Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau...

Nimekutana na habari ya Nancy Lema wa Mwanza nikaona ku-share nanyi wadau mtoe maoni.. je binti yupo sahihi au wrong?

Kafanya Shahada yake St Marys University of Minnesota na masters university of Minnesota huko USA.

Baada ya kumaliza masomo yake akaamua kurudi nyumbani kujiajiri kwa kuuza makande kisasa na kwao ni mambo safi hasa hasa...

Nawaza tu why dada zetu maskini hawapendi kujishughulisha huku washua hawachagui kazi.

Nimemkumbuka na Mercy Kitomari Nelwa Gelato naye ana degree ya U.K ila amerudi Tanzania anauza ice cream tu kisasa

 
Mimi nna degree ya SAUT nachoma mahindi hapa darajani hapa Mbeya.Huyo hafanyi biashara anajitangaza,tupo wengi huku tunatokea kwenye familia maskini mnoooo nadhani ndiyo maana hamtutangazi.....HAKUNA MTU HAPENDI KUFANYA KAZI,HAKUNA MTU ANAPENDA KULA BURE,SHIDA NI MTAJI NA KUPATA KAZI YENYEWE.
 
Ni vizuri kukosoana ila kwanini nisichague kazi? Swali langu la msingi ni kwanini watu tunawabana hadi kwenye kuchagua kazi.

-Acha watu wawe wanavyotaka wawe nawe kuwa unayetaka kuwa.

Hii dunia ipo fair saana.
 
makande yanahitaji mtaji kiasi gani?wabongo kwa visingizio
Wewee, hivi unadhani alichukua tu mahindi na maharage akapika makande wateja wakaja? Yaani napata picha hapa uswahilini kwetu nipike tu makande watu waje kula? Kwanza jina lake tu ni mtaji tosha, umeenda kuangalia hayo makande anayauzia sehemu gani? Anayapikaje? Anayapack vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuna nini huko marekani watu wasirudi kuuza kande home kwao,ulitaka auze KFC au MacDonald.
 
Kuna jamaa alikataa mshahara wa USA akarudi bongo akafungua ofisi mwaka jana ofisi yake ikashirikia shindano ikashinda zaidi ya 200M.

Huyu dada, Degree na Master ya Nje. Anauza makande.

Mimi sidhani kama mtu kufanya biz ya chini inatakiwa ihesabiwe kama inspiration kwa job seeker. Alitakiwa atuonyeshe tofauti yake kama huyo jamaa aliyekataa ule mshahara.

Hapa Tz tayari tuna degree holder anauza uji mwingine anauza mihogo. Yaani ni kwamba degree na master ya nje imewaza sawasawa na degree ya bongo jua kali.
 
Unaandika tu kirahisi anauza makande. Kama ambavyo mtu anaweza kuandika kirahisi Bakhresa anauza ice cream au unga wa ngano na tui la nazi.
 

vipi angeajiriwa kfc auze makande au chips za mwajiri wake.. ungemuona mjanja ??
 
Nimejifunza kitu kwa huyu dogo, kwanza kupika ni passion yake hicho ni kitu muhimu kabisa, pili amejua kusudi lake na analifanyia kazi kwa udanisi na furaha (Nanauka anasema tambua kusudi lako) tatu, anafanya biashara ya kuuza chakula na kunasiku maalumu anapika makande, nampa hongera kwa kujua kusudi lake, elimu alikua anapuyanga tu bora angesomea upishi mapema, lakini hajachelewa. So muandishi anasema eti kaamua kupika makande!?!??!?! Halafu tunaanza kulaumiana?!! Wasomi wa nchi hii wako confused kabisa! Jua kusudi lako basi. Sio kudanganyana msomi anapika makande na anatoboa, huyo anafanya biashara ya chakula na kuna siku ya makande, akijiongeza atapika na ugali was mtama. Hongera dogo kwa kujua kusudi lako. Sijapenda heading ya uzi imekaa kibiashara sana
 
Well done Nancy! Hii itakuongeza wateja. Achana na wanaokebehi, ni masembo.

Long term plan iwe ni pamoja na kuanzisha branches Dar, Arusha, Mbeya na Dodoma. Baada ya hapo ni franchise kwa kwenda mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…