Black and White - Hukumu ya Nguza Vicking (BABU SEA) na Wanawe

Black and White - Hukumu ya Nguza Vicking (BABU SEA) na Wanawe

Bw/Bi Dilunga?!!!

Nisingependa kuanza majibizano yasiyokuwa na tija. Uko huru kukosoa kadri unavyopenda kama sio kukandia, hayo yalikuwa maoni yangu kuhusu mfumo. Sikusema nachambua kesi yenyewe na ninazo sababu zangu za kukaa kimya.

Una uhuru wa kuendelea kuchambua kesi na si maoni yangu binafsi.

Siku njema.
 
Bw/Bi Dilunga?!!!

....ninazo sababu zangu za kukaa kimya.

Una uhuru wa kuendelea kuchambua kesi na si maoni yangu binafsi.
Unatoa comment halafu unasema mtu asi comment kuhusu ulicho comment? Unaogopa? Unaona mawakili wetu wa JF mlivyo fyongo? Kama una "sababu za kukaa kimya", kwa nini ulifungua mdomo kuanza kukosoa mfumo?

Eti wewe ni mtaalam "mwenye upeo wa sheria"! Eleza basi, nini kilienda mrama kisheria katika kesi?
 
Dilunga,

Peace unto you. Punguza munkari! Maisha haya mafupi ndugu yangu, jazba haikupeleki popote. Jifunze kufurahia siku uliyopewa na Mungu wako. Unapoteza muda kunikosoa. Mada sio mimi ila ni kesi ya babu seya, please, toa maoni yako jamii ielimishwe na wala sio kuanzisha sokomoko lisilo na kichwa na mguu.

Enjoy your day my friend!
 
Inabidi Tanzania tupate wataalam wa forensic, labda itasaidia kuondoa doubts na itasaidia kupunguza convictions kwa wasiostahili. Na nafikiri pia tunahitaji jury system, maana haya maamuzi ya mtu mmoja ni rahisi sana kuwa influenced. Bado nina amini kuwa hii kesi na nyingine nyingi haziwi proven beyond reasonable doubts. Haiwezekani kabisa mtoto wa miaka 6 akaingiliwa na mijibaba zaidi ya miwili na akaweza hata kusimama sembuse kutembea, akijitahidi kujikongoja mpaka nyumbani then asipopelekwa hospitali mapema huyo ataoza sehemu nyeti lazima.
Nafikiri nikipata pesa nitakuwa Mtanzania wa kwanza kuchukua degree ya forensic science na kurudi nyumbani kuwasaidia Watanzania wenzangu wanaofungwa kwa kuonewa kwenye criminal cases.
 
Kwa kawaida sperms zinaweza kukaa hai kwa zaidi ya siku mbili, na hii ingewezesha scientific proof kupatika kwa at least some of the kids, then ushahidi wa watoto ungekuwa nyongeza.
Gashle nakubaliana na wewe kuwa mfumo wetu wa sheria hauko sawa una mapungufu mengi na ndio maana ni rahisi watu kubambikiwa kesi. kwa kesi kama hii pamoja na scientific proof pia wangeweza kabisa kuweka mtego wakawakamata washtakiwa red handed kama ndio ilikuwa ni mchezo wao.
Tuchukulie tu simply cases za rushwa, je mtu anaweza kufungwa simply kwa sababu watu nane wametoa ushahidi dhidi yake kuwa walimpa rushwa????????? This case has more doubts kuliko watu wanavyofikiria.
Wengi wanatoa maoni ya jazba bila kijiuliza maswali ya msingi, siwalaumu sana kwa sababu kitendo chenyewe ni cha kinyama.
Inawezekana ni kweli kuwa hawa watoto waliingiliwa, medical proof imeonyesha hivyo, lakini proof ya kwamba waliingiliwa na babu seya na watoto wake ndio ina utata. Sio tu kwa sababu watoto kumi walisema hivyo ndio ni lazima wanasema ukweli Noooooooo, hiyo sikubaliani nayo. Kwa kesi kama hii forensic science ingesaidia sana kuondoa utata.
 
ruby,

Umefanikiwa kupata muda wa kutosha na kuisoma document hiyo with objective mind?
 
