Akaeleza kwamba hapo mwanzo, dunia yote ilikuwa ni Taifa moja, yaani nchi moja yenye lugha moja na usemi mmoja, lakini baada ya umoja wao kuzaa uasi wa Babeli, Mungu alichafua usemi wao ili wasisikilizane wao kwa wao, ndipo yalipozaliwa makabila na lugha nyingi, na wakashikamana katika makabila na lugha hizo, na kutawanywa katika dunia yote (MWANZO 11:1-9). Kilichofuatia, Mungu alianzisha nchi mbalimbali, zenye lugha mbalimbali, na kuwawekea mipaka ya nchi zao. "Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao." (MWANZO 10:5).