Binti Matola mwanamama shujaa aliyepinga uhuru wa Tanganyika kuwa 1971

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Historia ya Tanganyika imemficha mwanamama huyu ambaye alipingana na viongozi wa Tanu wakiongozwa na Mwalimu Nyerere na wazo la UN kuwa Tanganyika ipewe Uhuru mwaka 1971 na kushinikiza uhuru wa Tanganyika kuwa 1961 na kuleta slogan maarufu wakati wa uhuru ñi sasa.

Kuendelea kutawaliwa na waingereza kulikuwa hakuna faida kwa kuwa Waingereza walikuwa hawana mipango yoyote ya kumuendeleza mtanganyika kwa kuwa ilikuwa sio koloni ĺake kamili. Waingereza walikuwa wanapora tu mali za watanganyika
 
Mzee wetu Mohamed Said
anaweza kutusaidia zaidi kuhusu Hii Historia.Maana umeiacha na Mapengo mengi sana.Tupe wasifu kamili wa huyu Binti Matola,Makazi na kazi yake,Uhusika wake Katika Kudai Uhuru kwa kina na Vyanzo au chanzo cha Taarifa zako.
 
Lusomya,
Inakuwaje ikiwa tuna shujaa mpigania uhuru kama Bint Matola leo hatuna hata picha yake wala hajatajwa katika historia ya TANU?

Kuna mwenye jibu atupe?
 
Mzee wetu Mohamed Said
anaweza kutusaidia zaidi kuhusu Hii Historia.Maana umeiacha na Mapengo mengi sana.Tupe wasifu kamili wa huyu Binti Matola,Makazi na kazi yake,Uhusika wake Katika Kudai Uhuru kwa kina na Vyanzo au chanzo cha Taarifa zako.
Masokotz,
Mpaka leo natafuta picha ya Bi. Fatma bint Matola sijaipata.

Najiuliza kwa nini imekuwa hivi kuwa wapigania uhuru wote wamefutwa wamepachikwa watu wengine?:

Nani anajua historia za akina mama hao hapo chini waliopigania uhuru wa Tanganyika?"

Amina Kinabo
Moshi

Halima Selengia
Moshi

Lucy Lameck
Moshi


Tatu bint Mzee
Dar es Salaam

Halima Khamis
Dar es Salaam

Mwamtoro bint Chuma
Dar es Salaam

Nyange bint Chande
Tabora

Zarula bint Abdulrahman
Tabora

Sharifa bint Mzee
Lindi

Mwami Theresa Ntare
Kasulu
 

Attachments

  • 1712865259893.png
    51.8 KB · Views: 11
Washindi ndio huandika historia.
 
Washindi ndio huandika historia.
Yoda,
Washindi wameshinda nini?
'' Washindi'' wako waliandika historia lakini ndani hakukuwa na kitu.

Historia ya ''Washindi,'' leo imekuwa kichekesho.

Ndiyo kisa leo Watanzania wanauliza imekuwaje historia imeandikwa Fatma Matola hayumo?

Mohamed Said akaongeza na picha za wanawake wengi waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika lakini wamefutwa na ''Washindi.''

''Washindi'' ndio waandikao historia za uongo.
 
Pamoja na ukristo wangu naumia sana pia mchango wa uislam na waislam katika historia ya nchi yetu usivyotajwa popote. Na hata uamuzi wa waislamu kubariki mkristo Mw Nyerere kuwa kiongozi wao ndiyo chanzo cha umoja tunaojivunia leo...
 
Kwamba ulijaribu kuandika / kuiweka sawa hii Historia wino / text zikawa invisible ?

Ila haujachelewa unaweza kuleta habari zake hata leo..., bali hakuna ulazima wa kuwashusha wengine ili kuwapandisha wengine... Wote waelezewe kwa mchango wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…