bahatika kukopeshwa
Aombe tena chuo batch two
Then uo ufaulu wake wa 1.9 Ni Mdogo Sana kwa course ya Udaktari Kupata nafasi

So aombe courses ambayo atapata nafasi ya kusoma degree

Pia mkopo Kupata lazima Apate maana Hadi muda hakuna Form leaver ambaye kashajua kuwa kapata mkopo au kakosa sasa wewe umea-Adress kuwa kakosa mkopo wakati allocation hazipangwa ! Hapo umezua taharuki
 
Habari za jioni wakuu mabibi na mabwana

Huyu binti namfahamu tangu akiwa mtoto. Anatoka kwenye mazingira magumu kuliko ngumu wenyewe.

Hamjui baba yake mzazi, hajawahi kumsikia wala kumuona.

Mazingira ambayo mama yake hawezi kumiliki hata simu ya elfu20, hawezi lipa kodi vyumba2 vya elfu 60 uswahilini kwetu huku, hana uhakika wa kulisha watoto wake milo miwili kwa siku lakini amepambana hadi binti kafika kidato cha sita kwa msaada wa serikali na amepata hayo matokeo hapo.

Alipofaulu kidato cha nne kwenda kidato cha tano mkoani hata nauli wachana na Ile ada ya elfu70 ya Magufuli ilikua shughuli kubwa. Wakati wa kufunga shule ndio ilikua hadi walimu wapige simu kwa namba atakazowapa za ndugu na jamaa ndio arudi njiani. Yaani kwa kifupi amekua kwenye mazingira magumu nyakati zote shuleni na nyumbani

Pamoja na kuwa amesoma shule zetu za serikali tangu chekechea hadi kidato cha sita na matokeo yake ni hayo hapo, amejitahidi kadri ya uwezo wake kwa lengo la kuja kusomea masomo ya utabibu kama udaktari au maana ya lakini leo nimeumia kidogo baada ya kumkuta kajikunyata kwa huzuni baada ya kukosa ufadhili au mkopo wa serikali kwa kozi hizo ambazo ada zake zipo juu

Nimewaza nikaona nije hapa jukwaani kwa wajuzi wa mambo maana najua hapa kuna wazoefu, walimu, wasomi, washauri, wazazi wenye mapenzi mema labda Huyu binti anaweza saidika

Mtoto wa mwenzio no mtoto wako, natanguliza shukrani

Nawasilisha[emoji1666]

Cc Dada Ummy Wizara ya Afya Tanzania
Tulipomaliza form six shule yetu ilikua ya nne kitaifa na PCB wa kwanza alipiga one ya point 7,......,One ya Tisa hawezi kwa miaka hii,pata MD kwa vyuo vya serikali ambavyo ni rahisi kupata kwa uchumi wake.
Maisha hubadilika sana,kadri ya nyakati,.....
pia msihi,si kila anachotamani anaweza kukipata,,na ridhiki anapanga mwenyezimungu,na ridhiki ni kubwa zaidi ya matamanio yetu.
tulimaliza na mtu alipata 3 point 13,huyu alienda UDSM kusoma uvuvi na kufikia hadi level ya master na wakamuhitaji kufundisha akakataa,yupo anafanya kazi kwenye international firm za uvuvi biashara.
Yupo pia aliyesoma UDSM beekeeping,alikosa MD,sasa ni lecture UDSM na anapiga PhD pia.
Ajaribu kitu kingine,hakuna sehemu palipoandikwa ridhiki yake ataipata kupitia MD.
 
Asanteee
 
Back
Top Bottom