Biti la Trump limefanya kazi huko Gaza

Biti la Trump limefanya kazi huko Gaza

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Wiki iliyopita, tarehe 7, Januari 2025, akiwa Mar a Lago, Rais Trump alichimba biti.

Alisema kwamba ifikapo tarehe 20 mwezi hao mateka wa Hamas hawajaachiwa, basi huko Mashariki ya Kati patachimbika.

Mapema leo/ jana, imetangazwa kuwa Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano [licha ya kwamba mapigano halisi yalikuwa yashaisha maana Hamas walikuwa hawapigani kwa sababu wametandikwa vibaya mno].

Katika makubaliano hayo, Hamas na Israel watabadilishana mateka kwa awamu.

Huyu hapa Rais Trump akichimba biti. Sidhani haya makubaliano ni sadfa tu iliyotokea.

Ni matokeo ya biti la Trump kwa Hamas 🤣.

View: https://youtu.be/6RpFe9j8UpU?si=9uNmGyTKD_X9mJW-
 
IMG_7448.jpeg
 
Ni matokeo ya biti la Trump kwa Hamas
Nadhani tungetizama malengo ya kila mmoja halafu tutapata picha which is which.

Kampeni ya Israel ilikuwa na malengo makuu manne : kuitokomeza Hamas, kuwaachilia mateka, kuhakikisha Gaza haileti tishio tena kwa Israeli, na kuwarudisha wakaazi waliokimbia makazi yao Kaskazini mwa Israeli.

Israel imeshindwa kufikia malengo yake makuu, kama vile Marekani ilivyoshindwa huko Afghanistan na Vietnam.

Watu wanapaswa kuelewa: Kwa serikali kushinda dhidi ya wanamgambo kama Hamas au Hezbollah, nguvu haitoshi; unapaswa kushinda mioyo ya watu. Inabidi utoe mbadala bora kuliko hali ilivyo--katika kesi hii, Hamas. Inahitaji suluhisho la kisiasa, suluhisho la kiitikadi, sio la kijeshi. Lakini Israeli hawakushinda mioyo ya watu, kinyume chake kabisa. Israel na Marekani zilishindwa kuwaondoa kabisa kutoka Gaza--lengo lao kuu.

Hata Blinken juzi alisema Hamas imeongeza wapiganaji wengi zaidi hivi sasa kuliko walivyokuwa kabla ya vita.

Na vipi kuhusu mateka? Kuwaachilia mateka iliipaswa kuwa kipaumbele cha kwanza lakini Sio tu kwamba makumi yao bado wako mikononi mwa Hamas, lakini baadhi yao waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga ya Israeli.

Badala ya kutokomeza Hamas, Israel imejifanya kuonekana kama taifa la kihuni, na Hamas wametoka katika hali hii wakionekana kama "watetezi" wa upinzani wa Palestina.

Sisemi Hamas hawana lawama, La hasha. Lakini jibu la maelfu ya mabomu hayakuitokomeza Hamas; iliimarisha masimulizi yao. Kila bomu lililoua raia, kila mtoto aliyetolewa kutoka kwenye vifusi, kila familia iliyokata tamaa iliyoachwa bila chakula au maji-yote hayo yalivhochea mashine ya propaganda ya Hamas.

Kijiografia, sifa ya Israeli imeharibika, limebakia sasa kama taifa pariah.Nchi nyingi (kama Uhispania, Ireland, Norway..nk) zimelitambua rasmi taifa la Palestina na hata kujiunga na kesi ya afrika kusini dhidi ya israel

Sifa ya Israel Kimataifa imechafuka. Viongozi wake wanatafutwa rasmi kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wanajeshi wa IDF wamesimamishwa kote ulimwenguni. Kuna kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel na taswira yake imeharibiwa vibaya.

Kwa upande wa Palestina, ni wazi.. Gaza imeharibiwa. Zaidi ya 100k waliuawa na bado hakuna taifa la Palestina. Bado wanaishi bila utaifa chini ya vizuizi vya Israeli.

Hamas Walipata kabisa walichotaka. Walitaka kusalia madarakani, kurudisha sababu ya Palestina kuwa nchi huru, kuizuia mpango wa normalization wa Israel na Saudia na kusaidia wafungwa wa kipalestina kutoka jela.

