- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Nimekutana na video huko duniani, kahawa hii wanapewa tembo wale na tembo hao wakijisaidia inaenda kusafishwa kisha kuuzwa, wanadai eti ikipita kwenye mwili wa tembo inapunguza ladha ya uchungu, yaani isiwe kali sana.
Hii ni kweli wataalamu?š„²
Video hii hapaš
---
Nimekutana na video huko duniani, kahawa hii wanapewa tembo wale na tembo hao wakijisaidia inaenda kusafishwa kisha kuuzwa, wanadai eti ikipita kwenye mwili wa tembo inapunguza ladha ya uchungu, yaani isiwe kali sana.
Hii ni kweli wataalamu?š„²
Video hii hapaš
---
- Tunachokijua
- Kahawa ni kinywaji kinachotengezwa kutokana na buni ambazo ni mbegu za mbuni. Kahawa Inapendwa kwa sababu ya ladha yake pamoja na kafeini iliyomo ndani yake
Kumekuwa na video inayodai kuwa kahawa aina ya Black Ivory Coffee ni kahawa inayotokana na mbegu za kahawa(buni) kuchakatwa kwa kumezwa na tembo kisha kutolewa kwa njia ya kinyesi na mchakato mwingine kuendelea ili kupatikana kwa aina hiyo ya kahawa.
Je Ukweli ni upi?
Black Ivory Coffee ni aina ghali sana ya kahawa inayotengenezwa kwa kutumia mbinu maalum ya kuchakata Buni(mbegu za kahawa) kupitia mchakato wa kumeng'enywa na tembo.
Tembo hulishwa buni wakati tembo akila chakula chake cha kawaida huchanganyiwa na mbegu hizo, na kusubiri mchakato wa kumeng'enya chakula wa kawaida wa tembo na kisha akitoa kinyesi cheke zile mbegu z buni zitakazotoka bila kumeng'enywa kabisa hutolewa kwenye kinyesi cha tembo na kuchakatwa.
Mchakato huu unadai kwamba njia hii ya buni kumeng'enywa husaidia kuondoa asidi na Protini zilizo kwenye kahawa ambazo ndio hufanya kahawa kuwa chungu na kufanya kahawa kuwa na ladha laini, yenye utamu kidogo tofauti na kahawa nyinginezo. Aidha, kampuni ya Black Ivory Coffee Company Ltd inaeleza mchakato huu wa tembo huchangia kutoa ladha za kipekee kutokana na mimea mbalimbali tembo wanayokula.
Mwanzilishi wa Black Ivory Coffee ni Blake Dinkin, alianzisha mradi huu wa kahawa mnamo mwaka 2012 baada ya kufanya utafiti wa miaka mingi juu ya njia tofauti za kuchakata kahawa.
Dinkin alipata wazo la kutumia tembo baada ya kusikia kuhusu kahawa inayopatikana kupitia wanyama wengine, kama vile Kopi Luwak, ambayo inapatikana kupitia marten (mnyama mdogo anayeitwa civet). Alitaka kutengeneza kahawa yenye ubora wa hali ya juu, lakini kwa njia tofauti, na akaamua kutumia tembo, ambao wana mfumo wa kumeng'enya polepole zaidi na wanaweza kuleta ladha ya kipekee kwa kahawa.
Kupitia ushirikiano na mashirika ya hifadhi ya tembo nchini Thailand, Dinkin alianzisha uzalishaji wa Black Ivory Coffee. Pia, sehemu ya mapato kutoka kwa kahawa hii huenda kusaidia kulinda tembo na kusaidia jamii za wenyeji wanaoshirikiana kwenye mradi huo.
Kahawa hii inapatikana zaidi nchini Thailand na sehemu za Asia Kusini-mashariki, na kwa sababu ya mchakato huu mrefu na nadra, Black Ivory Coffee ni moja ya kahawa ghali zaidi duniani.