Black Americans wanaondoka Tanzania na hizi ndio sababu zao

Binafsi naona hizi sababu hazina mashiko yeyote kwa sababu kama walikuwa na long term plans basi wangekuja wachache kwa ajili ya kutafiti mazingira na sio kuchukua maamuzi ya mihemko. Pia nimejaribu kufuatilia back to africa movement na nimegundua kuwa haina support kiivyo na black Americans wenyewe hivyo ni idadi ndogo tu inatamani kuja kuishi barani Afrika. Au ndio tuseme wanakwepa korona kwa hiyo ikiwa sawa warudi makwao
In other words they should've known what to expect the moment they decided to set foot in Africa.
 
Mkuu isije ikawa unaona wazigua-wamarekani wanaokuja kwa wingi Tanzania ukadhani ni black American, sababu kuna wazigua toka Somalia wapatao 10,000 waliopelekwa marekani na kupewa uraia, na wanakuja tz kwa vile asili yao babu zao ni hapa tanzania.
 
Yaani uuze nchi (ardhi) kwa manufaa ya nchi?

Ni sawa na kusema " nimemkabidhi mke wangu kwa jirani kwa manufaa ya familia yangu"[emoji23][emoji23]
Tatizo lako mtazamo wako ume base kwenye emotional na sio facts
za kiuchumi

Mi naangalia faida za kiuchumi tutakazozipata km nchi

Mfano migodi ya dhahabu walivyopewa wazungu wanachimba dhahabu wanalipa mrahaba serikalini + kodi na pia wanatoa ajira ivo yaani
 
Hayo masharti maalumu ndo yanawashinda ndo mana warudi huko walikopangishwa
Masharti maalum hta kupata permit inakuwa ishu! Tanzania km kweli tunataka nchi yetu ipige hatua ni lazima tufungue uchumi wetu kwa mtu yoyote mwenye capital aje awekeze

Kwa hali ilivyo sasa ni wazungu pekee yao wenye mitaji ya mabilioni ndio wanaoweza kuja kuwekeza tanzania

Hatuwataki watu wenye mitaji ya kati waje wawekeze tumeweka masharti magumu mno dhidi yao
 
Kasome Sheria ya ardhi ya JMT!
 
Emotional= adjective [emoji777]
Emotion (s )= Noun[emoji3581]
 
dubai wageni wanaishi kwa parmit hawaruhusiwi kumiliki ardhi ukifungua biashara lazima uwe na partner mwanchi lakini wageni wamekubali na wamejaaa kwa nini tanzania wakimbie labda sema watanzania wasumbufu na wadanganyifu sio wakweli sio wachapa kazi story za usimba na uyanga mpaka makazini
 
Hao ni YouTubers na hizo ni mbwembwe tu. Tangu lini YouTuber anayesafiri akasettle sehemu moja.

Na wengi walijaa hapa kwasababu hatukuwa na lockdown na hivyo hawakuwa na option nyingine.

Sasa hivi nchi nyingi zimeshafunguliwa.
 
Nimekumbuka Professor Joshua Mkhululi.... ( Ken Edwards)
 
Hii issue ya kutoka nje ya nchi halafu ndio urudi tena kwa miezi mitatu mingine haileti maana hata kidogo. Yaani utoke uende Kenya ukalipe dollar mia huko halafu dakika kumi tu urudi uingie tena bila kulipa chochote.
Si afadhali hiyo dollar mia ningeilipa hapa ikasaidia ujenzi wa barabara hapa Tanzania kuliko kwenda kuilipa huko Kenya!!!
Wana-diaspora waliochukua uraia wa nchi nyingine hupata shida sana na sheria hii isiyokuwa na tija. Walau kungekuwa na special status ya wazawa waliobalidisha uraia kwa ajili ya maslahi tu na si vinginevyo, kubakia nchini for as long as they want because bottom line they love their motherland than their adopted countries.
Hiyo dollar mia watailipa bila kinyongo chochote hapa Tanzania iliradi tu wasisumbuliwe kutoka na kuingia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…