Vita hivi vinaendea kwisha, lakini cha kusikitisha ni kwamba tatizo la Waisraeli na Wapalestina bado halijaisha. Mzozo utaendelea kwa miaka ijayo.
 
Like, are you serious? You can sit there and with a straight face claim that Hamas won?

Reeeaally? Causing unspeakable and unmitigated suffering is a win?

Okay 🤣.
 
Alisema kwamba ifikapo tarehe 20 mwezi hao mateka wa Hamas hawajaachiwa, basi huko Mashariki ya Kati patachimbika
Usitumie maneno yako. Alisema hivi "kama mateka hawatowachiwa, basi gaza patawaka moto" hakusema patachimbika.

Sasa moto umewaka wapi? Gaza au California 😁.

Gharama za kuirudisha Gaza kwenye ubora wake ni takriban usd 70b. Hasara ya moto wa marekani mpaka sasa imefikia usd 275b na bado moto unaendelea kuwaka.
 
Like, are you serious? You can sit there and with a straight face claim that Hamas won?

Reeeaally? Causing unspeakable and unmitigated suffering is a win?

Okay 🤣.
Nimeandika kwa kiswahili na umeelewa vizuri, Sasa kilichokufanya ujibu kiingereza ni nini? kutuonyesha umesoma sana au point zako zimeenda shule kwa kuwa zimeandika kizungu?

Rudia kusoma, tuliza kichwa utaelewa. ukitanguliza ushabiki itakuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa.
 
Kama wameisambaratisha hamas, kwa nn kuna negotiation? Yani mmeshaiteka nchi nzima ila hamjafanikiwa kuwapata hao mateka, then utasemaje hamas kashindwa vibaya mno!

Haya mawazo ni ya nyie fools who depend on western propagandist medias kupata mambo yanayoendelea duniani!
 
Usitumie maneno yako. Alisema hivi "kama mateka hawatowachiwa, basi gaza patawaka moto" hakusema patachimbika.

Sasa moto umewaka wapi? Gaza au California 😁.

Gharama za kuirudisha Gaza kwenye ubora wake ni takriban usd 70b. Hasara ya moto wa marekani mpaka sasa imefikia usd 275b na bado moto unaendelea kuwaka.
Wala hakusema hivyo ulivyoandika wewe. Acha uzushi.
 
Kama wameisambaratisha hamas, kwa nn kuna negotiation? Yani mmeshaiteka nchi nzima ila hamjafanikiwa kuwapata hao mateka, then utasemaje hamas kashindwa vibaya mno!

Haya mawazo ni ya nyie fools who depend on western propagandist medias kupata mambo yanayoendelea duniani!
Gaza kuna nini cha maana kilichobaki?

Israel ilikuwa inajua hao mateka walipo.

Lakini kwa vile inajali wananchi wake, iliamua kutokutumia nguvu kuwakomboa kwa sababu kufanya hivyo kungekuwa ni counterproductive.

Kwa akili yako unadhani Israel ilishindwa kui carpet bomb Gaza?

Si kila wakati kutumia nguvu ni busara.
 
Usitumie maneno yako. Alisema hivi "kama mateka hawatowachiwa, basi gaza patawaka moto" hakusema patachimbika.

Sasa moto umewaka wapi? Gaza au California 😁.

Gharama za kuirudisha Gaza kwenye ubora wake ni takriban usd 70b. Hasara ya moto wa marekani mpaka sasa imefikia usd 275b na bado moto unaendelea kuwaka.
Mungu akuzidishie hikma na uoni mkubwa wa kuwaelimisha majuha
 
Nimeandika kwa kiswahili na umeelewa vizuri, Sasa kilichokufanya ujibu kiingereza ni nini? kutuonyesha umesoma sana au point zako zimeenda shule kwa kuwa zimeandika kizungu?

Rudia kusoma, tuliza kichwa utaelewa. ukitanguliza ushabiki itakuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa.
Una inferiority complex tu.

We mwenyewe umetumia maneno ya Kiingereza ila hujioni.

Jiangalie.
 
Nadhani tungetizama malengo ya kila mmoja halafu tutapata picha which is which.

Kampeni ya Israel ilikuwa na malengo makuu manne : kuitokomeza Hamas, kuwaachilia mateka, kuhakikisha Gaza haileti tishio tena kwa Israeli, na kuwarudisha wakaazi waliokimbia makazi yao Kaskazini mwa Israeli.

