CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Nakubaliana kwa asilimia kubwa. Hata Dangote Aliko, Tajiri namba moja Afrika, katika "ten commandments on money" amesisitiza kuwa moja ya kitu cha kumvusha mjasiriamali kirahisi ni shughuli za Processing. Dr. Olomi Pia katika "The Enterprise Map of Tanzania' ametafiti na kusema Uchumi wa Tanzania Umekuwa, Ume - double, na mchongo mkuwa ni wadau wanaofanya production na Processing. La msingi ni kuzalisha kwa kujali afya.
Ni kweli Kabisa Mkuu, Kuongeza thamani ndo mpango mzima, Tatizo la wakulima wengi wanauza mazao au wanunuzi nao wananunua na kuuza kama yalivyo hapo hakuna kitu.
Chukulia Mfano mtu anafanya biashara ya mazao ananunua Karanga Dodoma na kuja kuuza Dar, Hapo kama ananunua karanga na bado anakuja kuziuza kama zilivyo hapo hakuna kitu na utaona wafanya biashara wa aina hiyo wanaishi kwa ujanja ujanja tu.
Ujanja wa hao wafanya biashara ni kununua mchele wa Mbeya na kuchanganya na mchele wa Mrogoro au wa Moshi lakini kama mfanya biashara angejikita kununua mazao na kuyaongezea thamani na zani kungekuwa na tija.
![images[9].jpg images[9].jpg](https://xf23.jamii.app/data/attachments/3215/3215157-151fd75a6c0c5bc629dc99299ea10c23.jpg?hash=FR_XWmwMW8)
![images[8].jpg images[8].jpg](https://xf23.jamii.app/data/attachments/3215/3215158-3db1d4e89f326a579cdf15498aeaea0f.jpg?hash=PbHU6J8yal)