Binti wa kishua kanipenda ila nina mke na mtoto

Acha u Nyandindi, yaani mtu akikuomba TU mtoke tayari unaona kakupa mwandu? Baaaah bwana wewe bahh.
Hahaaa umenichekesha na kunikumbusha mengi sana.
Mosi bifu la Philipo Nyandindi a.k.a O-Ten mshamba wa Moro akajiunga na watoto wa East Coast Upanga akina AY akaukataa ubini wake.
Afande Sele akamchana kwenye wimbo.

Pili umeongea kiswahili cha 'Ntwara' a.k.a Mtwara Mwandu kwa maama ya Mbunye au kipochi manyoya... na msemo wa 'bhaaa'ni kimakonde zaidi... wewe utakuwa mhenga kijana wa late 90s hadi early 2000s.
 
Buheri mazee

Ebhana majuzi kati hapa nilikua napita zangu kandokando ya barabara kwambali nikaona gari imesimama nilivyoikaribia na kuanza kuipita ghafla ilitoka pisi kali Sana ikaniita"samahani kaka" nikasema bila samahani, Gari yangu imeisha mafuta na cjatembea na akiba hivi shell Iko wapi maeneo haya nikasema kama unadumu nipe nikakuchukulie ingawa Iko mbali kidogo akasema Sina, nikamwambia nipe hela nitajua huko huko Cha kufanya ingawa alionekana kusita ila alinipa kiasi Cha elfu 20 nikaenda fasta pale shell nikajaribu kuongea na mlinzi wa pale shell anisaidie kidumu bahati nzuri akanipatia kidumu Cha ltr5 nikampoza buku2000 Kisha nikaenda kupimiwa mafuta.

Nikachukua bodaboda ili aniwaihishe fasta tulipofika pale alipo yule binti alivyoniona tuu alitoa tabasamu murua na kusema nilidhani utaingia mitini si unajua Imani imekwisha sikuizi, nikasema hata kama ningekimbia na elfu 20 yako isingefanya niwe bakheresa shida zingebaki pale pale tuu, akasema nikweli ila nivijana wachache Sana wenye mawazo kama yako.

Basi akaweka Yale mafuta hatimae akawasha kitu kikakubari akanishukuru pia akanipa albino mmoja aisee kwakua nilikuwa nimepigika kutwa nzima nilishukuru Sana kwani nilipata pakuanzia kwa mama watoto, basi akaniomba na namba za simu nilisita kumpa ila ikanilazimu tubadirishane namba.

Zikapita Kama siku mbili akanipigia tukaongea mengi Sana ila kubwa alinisifia Sana kwa ukarimu na uaminifu wangu kisha akaniomba nitenge siku tukutane ili tufahamiane zaidi.

Sasa wakuu Mimi Nina mke na huyu manzi kaonyesha kunielewa na ukicheki kwao Wana mawe daah najuta kuoa mapema asa sijui nifanyeje ili ala ikae panga mbili na sijamwambia kuwa Nina mke namtoto.
Hauna picha yake maana hata nami kuna binti wa kishua ananimaindi.......ebu tuwekee tumuone!
 
Nenda kamsikilize kwanza , mahusiano kati ya mwanamke na mwanamme sio kila siku ni mapenzi
 
Buheri mazee

Ebhana majuzi kati hapa nilikua napita zangu kandokando ya barabara kwambali nikaona gari imesimama nilivyoikaribia na kuanza kuipita ghafla ilitoka pisi kali Sana ikaniita"samahani kaka" nikasema bila samahani, Gari yangu imeisha mafuta na cjatembea na akiba hivi shell Iko wapi maeneo haya nikasema kama unadumu nipe nikakuchukulie ingawa Iko mbali kidogo akasema Sina, nikamwambia nipe hela nitajua huko huko Cha kufanya ingawa alionekana kusita ila alinipa kiasi Cha elfu 20 nikaenda fasta pale shell nikajaribu kuongea na mlinzi wa pale shell anisaidie kidumu bahati nzuri akanipatia kidumu Cha ltr5 nikampoza buku2000 Kisha nikaenda kupimiwa mafuta.

Nikachukua bodaboda ili aniwaihishe fasta tulipofika pale alipo yule binti alivyoniona tuu alitoa tabasamu murua na kusema nilidhani utaingia mitini si unajua Imani imekwisha sikuizi, nikasema hata kama ningekimbia na elfu 20 yako isingefanya niwe bakheresa shida zingebaki pale pale tuu, akasema nikweli ila nivijana wachache Sana wenye mawazo kama yako.

Basi akaweka Yale mafuta hatimae akawasha kitu kikakubari akanishukuru pia akanipa albino mmoja aisee kwakua nilikuwa nimepigika kutwa nzima nilishukuru Sana kwani nilipata pakuanzia kwa mama watoto, basi akaniomba na namba za simu nilisita kumpa ila ikanilazimu tubadirishane namba.

Zikapita Kama siku mbili akanipigia tukaongea mengi Sana ila kubwa alinisifia Sana kwa ukarimu na uaminifu wangu kisha akaniomba nitenge siku tukutane ili tufahamiane zaidi.

Sasa wakuu Mimi Nina mke na huyu manzi kaonyesha kunielewa na ukicheki kwao Wana mawe daah najuta kuoa mapema asa sijui nifanyeje ili ala ikae panga mbili na sijamwambia kuwa Nina mke namtoto.
Kasema utenge siku mfahamiane zaidi wewe unasema kakupenda.....upo sawa kweli wewe au wewe ndio umempenda
 
Back
Top Bottom