Inabidi Tanzania tupate wataalam wa forensic, labda itasaidia kuondoa doubts Nafikiri nikipata pesa nitakuwa Mtanzania wa kwanza kuchukua degree ya forensic science na kurudi nyumbani kuwasaidia Watanzania wenzangu wanaofungwa kwa kuonewa kwenye criminal cases.

very interesting!
Kwani Mkuu cha ajabu hasa nini hadi ufikiri wewe utakuwa Mtanzania wa kwanza kusomea FS?
FS simply put is the application of science to the law.Huenda ukaenda ukasoma unachotaka kusoma, ukarudi na usiweze kutumia huo ujuzi wako kama wanavyoshindwa kuutumia hao wengine.Kwani kwenye hii kesi akina Dr Petronila na wengine walivyokuwa wanatoa ushahidi wao, ilikuwa ni nini kama siyo kutumia science katika kushauri mahakama kufikia uamuzi.

Kwani ndugu mpendwa unafikiri kitengo cha TDFA - Tanzania Drugs and food Authority,idara/division ya Forensic chini ya Mkemia Mkuu wa serikali na pia Goverment Chemistry Lab na vitengo vingine vimekuwepo kwa kusudio gani?

Nadhani tatizo siyo watu waliosomea fani bali ni mfumo mzima kuanzia investigation, prosecution hadi hearing/trial.Hii siyo kwa kesi ya Babu seya tu.Kuna watu wana taaluma na ujuzi wao, halafu kuna mfumo na taratibu ambazo haziendani na matumizi ya ujuzi au fani.Mfano mzuri ni kesi ya Prof Mahalu ambapo kulitokea mabishano ya kisheria kuhusu kukubalika ama kutokukubalika kwa ushahidi uliotolewa kupitia Video Conference ambayo ni njia ya kisasa zaidi ya mawasiliano hasa pale inapokuwa vigumu kumpata mtu kufika eneo physically.Tanzania bado tuko nyuma sana katika matumizi ya tech na mbinu mpya na ndiyo hasa lengo kuu la Legal Sector Reform Programme kuboresha mifumo ya utoaji haki na kuifanya iwe modern zaidi kuenda na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni.Hivyo Mkuu usishangae ukaenda kusomea degree yako ya Forensic ukarudi ukajikuta uko benchi kwa vile mifumo na taratibu bado ni ya kizamani na haiko tayari kutumia ujuzi wako.
 
Naona mkuu hapo juu hujanielew kidogo, japo umesoma sentensi mpaka mwisho. Nimesema nafikiri nitakuwa mtanzania wa kwanza kusomea forensic na kurudi nyumbani kusaidia watu katika kesi za jinai.
Ushahidi uliotolewa na daktari unaonyesha watoto waliingiliwa, swala zima hapo ni proof ya waliingiliwa na nani??????
 
Mkuu,
Asante na nadhani nilikuelewa na ndiyo maana nikajitahidi kuonyesha tatizo liko wapi.Kwenye kesi ya Nguza na wanawe, utakumbuka kulikuwa a kupelekwa hospitali akina Nguza na wanawe kwenda kupimwa.Utakumbuka pia Nguza akijitahidi sana kuonyesha kuwa yeye ni importent.. yote hii ni katika kujaribu kukwepa sheria isichukue mkondo wake.Anyway labda kulikuwa na hitilafu za hapa na palepale hilo linawezekana kabisa.

All in all, labda una mapendekezo kwa waliopo sasa ( experts in science na wanasheria) ni vipi wanaweza kutumia ujuzi na fani zao katika mfumo uliopo, ili haki itendeke.Nadhani moja wapo ya lengo la mijadala hapa JF ni kubadilishana uzoefu na mawazo ili kama kuna uwezekano tuboreshe hali tuliyo nayo katika nyanja mbalimbali.
 
