Kumekuwa na minong'ono ya hapa na pale kuhusiana na inshu ya Babu Seya na wanawe. Wengine wanasema alibambikizwa kesi ya ubakaji, wengine wanasema ni kweli alibaka, kwa kifupi kuna mengi sana yanaongelewa chini kwa chini.
Lakini kwa sababu hili ni jukwaa huru siyo vibaya tukijulishwa ukweli na member wenzetu wanaoujua ukweli ili na sisi tufahamu nini hasa kilichofanyika mwaka 2004. Binafsi nilisikia sana watu wakiongea mitaani kuwa Babu Seya alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa "MKWERE", na mara kadhaa alionywa lakini hakutaka kusikia, kitu kilichopelekea "MKWERE" kumfundisha adabu Babu Seya na wanawe kwa kuwabambikizia kesi ya ulawiti na ubakaji.
Tena inasemekana hata wimbo wa ule maarufu wa "SEYA TUTOKE WOTE", ulitungwa kama "dedication" kwa mke wa MKWERE.
Haya ni mambo ambayo yamekuwa yakiongelewa sana mtaani. Kama mtakumbuka hata katika kampeni za Uchaguzi mkuu za mwaka 2015, mzee Lowassa alisema akishinda Urais, basi atamwachia huru Babu Seya na wanawe. Nakumbuka alitoa ahadi hiyo akiwa Zanzibar kwenye kampeni.
Hakika kuna maswali mengi sana ya kujiuliza ambayo ningeomba mnisaidie kupata majibu;
1-Hivi ni kweli Babu Seya aliwabaka wale watoto?
2-Kama ni kweli aliwabaka watoto wadogo kwanini Rais Magufuli amewapa wabakaji msamaha?
3-Je, ni kweli Babu Seya alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa MKWERE?
4-Kama wale watoto hawakubakwa, nini kilichofanyika?
5-Inasemekana wale watoto walikuwa na umri wa maika sita mpaka nane wakati ule, hivyo kwa sasa hivi ni wadada wenye miaka 19 mpaka 21. Je, sasa hivi wako wapi?
6-Je, inawezekana kwa waandishi wa habari au mtu binafsi kuwahoji hawa wahanga ili kuujua ukweli?
Naomba mwenye majibu sahihi atujulishe atuambie ukweli wote. Mimi nahisi hili swala la akina Babu Seya na wanawe lilikuwa limegubikwa na utata mkubwa sana ndiyo maana hata Lowassa aliahidi kuwaachia huru kama angeshinda Urais. Kitu alichokiahidi Lowassa ndicho hicho amekifanya Rais Magufuli, jambo ambalo linadhihirisha wazi kabisa kuna kitu nyuma ya pazia kuhusu Babu Seya na wanawe.