BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

mkuu mimi ni mdau wa serikali tatu,Wala sina chama cha siasa,katika Sakarya hili la mungano ni CCM ndio wenye msimamo wa serikali mbili,lakini ujue kuwa katika wafuasi wa kakobe na CCM wako vile vile sasa unataka kuniambia kuwa wanachama wa CCM wamkimbie kakobe

chabuso;
Naamini utanielewa kwa nini nimempenda Kakobe. Hata ccm aliyemsikiliza atajitahidi kutafakari kidogo aone chema kilichoko ndani ya serekali 3 amuunge mkono. Hatuna mahali pa kusemea hoja zetu ka si majumba ya Ibaada kama Lukuvi
 
Kabisaaaaaaa.....abarikiwe zaodi na zaidi
 
Yaani huyu Pengo majanga.. ametia aibu..
amemchukiza adi ngalalekumtwa ambae ndiye raisi wa baraza la maaskofu.. na ndiye msemaji wa kanisa.. lakini uccm wa pengo umeleta shida
 
Amesema Tanganyika huru lazima ipatikane ni
suala la muda tu
Nchi yetu imekuwa katika laana kwa muda mrefu
kwa sababu tumeshindwa kuilinda mipaka yetu
Moto wa kudai Tanganyika umewaka na hamna
mtu awezaye kuuzima. Awaonya watawala kusoma
alama za nyakati na amewataka kuiepusha nchi
kuingia katika machafuko kwa kuridhia Serikali ya
Tanganyika.
Pia amesema Nyerere sio Mungu naye ana
mapungufu yake wanaomuabudu wanakosea.
Kosa alilolifanya Nyerere ni kuruhusu kuunda
serikali hewa ya Tanzania bara ambayo kimsingi
haipo ukiliganisha na Zanzibar.
Amewaonya viongozi wanaopinga kurejeshwa
kwa Tanganyika kuwa wataitumbukiza nchi katika
machafuko.
...Hizo zilikuwa salamu za Pasaka alizozitoa leo
katika kanisa la FGBF Dar es salaam.
kwamba nchi imelaaniwa kwasababu imekataa kuitwa tanganyika?.
 
Kakobe alishawahi kusema unafiki ufuatao!
(1) Mwaka 2000 alisema Lyatonga Mrema ndie chaguo la "mungu" na ndie rais ajae WA Tanzania. [Ukweli ulionekana na Mrema alishindwa vibaya mno na mkapa]

(2) Aliiambia serikali ikiwa nyaya za umeme zikipita juu ya kanisa lake basi hazipitisha umeme. [ukweli Ni kwamba nyaya zilipita na umeme umepita juu ya kanisa lake].


Kusikiliza utabiri WA Kakobe Ni sawa na kusikiliza Utabiri wa PELE wa Brasil.

KAKOBE ACHA KUTOKWA NA MAPOVU!

Mchango wakp huu ni dalili kwamba watala wapata ujumbe wa Kakobe ndo maana wamekutuma.Sasa kabla hukawa wakili wao kuwatetea wambie wakipe mkanda wa kiti moto kilocho ongozwa na Pascal Mayalla. Kuna siri kubwa ktk mkanda ule.
UKISIKILIZA NDIPO UJE KUJIBIZANA NAMOIMI HUMU.
 
Ni mpiga kura wa hao wanasiasa .kwahiyo siasa .inamhusu

Kakobe ni bora aendelee hivyo hivyo kuwa mpiga kura kutokana na hisia zake lakini asiwabague wafuasi wake wanaotaka serikali mbili,au tuseme kakobe hana wafuasi wa CCM
 
namkumbuka na kauli zake wakati UMEME unapitishwa juuu ya madhabahu yake
 
Kakobe alishawahi kusema unafiki ufuatao!
(1) Mwaka 2000 alisema Lyatonga Mrema ndie chaguo la "mungu" na ndie rais ajae WA Tanzania. [Ukweli ulionekana na Mrema alishindwa vibaya mno na mkapa]

(2) Aliiambia serikali ikiwa nyaya za umeme zikipita juu ya kanisa lake basi hazipitisha umeme. [ukweli Ni kwamba nyaya zilipita na umeme umepita juu ya kanisa lake].


Kusikiliza utabiri WA Kakobe Ni sawa na kusikiliza Utabiri wa PELE wa Brasil.

KAKOBE ACHA KUTOKWA NA MAPOVU!

We ndio unatokwa na povu hapa kwa kusikiliza propaganda badala ya facts,

1)Hoja ya kutoa utabiri wa Mrema kuwa atakua rais ilishajadiliwa sana hapa sina haja ya kuirudia, do your homework

2)Kuhusu nyaya za umeme kupitisha umeme pale, kwa taarifa yako umeme haujawahi kupita pale, Waandisi toka UDSM waliposhindwa kutoa facts ni kwa nini kuna "VOLTAGE DROP" kwa umeme unapofika pale kwa Kakobe walishindwa kuja na majibu ya maana serikali yako tukufu ikaamua kuwaleta wajapani wafumue vile "VIKOMBE" na kuweka vipya, zoezi lilipokamilika walipopima wakauta kuna kitu wanaita "VOLTAGE SURGE" na wakashidwa kujua ni kwa nini kwa maana kila kitu kiko sawa, cha ajabu katapila lao likazima kabisa na kushindwa kufanya kazi wakaogopa wakakimbia na kuacha mitambo yao na waandishi wa habari wakapiga picha mpaka leo

