Binti kamaliza form 6 na ndoto za kusomea udaktari kwa matokeo ya Division 1 ya 9; Physics C, Chemistry C, Biology C, Maths C, amekosa mkopo

Binti kamaliza form 6 na ndoto za kusomea udaktari kwa matokeo ya Division 1 ya 9; Physics C, Chemistry C, Biology C, Maths C, amekosa mkopo

Kumbe unaweza soma udaktari ukiwana makarai kwenye physics chemistry na bioligia🤔🤔🤔🤔
 
Nahisi umechanganya mambo. Kama ameomba chuo mwaka huu nafikiri ulitaka kusema amekosa udahili kwa vyuo vya serikali maana mkopo bado hawajatoa majina ya waliopata na kukosa. Kwa ufaulu huo kupata kozi za udaktari kwa vyuo vya serikali sahau, labda vyuo binafsi ambapo hatoweza kumudu ada maana ni ghali.

Kama una lengo la kumsaidia kweli na hautaki abadili kozi basi mtafutie ufadhili mahali pengine pa kujazia patakapopungua.
 
Mkopo bado hawaja toa.. Akiomba kcmc, cuhas anapata bila ubishi

Unamaanisha kakosa mkopo upi?
 
Sijasema uongo, nimepewa maelezo nakaona sielewi heri nije kwenu kwa ushauri
Mikopo bado haijatolewa awahi kupata chuo.
Chuo ana ufaulu mzuri lakini asiweke mayai yake kwenye kapu moja. Afikirie course nyingine seriously na muda umebaki mchache. AWAHI FAST. Kuwahi kupata chuo inaongeza uwezekano wa kupata mkopo.
 
Nahisi umechanganya mambo. Kama ameomba chuo mwaka huu nafikiri ulitaka kusema amekosa udahili kwa vyuo vya serikali maana mkopo bado hawajatoa majina ya waliopata na kukosa. Kwa ufaulu huo kupata kozi za udaktari kwa vyuo vya serikali sahau, labda vyuo binafsi ambapo hatoweza kumudu ada maana ni ghali.

Kama una lengo la kumsaidia kweli na hautaki abadili kozi basi mtafutie ufadhili mahali pengine pa kujazia patakapopungua.
Hata vyuo binafsi hawezi kupata udaktari kwa Division one (point 9) kwa mwaka huu.

Halafu hii dhana ya vyuo binafsi na umma huwa nyinyi mnaipata wapi katika zama hizi za sasa?

Hivi mnaelewa jinsi udahili ulivyo tight kwenye kozi za afya zama hizi?

Yaani unaweza ukawa na division one na bado usipate chuo chochote kwa kozi yoyote ya afya mwaka huu.
 
Mkopo bado hawaja toa.. Akiomba kcmc, cuhas anapata bila ubishi

Unamaanisha kakosa mkopo upi?
Huko kote hakuna mwanafunzi mwenye division one (point 9) aliyefanikiwa kupata kozi ya udaktari mwaka huu mpaka sasa.
 
Hata vyuo binafsi hawezi kupata udaktari kwa Division one (point 9) kwa mwaka huu.

Halafu hii dhana ya vyuo binafsi na umma huwa nyinyi mnaipata wapi katika zama hizi za sasa?

Hivi mnaelewa jinsi udahili ulivyo tight kwenye kozi za afya zama hizi?

Yaani unaweza ukawa na division one na bado usipate chuo chochote kwa kozi yoyote ya afya mwaka huu.
Labda uongelee mwaka huu. Ila mwaka jana dogo alipata.
 
Huko kote hakuna mwanafunzi mwenye division one (point 9) aliyefanikiwa kupata kozi ya udaktari mwaka huu mpaka sasa.
Mdogo wangu ana hilo tatzo na yuko jeshin..cjui nimu applaie koz gan
 
Acha uongo vyuo binafsi anapata vizuri labda government
Wewe unaongea tu, mimi nina ndugu, rafiki watatu ambao mwaka jana watoto wao walikosa kozi ya udaktari baada ya kuomba karibu vyuo vyote hapa Tanzania (wawili walikuwa na Division one point 9 na mmoja ni Division one point 8), wakajipanga kwenda Ukrane kusoma kwenye intake ya March/April mwaka huu (ujio wa vita ukaharibu mipango yao) wakaamua kusubiria mwaka huu waombe upya tena vyuo vya Tanzania, na wameomba vyuo vyote vya Udaktari, round ya kwanza imetoka na wamekosa kote.

Mzazi mmoja kajiongeza na kwenda kabisa kwenye vyuo vya KCMC na Bugando kuuliza kulikoni, akakuta mwanafunzi wa alama za chini kabisa aliyepata kozi ya udaktari alikuwa na Division one point 7. Wanataka kujaribu round ya pili.
 
Ilibidi ifike wakati hawa watoto wanaosoma kwa shida watambuliwe wapewe kipaumbele kwa mazingira yoyote yale.
Kwa mimi mtoto wa mazingira kama hayo anastahili kwenda vyuo vya serikali akasome huo udaktari licha ya alama hizo kuwa chini. Sema ndio hivyo li nchi letu linajiendea tu mradi liende
 
Back
Top Bottom