Israel imeshindwa kufikia malengo yake makuu, kama vile Marekani ilivyoshindwa huko Afghanistan na Vietnam.

Watu wanapaswa kuelewa: Kwa serikali kushinda dhidi ya wanamgambo kama Hamas au Hezbollah, nguvu haitoshi; unapaswa kushinda mioyo ya watu. Inabidi utoe mbadala bora kuliko hali ilivyo--katika kesi hii, Hamas. Inahitaji suluhisho la kisiasa, suluhisho la kiitikadi, sio la kijeshi. Lakini Israeli hawakushinda mioyo ya watu, kinyume chake kabisa. Israel na Marekani zilishindwa kuwaondoa kabisa kutoka Gaza--lengo lao kuu.

Hata Blinken juzi alisema Hamas imeongeza wapiganaji wengi zaidi hivi sasa kuliko walivyokuwa kabla ya vita.

Na vipi kuhusu mateka? Kuwaachilia mateka iliipaswa kuwa kipaumbele cha kwanza lakini Sio tu kwamba makumi yao bado wako mikononi mwa Hamas, lakini baadhi yao waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga ya Israeli.

Badala ya kutokomeza Hamas, Israel imejifanya kuonekana kama taifa la kihuni, na Hamas wametoka katika hali hii wakionekana kama "watetezi" wa upinzani wa Palestina.

Sisemi Hamas hawana lawama, La hasha. Lakini jibu la maelfu ya mabomu hayakuitokomeza Hamas; iliimarisha masimulizi yao. Kila bomu lililoua raia, kila mtoto aliyetolewa kutoka kwenye vifusi, kila familia iliyokata tamaa iliyoachwa bila chakula au maji-yote hayo yalivhochea mashine ya propaganda ya Hamas.

Kijiografia, sifa ya Israeli imeharibika, limebakia sasa kama taifa pariah.Nchi nyingi (kama Uhispania, Ireland, Norway..nk) zimelitambua rasmi taifa la Palestina na hata kujiunga na kesi ya afrika kusini dhidi ya israel

Sifa ya Israel Kimataifa imechafuka. Viongozi wake wanatafutwa rasmi kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wanajeshi wa IDF wamesimamishwa kote ulimwenguni. Kuna kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel na taswira yake imeharibiwa vibaya.

Kwa upande wa Palestina, ni wazi.. Gaza imeharibiwa. Zaidi ya 100k waliuawa na bado hakuna taifa la Palestina. Bado wanaishi bila utaifa chini ya vizuizi vya Israeli.

Hamas Walipata kabisa walichotaka. Walitaka kusalia madarakani, kurudisha sababu ya Palestina kuwa nchi huru, kuizuia mpango wa normalization wa Israel na Saudia na kusaidia wafungwa wa kipalestina kutoka jela.

Vita hivi vinaendea kwisha, lakini cha kusikitisha ni kwamba tatizo la Waisraeli na Wapalestina bado halijaisha. Mzozo utaendelea kwa miaka ijayo.
Na wenyewe watajipanga tena kwa maelfu ya miaka..........naamini kizazi cha wajinga wapenda kufa ndio kinaenda kupotea ...........hakuna mwananchi mwingine ambaye atapenda kuona tena gharika linatokea pale gaza kwa ajiri ya ujinga.........next time watatumia busara zaidi na sio mihemko kama sasa .......kwenye hili palestine kwa upande wa gaza amepoteza pakubwa........atake hasitake.........wale Israel wataenda marekani na UK huko ndio wanakopenda kusafiri
 
Almendezz great analysis. Kuna mdau kauliza, hivi unafanya negotiation na mtu uliyemshinda kwenye uwanja wa vita?
Ukitaka kuielewa dunia ya sasa usitegemee western media propaganda machines.
You can't bomb your way to peace. Israeli wanted just that.
You can destroy buildings and economies but you can never destroy human spirit.
Hamas kapigwa mno. Lakini mwisho wa siku, hii vita imemuanika Israeli na kuonyesha ni jinsi gani mataifa ya magharibi yalivyo na kiwango kikubwa sana cha unafiki.
Siasa za akina Trump na wenzake kwamba mwenye nguvu mpishe, haziwezi kuleta amani duniani.

Siku zote fear fools, especially when they gang up together.
 
Back
Top Bottom