Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Huyu binti kanivutia sana. Ni mbunge huko New Zealand. Ndo mbunge mwenye umri mdogo kwenye bunge la nchi hiyo. Ujasiri na uthubutu wake ni A+.
Wiki iliyopita, mnamo tarehe 14 Novemba, katika hatua ya kuupinga muswada mpya ambao unafasili misingi ya mkataba kati ya jamii ya Maori [jamii atokayo] na Wakoloni wa Kiingereza, alianza kuimba na kucheza wimbo wa “Ka Mate” huku akiichana na kuitupa karatasi ambayo muswada huo ulikuwa umeandikwa.
Wamaori wenzie ndani ya bunge nao walimuunga mkono kwa kuanza kuimba na kucheza Haka.
Wow! Ni binti wa 2002.