BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

mkuu punguza jazba tayar bishop mokiwa ameshafunguka

Nina hasira sana, na mtetemela, Diocese yetu ya victoria nyanza imekufa kabisa kwa sababu yake , tulikuwa tunamwita aje kutusuruhisha migogoro ya diocese yetu , na tunamwambia kuna hili ..na ..hile , lakini wanapokaa
vikao vya faragha anapewa rushwa, asubuhi anapanda ndege huyoooo, na tulimwitwa mara mbili.

diocese iko tabani kabisaaaaaaaaa ,
 
Viongozi wa dini, mnaelekea kuhubiri miti sasa chungeni ndimi zetu,, mamlaka za kidunia zitatangamana zenyewe kwa zenyewe.
 
Hata yesu aliuwawa mikononi mwa watawala wakishindwa kuitetea kweli na kulinda vyeo vyao.. Nawashangaa wakiristo wanao itetea serikali yenye maovu lukuki
 
Akaeleza kwamba hapo mwanzo, dunia yote ilikuwa ni Taifa moja, yaani nchi moja yenye lugha moja na usemi mmoja, lakini baada ya umoja wao kuzaa uasi wa Babeli, Mungu alichafua usemi wao ili wasisikilizane wao kwa wao, ndipo yalipozaliwa makabila na lugha nyingi, na wakashikamana katika makabila na lugha hizo, na kutawanywa katika dunia yote (MWANZO 11:1-9). Kilichofuatia, Mungu alianzisha nchi mbalimbali, zenye lugha mbalimbali, na kuwawekea mipaka ya nchi zao. "Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao." (MWANZO 10:5).
 
Ikiwa watu wanadai muundo wa Serikali tatu ili kupata Tanganyika huru, siungi mkono hilo. Na ikiwa watu wanadai Serikali mbili ili kupata Zanzibar huru au ili Tanzania bara iendelee kuonekana kujitawala Zanzibar pia siungi mkono. Muungano unazaa nchi moja lakini mfumo/muundo wa utawala unaweza kuainishwa itakavyokubalika.
 
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa

Ikiwa ulichoandika ni sahihi, unadhani ni kwa nini ndani ya bunge la kutunga katiba limejuisha maaskofu, mashehe na wachungaji kutoka dini na madhehebu mbalimbali??? kwanini wasingeachwa ili katiba itungwe na wanasiasa pekee????
 
Aliendelea kuelezea kwamba, kazi ya kugawa nchi hizo, ilikuwa kama kugawa urithi kwa kila mmoja. Nchi ni urithi waliopewa wananchi wa nchi husika (KUTOKA 6:8; EZEKIELI 33:24). Kama ilivyo katika familia ambapo urithi wa kila mtoto, hutofautiana, huyu akapewa urithi mzuri zaidi kuliko mwingine (ZABURI 16:6), ndivyo ilivyokuwa katika kugawa urithi wa nchi. Alitoa ufafanuzi wa kina na kuelezea kwamba wanadamu waliohusika kugawa mipaka hiyo, kwa mfano "Berlin Conference 1884-1885", hao tu walitumiwa na Mungu kutekeleza mpango wake.
 
hata nabii "Samuel" alikemea maovu aliyoyafanya Mfalme "Sauli",na pia Mfalme "Daudi" kutembea na mke wa mtu,alikemewa na nabii "Nathani",naye akatubu,ila "Sauli" hakutubu akafa kifo kibaya,yupo Mfalme Ahabu alifanya mabaya kwa kumuua "Nabothi",Myzreeli,Mungu akamtuma Nabii "Eliya" amkemee kwa kitendo alichofanya,baadaye naye Mfalme "Ahabu" alikufa kifo kibaya.Leo tunahitaji watumishi wa Mungu wanaosema kweli kwa viongozi,big up Mch.Kakobe na Rev.Mtikila
 
Itabidi Askofu Kakobe amualike mh. Lukuvi ili aje abalance haya madai ya Tanganyika yetu. Itabidi watawala wetu watafute propaganda mpya, maana madai ya Tanganyika siyo ya UKAWA tu kama wanavyotaka kutuaminisha na kututishia.
 
Imefika wakati no way out lazima tupate nchi yetu ya Tanganyika then tufanye referendum ya muungano...
 
Aliendelea kusema, katika kazi ya kugawa urithi na kugawa mipaka ya nchi, Tanganyika tulipata urithi mzuri sana (ZABURI 16:6), kuliko nchi nyingi za Afrika. Akatoa mfano jinsi ugawaji wa mpaka ulivyopindisha mchoro wa ramani, kuhakikisha Mlima Kilimanjaro, unakuwa urithi wetu, na tukapewa maziwa mengi, mito mingi, bahari, na urithi mwingine mkubwa sana, tofauti na nchi nyingi za Afrika.
 
Back
Top Bottom