BMT: Marufuku Simba Na Yanga Kubadili Umiliki, Zibaki Kwa Wanachama

BMT: Marufuku Simba Na Yanga Kubadili Umiliki, Zibaki Kwa Wanachama

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,866
Reaction score
5,747
Serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania(BMT) imezisitishia timu za Simba na Yanga mipango ya kubadili umiliki wa Timu hizo na hivyo Wanachama kuendelea kuwa wamiliki halali wa timu hizo.

Baraza la Michezo la Taifa limezitaka timu hizo zifuate sheria katika michakato yao ya kubadilisha umiliki hadi hapo klabu hizo zitakapo badilisha katiba zao kutoka kwenye umiliki wa wanachama kwenda kwa umiliki binafsi.

BMT imesema kuendelea na michakato hiyo bila kubadilisha katiba ni kinyume na sheria na hatua stahiki zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.

 
Siasa na ufinyu wa uelewa katika soka la kisasa ndio unazifanya timu zetu kuwa na maendeleo duni ndani ndani na nje ya nchi
 
Ina maana wanachama wanapangiwa wanachotaka uamuzi Wa kubinafsisha ni Wa wanachama BMT bakini na timu za taifa
 
BMT tafuteni timu.zenu simba na yanga ni za wanachama ambao wameamua waaze hisa/kukodisha kama ni hivyo hata Bakhresa akitaka kuuza Azam atazuiwa
 
OK,AKILI-MBOVU AONGOZE TIMU,WAFADHILI KAENI PEMBENI IF POSIBLE ACHANENI NA HUU UPUUZI WA AJABU./
 
Yote haya ni fitna za yanga na si mwingine bila wao kukurupuka na timu yao leo wala yote yasingekuwepo
 
Siasa kwenye mpira wapi na wapi? Maamzi ya kuuza hisa si yawanachama,wao BMT wanaona raha timu zetu kuburunda kila siku kwa kukosa usimamizi mzuri.
 
BMT ni mbovu IVUNJWE TU HAKUNA NAMNA,WE WANT TO GO AHEAD ON FOOTBALL,KWA KASI YA RAIS WETU, MABWANA HAWA PAMOJA NA VIBABU VYAO VICHAWI HAWATAKI MAENDELEO KILABUNI../
• NI TABIA YA WACHAWI KUTOPENDA KITU MAENDELEO.../
CHUNGUZENI....!?!
 
Hivi mtu anweza kukupangia jinsi ya kuiendesha familia yako? Wenye timu ndio wameamua timu zao zibadilishe mfumo wa uendeshaji.
 
Siasa kwenye mpira wapi na wapi? Maamzi ya kuuza hisa si yawanachama,wao BMT wanaona raha timu zetu kuburunda kila siku kwa kukosa usimamizi mzuri.
Kuongoza timu mpaka kufikia deni la Bilion 11 ndo usimamizi mzuri???
tunahamu sana ya kufikia maendeleo lakini siyo kwa njia hii
 
Back
Top Bottom