Boarding Schools 1970s-2000: Kambi za watu katili, wanaopenda masomo, mateso, ukakamavu, walokole na wazinzi

Boarding Schools 1970s-2000: Kambi za watu katili, wanaopenda masomo, mateso, ukakamavu, walokole na wazinzi

Dada hujaolewa unaonekana una stress za maisha. Au upo period?hujalazimishwa kusoma mwanaisha umekuwa kama umechanganyikiwa toka omari akupige chini unawachukia wanaume na unatafuta ugomv na kila mtu. Unawatafuta na wengine huwafaham ili iweje?we pambana na hali yako ya kimaumbile na uchumi. Acha kudakia ya wanaume. Umerud kwa wazaz mwanamke mzima unabaki kubwatukia watu na ids zako mbili sometme unajifanya mwanaume unasahau hii ID nlikufungulia mimi tena tukiwa bar na ommy akiwepo.
mkuu nikajua huyu ni mwanaume kumbe demu?
 
piga cm kwa wazazi wako huku unachungulia tundu la choo ,zamani ujinga hatutaki
 
Ni demu ila ni kama kachanganyikiwa flan hivi baada ya kutoswa na jamaa yangu ommy. So siku hizi anadandia dandia wanaume na hajielew... Smetme anajifanya ye mwanaume ili sijui iweje kwenye posts zake.

mkuu nikajua huyu ni mwanaume kumbe demu?
 
Ni demu ila ni kama kachanganyikiwa flan hivi baada ya kutoswa na jamaa yangu ommy. So siku hizi anadandia dandia wanaume na hajielew... Smetme anajifanya ye mwanaume ili sijui iweje kwenye posts zake.
Weka ushahidi kama ni ke.
Pamoja na yote hii hadithi ni kweli watu walio pitia wanayaelewa na bila ya kigugumizi kaandika vizuri
 
Ni demu ila ni kama kachanganyikiwa flan hivi baada ya kutoswa na jamaa yangu ommy. So siku hizi anadandia dandia wanaume na hajielew... Smetme anajifanya ye mwanaume ili sijui iweje kwenye posts zake.
msamehe bure mkuu,vibuti sio vya mchezo
 
Namfaham ningekuwa naruhusiwa ningeweka picha. But namfaham na ukisoma posts zake nyingi ingawa kwa id hii hujifanya mwanaume zipo nyingine ndo ana behave kama mwanaume.

Weka ushahidi kama ni ke.
Pamoja na yote hii hadithi ni kweli watu walio pitia wanayaelewa na bila ya kigugumizi kaandika vizuri
 
Simulizi imekaa vizuri. Sisi wa Day hizi story tulikuwa tunaletewa na wenzetu wa boarding nyakati za likizo!
 
Kuna maeneo na majina sitoyataja kwa makusudi ili kuficha walioathirika na matukio yaliyotokea ambao kwa sasa wengine ni watu wakubwa na vyeo vyao serikalini na vyombo vya dola.

Ilikuwa siku ya jumamosi mida ya saa 9 ndo naingia eneo la shule. Ni mkoa wenye baridi sana. Nawaona watu mbalimbali wenyeji wakiwa wamevaa nguo nzito kiasi flan wamekusanyika maeneo mbalimbali wakiota moto na kuchoma mahindi.

Tunapotembea mimi na watu wengine wawili mimi nikiwa na bag langu kubwa la mgongoni na sanduku la bati ngumu (trunker) amenibebea mwnakijiji mmoja ambaye ni mbeba mizigo. Pia juu yake limefungwa godoro la futi nne kwa sita nchi 6.nawaona wenzangu wengine wawili nao na mabegi,godoro na hayo masanduku.

Wanatokea watu watatu wanakuja kumpokea mmoja ya wale wanafunzi. Mimi nlikuwa na bro mmoja ambaye tunatoka naye mtaa mmoja dar so alikuwa kama kaka yangu. Na wenzake wawili. Wale wanafunzi wenzangu wapya mmoja wao akapokelewa na mtu mmoja mkubwa kiasi na amekomaa. Alikuwa amevaa viatu kama vya jeshi vyeusi na surual ya jeans imepauka inambana imemlegea kidogo kiunoni.alimfuata yule mgen mwenzangu na kumpokea mzigo na ghafla akaanza kulia kwa sauti huku anaomba apewe bag abebe. Yule mwanafunzi ambaye nlikuja kumfaham kwa jina la sunday akagoma kwanza lakini alipoona jamaa anasisitiza akampa.jamaa akabeba ule mzigo huku akilia na kuongoza njia.cha ajabu wenzake aliokuja nao wala hawakusema kitu zaidi ya kutembea kama vile wapo kwenye majonzi.

Wakiwa wanatembea akaja mwingine huyu alikuja na furaha sana akicheka na kuonesha furaha akampokea mwingine nliyekuja kumfaham kuwa anaitwa shaban.akamkumbatia.shaban(jina bandia kwa sasa huyu ni XXXXXXXXXXX hapa nchini) akashtuka kidogo jamaa akaomba ampokee na kumakaribisha kwa bashasha kubwa sana. Naye akabeba mzigo akaongoza kuelekea barabara moja ambayo kuna kibao kimeandikwa shule ya sekondar XXX.

Tukaelekea huko hapakuwa mbali sana.kwa kweli nlikuwa nasikia baridi mpaka meno yanagongana nikawa nmajikumbatia pamoja na kuvaa coat zito halikufua dafu.

