GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Sikuwa nakifahamu! Lakini miaka michache baada ya kusikia kikielezewa, nilifanikiwa kukila.
Mara yangu ya kwanza kuila ilikuwa ni Jumatatu, 28/06/2021, Zanzibar, kwenye mghahawa uitwao ZANZI BBQ. Mghahawa upo pembezoni mwa barabara inayoelekea Airport. Nafikiri unamilikiwa na Mhindi.
Lakini baada ya kurudi Tanganyika, imekuwa ni nadra sana kukipata hicho chakula kwenye mighahawa ya kawaida.
Mghahawa pekee ninaoufahamu
Mwanza unakoweza kupata Biriyani ni Baraka Cafe iliyopo maeneo ya Natta jijini Mwanza. Changamoto yake ni kwamba siku pekee ya kuweza kupata hicho chakula hapo Baraka Cafe ni Ijumaa.
Tokea mwaka 2021, nimeshakula Biriyani mara kadhaa. Ni kizuri. Ni kitamu. Japo niliyoila Zanzibar, kwa mujibu wa mtazamo wangu, ni nzuri zaidi kuliko niliyoila hapa Tanganyika. Hata hivyo, ni nzuri kuliko pilau.
Ni kwa nini chakula kizuri kama
hicho ni nadra kupatikana?
Kwa nini baadhi ya mighahawa Biriyani hupatikana siku ya Ijumaa pekee?