BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

Acha hizo kuna range rovers nyingi sana nimeziona gereji za mitaa ya kinondoni na sinza zimetelekezwa sijui kuna siri gani humo

Kuna garage nimekuta Disco 4 . siwezi sema zimetelekezwa ila zimekaa kitambo.

Moja ya sababu naelewa ni gharama za matengenezo ambazo mtu akiambiwa lazima akajipange kwanza ba gari haiendesheki
 
Ina maana kwenye garage zote za Tanzania hakuna gari za kijapan?
Kumbuka watu wote hatuwezi kumiliki Toyota Tu kuna wengine huwaambii kitu Kwa mjerumani....
Ndio hao sasa wameyatelekeza.
Utawaambia nini?
ni kweli "huwaambii kitu"

Sinza Kumekucha pale Soprano Garage asimilia 85% ya magari yaliotelekezwa pale (tuseme yanayokaaga miezi mpaka yapone) ni European Cars.

Toyota zilizopata ajali zinaletwa hazichukui hata siku tatu zinarudi kwa Road.
 
Kuna garage nimekuta Disco 4 . siwezi sema zimetelekezwa ila zimekaa kitambo. Moja ya sababu naelewa ni gharama za matengenezo ambazo mtu akiambiwa lazima akajipange kwanza ba gari haiendesheki
Umaskini ndio tatizo, unakopa benki milioni 35, unamvua mtu Disco 4 milioni 30 ili uvimbe nalo mjini. Unaenjoy nalo baada ya miezi mitatu linakorofisha linazima.

Unalikokota mpaka gereji unaambiwa mpaka lipone inatakiwa uweke milioni nane mezani. Unaamua kulikacha ujipange mdogo mdogo. Linabaki kua screpa la madogo wanaosadia fundi kupumzikia na kuvutia sigara gereji.
 
Upo sahihi mkuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…