Umeme haujawahi kupita pale na hautapita, mabingwa wa electronics toka JAPAN wameshindwa kujua chanzo na tangu walipoaga mpaka leo hawajarudi hata kuchukua vifaa vyao. Na JK mpaka leo hajawahi kuuzindua ule mradi ambao waliufungua kwa mbwembwe zote mbele ya kamera na umewagharimu billions 30
 
Yaani huyu Pengo majanga.. ametia aibu..
amemchukiza adi ngalalekumtwa ambae ndiye raisi wa baraza la maaskofu.. na ndiye msemaji wa kanisa.. lakini uccm wa pengo umeleta shida

mkuu pengo ni taasisi kubwa kuna kitu ataibuka achacho tu time will tel
 
This time sujui ccm na usalama wao wa taifa watamng'oa meno na kucha nani kwa maana kila kona ya nchi mambo yamebana ba watu wanataka Tanganyika na Zanzibar yao...
 
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa

Hili suala la kuchanganya dini na siasa ambalo baadhi ya watu kwa nia binafsi wamekuwa wakilipigia kelele na ukiwauliza waeleze kwenye Biblia wapi inazuia hawakuelezi!Mbaya zaidi wanalipigia kelele kwa mtu anayesema ukweli unaowagusa wao.Askofu Kakobe angesema mambo yanayowafurahisha watawala usingesikia kabisa suala la kuchanganya dini na siasa.Wapo viongozi wa dini kadhaa wanaozungumza mambo yanayowafurahisha watawala,husikii huyu amechanganya dini na siasa!.Ifikie pahala tupende kuambiwa ukweli ili tuiponye nchi na vizazi vijavyo.Tusifurahie kudanganywa hakuwezi kulijenga Taifa.Anayedhani anaweza kumnyamazisha Askofu Kakobe kwa kauli za kusema anachanganya dini na siasa ni kupoteza muda.Kwa suala la Biblia amepewa neema kubwa sana ya Mungu ya kuijua kwahiyo huwezi kumdanganya kwa porojo hizo!Soma Biblia uone jinsi watumishi wa Mungu walivyowakemea watawala walipofanya maovu.Watanzania sio matahira hivyo mnavyodhani,wanajua ngano na makapi.Kama kuna mshirikina bado anawadanganya kwamba watanzania wataendelea kuwa mazezeta kwa uchawi wake anajidanganya nafsi yake.KILA LENYE MWANZO LINA MWISHO.
 
na wewe unayeleta
tuhuma ambazo huwezi kuzithibitisha ni TAPELI! anayepinga serikali ya
tanganyika ni MHAMIAJI HARAMU!

mkuu nimeipenda sana hii sentensi "ANAYEPINGA SERIKALI YA TANGANYIKA NI MHAMIAJI HARAMU"
 
Maaskofu wote waliozungumzia habari ya katiba mpya makanisani mwao, hawajui kazi zao hapa funiani, Huyu Yesu wanaeday kafa na kufufuka siku hii ya leo hakuwahi hata cku moja kuongelea siasa. Yeye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuhubiri injili. Aliwaambia wamini wake kuwa wziheshimu mamlaka zilizowekwa hapa duniani kwani nazo zimewekwa na Mungu. Nyie maaskofu niwashari tu kwamba, ombeeni zoezi hilo lifanyike kw amani habari ya serikali 1, 2, 3.......au ya mkataba c kazi yao ombeni muendelee kupata nafasi ya kuabudu vyema
 
kwani ule mradi ulishasikia ulizinduliwa lini?
kwani kupitisha nyaya tu za umeme mpaka wazindue?.

Swali ni kwamba kuna nyaya zimepita pale?kama ndio zipo,then umeme unapita hapo.
Huyu kakobe hata mwaka 1995 alimpigia kampeni mrema akidai ndo raisi ajae,akaishia kuvuna aibu.
 
Acha udini wewe! Utaperi huo umeona wapi na hali wewe muda wote upo msikitini?

Turudi kwenye mada yenyewe "Tanganyika Huru Lazima Ipatikane".Uongo na uzushi sikuzote haulipi! Ukisikia mambo kama hayo kwa yeyote anayefikiri atajua ni uongo wa mchana kweupe.Ni tuhuma za kutunga kwa kudhani watamkwamisha Askofu Kakobe.Walishindwa,wameshindwa,wataendelea kushindwa na hawana nafasi ya kushinda milele!Kadiri wanavyoendelea kusema uongo ndivyo Mungu anavyozidi kumwinua mara elfu.Kweli ina nguvu mara nyingi kuliko uongo!
 
Kakobe alishawahi kusema unafiki ufuatao!
(1) Mwaka 2000 alisema Lyatonga Mrema ndie chaguo la "mungu" na ndie rais ajae WA Tanzania. [Ukweli ulionekana na Mrema alishindwa vibaya mno na mkapa]

(2) Aliiambia serikali ikiwa nyaya za umeme zikipita juu ya kanisa lake basi hazipitisha umeme. [ukweli Ni kwamba nyaya
zilipita na umeme umepita juu ya kanisa lake].


Kusikiliza utabiri WA Kakobe Ni sawa na kusikiliza Utabiri wa PELE wa Brasil.

KAKOBE ACHA KUTOKWA NA MAPOVU!


Lakini ndugu yangu wewe ni mtanganyika au mtanzania bara?
 
Back
Top Bottom