Binti wa kishua kanipenda ila nina mke na mtoto

Binti wa kishua kanipenda ila nina mke na mtoto

Mlundilwa Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2019
Posts
3,187
Reaction score
4,857
Buheri mazee

Ebhana majuzi kati hapa nilikua napita zangu kandokando ya barabara kwambali nikaona gari imesimama nilivyoikaribia na kuanza kuipita ghafla ilitoka pisi kali Sana ikaniita"samahani kaka" nikasema bila samahani, Gari yangu imeisha mafuta na cjatembea na akiba hivi shell Iko wapi maeneo haya nikasema kama unadumu nipe nikakuchukulie ingawa Iko mbali kidogo akasema Sina, nikamwambia nipe hela nitajua huko huko Cha kufanya ingawa alionekana kusita ila alinipa kiasi Cha elfu 20 nikaenda fasta pale shell nikajaribu kuongea na mlinzi wa pale shell anisaidie kidumu bahati nzuri akanipatia kidumu Cha ltr5 nikampoza buku2000 Kisha nikaenda kupimiwa mafuta.

Nikachukua bodaboda ili aniwaihishe fasta tulipofika pale alipo yule binti alivyoniona tuu alitoa tabasamu murua na kusema nilidhani utaingia mitini si unajua Imani imekwisha sikuizi, nikasema hata kama ningekimbia na elfu 20 yako isingefanya niwe bakheresa shida zingebaki pale pale tuu, akasema nikweli ila nivijana wachache Sana wenye mawazo kama yako.

Basi akaweka Yale mafuta hatimae akawasha kitu kikakubari akanishukuru pia akanipa albino mmoja aisee kwakua nilikuwa nimepigika kutwa nzima nilishukuru Sana kwani nilipata pakuanzia kwa mama watoto, basi akaniomba na namba za simu nilisita kumpa ila ikanilazimu tubadirishane namba.

Zikapita Kama siku mbili akanipigia tukaongea mengi Sana ila kubwa alinisifia Sana kwa ukarimu na uaminifu wangu kisha akaniomba nitenge siku tukutane ili tufahamiane zaidi.

Sasa wakuu Mimi Nina mke na huyu manzi kaonyesha kunielewa na ukicheki kwao Wana mawe daah najuta kuoa mapema asa sijui nifanyeje ili ala ikae panga mbili na sijamwambia kuwa Nina mke namtoto.
 
Buheri mazee

Ebhana majuzi kati hapa nilikua napita zangu kandokando ya barabara kwambali nikaona gari imesimama nilivyoikaribia na kuanza kuipita ghafla ilitoka pisi kali Sana ikaniita"samahani kaka" nikasema bila samahani,
Acha u Nyandindi, yaani mtu akikuomba tu mtoke tayari unaona kakupa mwandu? Baaaah bwana wewe bahh.
 
Buheri mazee

Ebhana majuzi kati hapa nilikua napita zangu kandokando ya barabara kwambali nikaona gari imesimama

Usichukulie kama ndo kakupenda kimapenzi, inawezekana kwa kitendo chako cha uungwana anataka kukupa dili ila wewe unawaza tu chini.

Nakushauri ukutane naye na uwe mstaarabu tu usikimbilie kuongea ujinga, yeye ndo ameomba muonane, mpe nafasi aongoze mjadala.

Kama akiamua kukutunuku ngozi, tesa kucha hasa. Mjini msingi kiuno pia akikupa dili, baki na uungwana na uaminifu. Usimuangushe
 
Buheri mazee

Ebhana majuzi kati hapa nilikua napita zangu kandokando ya barabara kwambali nikaona gari imesimama nilivyoikaribia na kuanza kuipita ghafla ilitoka pisi kali Sana ikaniita"samahani kaka" nikasema bila samahani,
Acha tamaa na upumbavu utakuja vunja familia yako na kulia kama mbwa koko kwa upumbavu wako
 
Back
Top Bottom