Wakati Nyerere anaondoka mwaka 1985 ulikuwa wapi na ulikuwa na umri gani?
Kwa tàarifa yako Nyerere aliondoka kwa kuwa nchi ilifirisika.
Ilifirisika mikononi mwake kutokana na sera zake.
Viwanda vilikuwa magofu, havikuwa na uwezo wa kuzalisha Mali, maana ni kama vilikufa.
Havikuwa na uwezo wa kununua maligafi, havikuwa na uwezo kufanya ukarabati wa majengo na mitambo. Viwanda na bàdhi ya mashirika ya uma kama RTC, BHESCO, AISCO, DARTEX, HOSCO, RETCo nk, havikuwa na uwezo hata wa kulipa mishahara wafanyakazi wake.
Suluhu ilikuwa kuviuza, wafanyabiashara wazalishe ili serikali ikusanye kodi.
Haya yalikuwa ni moja ya mashariti ya Benki ya Dunia na shirika la fedha ulimwenguni.
Ungekuwepo wakati huo usingeropoka upuuzi huu.