Hatimaye Mahakama ya Rufaa imetoa hukumu. Hakuna rufaa baada ya hapo!
 
Hivi ile conspiracy theory ya Babu Seya kutembea na mke wa kigogo na huyu mkubwa kuamua kumzushia kesi na kumfunga yeye na familia yake vipi? Au ni maneno ya mitaani tu?

Mimi nakumbuka siku ya hukumu wasanii na wananchi wengi waliyatamka hayo juu ya hicho kisasi na pia hili lisemwalo halijakanushwa hadi sasa.
 
yani ukisoma hiyo hukumu na facts na evidence zilizo humo uwezi kudhani kuwa wange shinda hili.
 
watanzania wenzangu mamlaka yana nguvu, kushinda haki tafakari chukuwa hatua.
 
Kumekuwa na minong'ono ya hapa na pale kuhusiana na inshu ya Babu Seya na wanawe. Wengine wanasema alibambikizwa kesi ya ubakaji, wengine wanasema ni kweli alibaka, kwa kifupi kuna mengi sana yanaongelewa chini kwa chini.

Lakini kwa sababu hili ni jukwaa huru siyo vibaya tukijulishwa ukweli na member wenzetu wanaoujua ukweli ili na sisi tufahamu nini hasa kilichofanyika mwaka 2004. Binafsi nilisikia sana watu wakiongea mitaani kuwa Babu Seya alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa "MKWERE", na mara kadhaa alionywa lakini hakutaka kusikia, kitu kilichopelekea "MKWERE" kumfundisha adabu Babu Seya na wanawe kwa kuwabambikizia kesi ya ulawiti na ubakaji.

Tena inasemekana hata wimbo wa ule maarufu wa "SEYA TUTOKE WOTE", ulitungwa kama "dedication" kwa mke wa MKWERE.

Haya ni mambo ambayo yamekuwa yakiongelewa sana mtaani. Kama mtakumbuka hata katika kampeni za Uchaguzi mkuu za mwaka 2015, mzee Lowassa alisema akishinda Urais, basi atamwachia huru Babu Seya na wanawe. Nakumbuka alitoa ahadi hiyo akiwa Zanzibar kwenye kampeni.

Hakika kuna maswali mengi sana ya kujiuliza ambayo ningeomba mnisaidie kupata majibu;

1-Hivi ni kweli Babu Seya aliwabaka wale watoto?

2-Kama ni kweli aliwabaka watoto wadogo kwanini Rais Magufuli amewapa wabakaji msamaha?

3-Je, ni kweli Babu Seya alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa MKWERE?

4-Kama wale watoto hawakubakwa, nini kilichofanyika?

5-Inasemekana wale watoto walikuwa na umri wa maika sita mpaka nane wakati ule, hivyo kwa sasa hivi ni wadada wenye miaka 19 mpaka 21. Je, sasa hivi wako wapi?

6-Je, inawezekana kwa waandishi wa habari au mtu binafsi kuwahoji hawa wahanga ili kuujua ukweli?

Naomba mwenye majibu sahihi atujulishe atuambie ukweli wote. Mimi nahisi hili swala la akina Babu Seya na wanawe lilikuwa limegubikwa na utata mkubwa sana ndiyo maana hata Lowassa aliahidi kuwaachia huru kama angeshinda Urais. Kitu alichokiahidi Lowassa ndicho hicho amekifanya Rais Magufuli, jambo ambalo linadhihirisha wazi kabisa kuna kitu nyuma ya pazia kuhusu Babu Seya na wanawe.
 
Stori hii inafundisha usiwe na ukaribu na Nae atakuchukulia mke.
 
Namba sita ndiyo muafaka. Lkn hawajulikani and they are not willing, if they do really exist to show identity
 
Nasubiri wanaojua hili waje kutujuza binafsi sina nikijuacho.
 
Nasubiri jibu la swali namba moko! Linaniumiza sana kichwa,yaani sili wala sinywi!!
 
Back
Top Bottom