Well binafsi naweza nikakushauri kama unatumia website zaidi ya moja tumia zote mbili kwa maana kuna vitu utavikosa kwenye wordpress na utavipata kwenye Blogger..
Mathalani unataka traffic kubwa na hutaki kutumia pesa nyingi kwa kuzipata ni vema zaidi ukatumia Blogger kwa maana mfano Afrika Mashariki watumiaji wengi wa internet search engine yao pendwa ni Google hivyo Blogger ni Mali ya Google.
Hutafikia kiwango chao cha posts wanazotaka kuanza kukuwekea traffic halafu ukakosa traffic lazima watakutumia traffic ambayo ni nzuri kulingana na Articles ulizonazo..
On the other way,
WordPress hata ukisema ununue plugins ambazo ni Search Engine Optimize nzuri bado hawa wana mbinu ya kutuma fake traffic ambazo ukiziangalia utaona ni traffic zinazotoka eneo lako lengwa lakini ukweli wake utaupata kwenye adsense account.
Upande wa watu waliotembelea tovuti yako (
Sio watu walioview ads zako) yaani general visitors hata wale ambao wameclick na kuondoka (
Sio walioclick tangazo) utawaona kwenye adsense dashboard kuna jinsi ukiiset..
Binafsi kunakipindi nilikuwa napata visitors 1,500 kwa siku kupitia blogger lakini nilihamia na kukaa Wp kwa miaka miwili nikawa napata 500 na hapo ukumbuke mbinu zote unazohisi unazifahamu nimeshatumia..
nikaipa 2yrs ili ikae vema na google matokeo yake nikawa napata 250 traffic kwa siku na kila baada ya mwezi utakuta Plugin moja au mbili zimecrash na bado umeweka automatic updates...
Kufupisha maelezo kama unafanya tovutia kama ajira yako ya kila siku yaani kila siku lazima uingie kufuatilia tovuti yako inaendaje basi Wordpress ni chaguo lako...
Lakini kama ni mtu wa matumizi ya mara 3 kwa wiki itakusumbua tu maana WordPress ni kwa matumizi ya watu ambao blogging ni ajira yao na hawana mambo mengine yanayoweza kuwataka kwa muda sahihi..
Nadhani hadi hapo kwa uchache nitakuwa nimechangia upande wa wewe kuita moja takataka na nyingine safi..
Twende kwenye ipi Bora kwa adsense...
99% blogger ni bora zaidi kwa adsense kwa maana ipo chini ya Google na Adsense vile vile ni chini ya Google
Kama unataka kutengeneza pesa za adsense vizuri bila mashaka tumia blogger wao wananjia ya kumuwekea matangazo hata mtu mwenye tovuti ya kiswahili japo bado sio official kuna vigezo utatakiwa kufikia....
Watu wengi hukimbilia Wp kwa kudhani ni vile kuna option ya kuunga Ezoic na Media na utumbo mwingine wa matangazo kutawaletea faida kubwa lakini tuchukulie mfano watu walioikimbilia ezoic kwa wordpress ajiri ya matangazo walikutana na nini...
Articles nyingi ambazo hata ukielezea tu sehemu za uchi vyovyote vile hata dawa ya fungus sehemu za siri hutapokea tangazo lenye support ya Ezoic hata kama utoe maelezo kuwa ni dawa na sio hivyo tu hata kwa articles nyingine kama hujafikisha maneno wastani 600 hadi 800 hupati tangazo la Ezoic maana wao wanajudge moja kwa moja utapata low traffic kwenye hiyo post...
Ni mengi ya kufuatilia lakini kwa thread yako imeonyesha ni mtu mwenye kutaka ushuhuda wa blogger au Wp ipi inaingiza pesa za adsense zaidi
Tuanze na Wp:
Hii hutopata senti nyingi za adsense kwa maana ili uweze kumaintain WP lazima kwanza umwage pesa ambayo haitakurejeshea trust me utakuwa huna tofauti na watu wanaocheza vikoba hivyo Wp inamfaa mtu ambaye website yake ni ya biashara yani yenyewe inafaida ndani yake watu wakitembelea.
Tuje kwa Blogger:
Hii utapata senti nyingi za adsense lakini maarifa yake utatakiwa u block unwanted ads zote zenye kuleta matangazo yenye malipo madogo na zipo nyingi sana lakini trust me ukitenga masaa matano ya siku moja kwa ajili ya kufunga hizi basi ndani ya siku 2 zijazo utaona mabadiriko kwenye mapato yako..
Imagine wewe katika tovuti yako unaonyesha matangazo ya 0.008$ ni sawa na 0.8$ kwa watembeleaji 100 na mwenye tovuti mwenzio anaonyesha ya 0.20$ ni sawa na 20$ kwa watembeleaji 100 sasa tuangalie mara 100....... nadhani jibu utalipata..
Most of the time matangazo makubwa huonyeshwa automatic kwenye tovuti kubwa na madogo huonyeshwa kwenye tovuti ndogo sasa ili uweze kwenda nao sawa lazima uzingatie uchambuzi wa matangazo na ndio msaada wanaokupa Ezoic uchambuzi wa matangazo ya kukuonyeshea!!! kwa nini usifanye mwenyewe???
Hawana tofauti na madalali in the end wao wanapataje pesa????
Hivyo kama ni mtu kuuza bidhaa zako mwenyewe kwenye tovuti yako basi Wp itakufaa zaidi lakini kama ni mtu wa kufundisha chochote kwenye tovuti yako basi blogger is the best nayo uizingatie katika templates zake maana zingine ukiwa nazo kweli kabisa utaona blogger ni muozo.
lakini ukiwa na ambazo ni sahihi basi blogger ni almasi.. in fact nani kaanza kuuza ads?
The same goes to Wordpress ukiwa na hosting nzuri nayo jitahidi isiwe ya HTML website pia jitahidi usiwe na too much unused CSS na codes za ajabu ajabu na kama utaweza domain na hosting yako iwe kwa kampuni moja japo utatakiwa kila baada ya muda fulani ulipie which is not good kwa mtu atakae kuwa na website ambayo haimuingizii pesa zaidi ya matangazo tu...
View attachment 2582809
Sijui kama hicho kipicha kitakusaidia kupata uthibitisho unaotaka.
Rakims