Binti wa TB Joshua kuolewa Arusha

Jumamosi ntaenda moyo safi kuushuhudia hii harusi
 

Mkuu TheChoji salam. Bwana Harusi alikuwa mmojawapo wa "Evangelist" pale SCOAN ambapo Bibi Harusi ni Mwanasheria. https://www.nairaland.com/2862381/serah-joshua-promise-joshua-tb.

Sasa kwanini hao vijana wanaoana Tanzania katika Kanisa la RC ni siri kubwa sana ambayo ni "Insiders" wa SCOAN ndio wanaoweza kuieleza. Ukiangalia pale SCOAN Evangelist wengi kama sio wote ni "Single" na kuna "Notion" imekuwa ikisemwa kati yao kuwa walioamua kwenda kuoa au kuolewa wamekuwa "Backsliders". kuna Dereva fulani mashuhuri kwa kuwabeba wageni wa SCOAN ambaye alishawahi kuniambia kwamba yamkini hata Evelyne Joshua (Mrs T.B Joshua) hana furaha (haifaidi sana) na ndoa yake kutokana na muda mwingi ambao Prophet T.B Joshua anautoa (Dedicate) kwa mambo ya huduma.

Ukiangalia hizo picha ina maana hao tayari ni Maharusi baada ya kufunga ndoa ya kimila. Je T.b Joshua ameridhia hiyo ndoa au maharusi walifanya uzinzi wakafukuzwa kanisani hilo ni Jambo ambalo tunaweza kulifahamu hapo baadaye.

Ahsante
 
kuna watu wanazaliwa hadi wanakufa hawajawahi kuonja shida..
wanaziskia tuu shida shida hawajui hata zinafananaje.
na ahera ukienda unaona wanaingia peponi we unatupwa motoni
Nakuambia hiyo siku ya kiama utaibuka ubishi mkali sana kama yatafanyika mambo ya upendeleo kama hayo. 😁😁
 
waweke harusi yao YouTube tusikie maneno ya tb Joshua
 
Mkuu vp unaweza kwa bahati ukajaaliwa kuwa na namba ya huyo binti na Mungu akubariki?
... eti Mungu akubariki; ha ha ha! nenda kule Jamii Photos (ule uzi wa Special Thread sijui Beautiful Ladies Worldwide) ukajitwalie misambwanda kule; usitake kuharibu watoto waliolelewa kimaadili.
 
... eti Mungu akubariki; ha ha ha! nenda kule Jamii Photos (ule uzi wa Special Thread sijui Beautiful Ladies Worldwide) ukajitwalie misambwanda kule; usitake kuharibu watoto waliolelewa kimaadili.
Hawa waliolelewa vizuri ndio watam mkuu 😂
 
TB Joshua akija,sherehe itageuka kuwa spritual conference.Maana najua kuna wenye shida ya kiroho waliochangia hiyo ndoa kwa lengo la kukutana na upako wa wa T.B.Joshua
 
Mbona mzigo wa kawaida sana, kama Wanaija wenyewe wameususa pamoja na mimali yote hiyo basi huyu meku atakuwa ameona fursa, ila asisahau ya Ben Paul, kuolewa na mtoto wa kishua jua ndugu zako pamoja na wazazi wako watakuwa kama mashamba boy tu.
... hekaya za mswahili!
 
Yaani kweli unategemea bia kwenye Harusi ya TB Joshua?
Upo timamu kweli
 
kwahiyo binti ni RC siyo wa dhehebu la dady,sasa wazee wa machimbo fursa zimefunguka kwenda Niger delta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…