Biriyani: Chakula kitamu lakini adimu

Pilau nayo ilikuwa inapikwa ikulu tu miaka ya nyuma!!😂😂

Hiyo biriyani itakuwa mtaa tu spoon😂😂😂
Kwa nini baadhi ya mighahawa hiyo huduma hupatikana Ijumaa pekee?
 
Hua nakula nyumbani,kama umeoa mwambie mkeo akupikie...kwa sasa wanawake wanajifunza mapishi kwenye mitandao na wanaweza wakapika vizuri kabisa.
 
kuna wamama mtaani wako vizuri sana kwenye kusuka biriani
nikiwa na hamu namkodi, ananipikia cha siku kadhaa, mchele wa kawaida siyo basmat(mchele feki)
Huwa najiuliza mfano mchele super wa Ifakara au kyela huwa haufai kupikia biriani mpaka hiyo basmati?
 
Kwa hapa DSM nimekula sehemu 5 tofauti, kuna Mgahawa upo pale Salamander Tower, Mwingine upo pale TPA HQ, Risa BBQ pale Lumumba na Sinza mgahawa fulani hivi, ila kwa SELE BONGE KINONDONI ndo pameshindikana *****, yule mwamba ana balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…