Blue ticks za whatsapp: Ni kwamba huyo mtu yupo busy sana au ameamua tu kukuonesha dharau za waziwazi?

Atanijibu kwa muda wake, which is perfectly fine.

Kama kuna kitu muhimu sana nampigia.

Mara nyingine mtu anaweza kusoma message akataka kujibu, akatingwa na mambo mengine akasahau kujibu haraka.

Hata mimi huwa inanitokea hivyo.

Bila ya nia mbaya wala dharau.
 
Nimeacha kuchat na wengi sababu hiyo,yaani mtu anaisoma kabisa na anajua hii sms inahitaji jibu anapotezea na yupo online unamuona
 
Kama kuna kitu muhimu sana nampigia.

Mara nyingine mtu anaweza kusoma message akataka kujibu, akatingwa na mambo mengine akasahau kujibu haraka.

Hata mimi huwa inanitokea hivyo.

Bila ya nia mbaya wala dharau.
USHAURI WANGU: Hao Whatsapp kama wanaweza pale katika emoji zao waweke "quick text" ambayo mtu akibonyeza mara moja itaandika "Nimepokea ujumbe wako na nitakujibu nikipata nafasi, kwa sasa nipo busy"
 
Hata kama ni dharura na akikujibu baada ya siku saba bado ni "perfectly fine"?...
Dharula unampigia simu.

Kuweka expectations za mtu kukujibu kwa muda fulani ni aina fulani ya insecurity.

Watu tunaotafutwa kwa kiasi kikubwa hatuna tatizo hilo.

Na mtu akichelewa kunijibu, that is his/her loss.

Kwa sababu mara nyingine nasalimia watu nikiwa na mood ya kugawa hela na zawadi ndogo ndogo zisizopungua thamani ya $100 🙂

Au kutoa bonge la idea ya kumfungua macho mtu. Au kumfariji mtu.

Wanaonijua huwa hawakawii kunijibu, wanaokawia kunijibu hawanijui. Nami sina hulka ya kutaka kujulikana au kuombeleza urafiki.
 
USHAURI WANGU: Hao Whatsapp kama wanaweza pale katika emoji zao waweke "quick text" ambayo mtu akibonyeza mara moja itaandika "Nimepokea ujumbe wako na nitakujibu nikipata nafasi, kwa sasa nipo busy"
Wangeweka option ya kukataa kuonesha kama umesoma au hujasoma text ingesaidia pia.

Kama walivyoweka option ya kuficha last time mtu alivyokuwa online.

Sasa mtu yupo katika mikutano yake muhimu, unataka akatishe mikutano kukujibu wewe message ya salamu Whatsapp?

Akianza kukujibu napo atapata lawama kutoka watu alio nao kwenye mkutano.

Huyu katudharau, yupo nasi hapa kwenye mkutano, lakini haweki attention hapa, anajibu messages za Whatsapp!
 
Hiyo option ipo mkuu.Mi nikitumiwa text naifungua,ila aliye tuma haimletei ile blue tick.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…