Ilifika jioni baada ya kila mtu kuwa ameoneshwa sehem ya kuishi.kulikuwa na mabweni makubwa manne. Ila mimi na hawa kaka zangu mmoja tukiwa tumetoka naye dar tulienda kukaa nyumba moja ambayo ilikuwa zaman ya mwalimu ila ikabadilishwa kuwa bweni kwa viongozi.huyu bro alikuwa kaka mkuu, mwenzake mmoja alikuwa waziri mkuu na mwingine waziri wa chakula.

Usiku kama saa mbili mlango ukaja kugongwa... Akatoka bro( hivi sasa ni mtumishi wa Mungu) wakaongea maneno kadhaa akaja kunambia wenzangu wananiita niende prepo(masomo ya jion) nikamwambia sina cha kwenda kusoma na nmechoka.kule mlangoni jamaa akasisitiza basi hata nikawasalimu. Nikaona isiwe shida sababu ya mazingira ya kule nlikuwa nikaenda room nikavaa combat, coat zito na boots nikafika mlangon nikamwona jamaa siyo friendly ila analazimisha kuonesha yupo friendly na wenzake kwa nyuma ule ukimya wao ulinishtua. Nikawaambia subiri nikarudi ndani. Nikaenda kubadilisha mkanda nikavaa mkanda wa mzee ambao alikuwa anautumia zaman alipokuwa mwnajesh.

Walikuwa jamaa watatu wakanichukua wakanambia twende wazee wakakusalimu. Kulikuwa na giza shulen tulikuwa tunatumia taa za solar sabab umeme ulikuwa bado kufika. So njia nzima ilikuwa giza kunasikika tu sauti ya wadudu na wanaonekana wale wadudu wanaotoa mwanga wanaruka ruka.sikuwah kuwaona mwanzo nlikuwa nawaogopa nikidhan wanaweza niunguza.nlipoona wenzangu wanakaza mwendo sikujali nikapiga moyo konde. Mbele nikasikia sauti ya kilio na jamaa wakifoka "salimia wazee" kulikuwa na kimto maringo ile sehemu hakikuwa kinakauka miaka yote.maji yalikuwa ya baridi sana. Nikaona mtu analazimishwa akae chini ya maji akiibuka anachapwa viboko maji machafu yenye matope...anazama akiibuka anachapwa anarud kwenye maji. Nikaingiza mkoni chin ya coat nikalegeza mkanda. Yule jamaa kule eiendelea kumpa kipigo wakiwa walikuwa watu wawili waliojifunika usoni.mimi nikapata wazo hali si nzuri hasa baada ya kuona jamaa nliokuwa bao kama wanataka kunitanguliza basi nikawa makini. Jamaa mmoja alinisukuma ili nianguke kumbe mwenzie nlikuwa standby nikaenda mbele kwa kasi sikuanguka nikawa tayar nmeshachomoa mkanda na kumpiga nao aliyenisukuma alipiga kelele "jichoooooooo" kile chuma cha mkanda kilimpasua jicho. Tayari mimi nlikuwa nmeshapandisha mori. Nawaambia asogee mwngne.kile kilio kiliwafnya jamaa wasije mmoja akasoge nikampiga na mkanda kichwan akachanika mwingne akakimbia na hawa wakakimbia nami nikawa nakimbia kurud bwenini kwangu sasa. Nao wakidhan nawakimbiza mpaka walipotokomea kwnye miti mi nikarud bwenini.nahema sana nina mkanda mkono na damu imenirukia.

Wale mabro kuniona wakaniuliza umeumizwa na nini sikujibu kitu nikavua lile coat...mmoja akatoka kasi kuelekea kwenye mabweni ya jumla.kufika kule anasema likumkuta mwanafunz mmoja kapasuka jicho lote na mwingine kachanika kichwan.

Akarud kuuliza ilikuwaje.nikamweleza.yule wa jicho haraka akapelekwa dispensary na alichanika hapakuwa pakubwa sana akagoma kwenda.ikawa usiku mzito ambao sikulala kwa amani maana nlikiwa nawaza nini next.

Jumapili mapema nliamka nikawa nje nasubiria nini kinafuta pale kwenye kabwen ketu walikuja watu weng kiasi wanaoneshana vidole vikinielekea mimi.wakawa na mengi ya kuongea.

Yule jamaa alichukuliwa na gari la misheni kupelekwa mjini kwa matibabu.jumapili tete ikapita.jumatatu asub assembly tukakaribishwa na yakatolewa matangazo ya matukio makubwa mawili moja la form one mmoja(njuka) kuteswa mpaka kuamua kuondoka kurudi home na lingine form two wawili kujeruhiwa.mwalim akataka wahusika wapite mbele.wote wakanyamaza.wale waliokuja kuniita pia hawakujitokeza..... Huo ulikuwa tu mwanzo wa maisha ya kisasi,ubabe na masomo shuleni hapo. Ulikuwa mwanzo wa kuanza kuishi kwa matumaini, looking over the shoulders na kwa umakini kila hatua. Yalikuwa maisha yaliyojaa hofu isiyo na woga na ujasiri wenye wendawazimu.

NB: NITAPUNGUZA BAADHI YA DETAILS HASA BAADA YA JAMAA MMOJA NLIYESOMA NAYE KUNIPIGIA SIMU AKIHISI KABISA NI MIMI NMEMZUNGUMZIA YEYE. NA LENGO LANGU NI KUBAKI MTU ASIYEJULIKANA. HIVYO NTAONDOA BAADHI YA DETAILS ILI WAHUSIKA WASIJE WAKAFAHAMIKA. SI LENGO LANGU KUWA EXPOSE. WENGI WANA NAFASI MUHIMU KITAIFA. KASORO MIMI TU.

Ntaendelea niwaache mpuzike kiasi...
Aisee.
 
Siku hizi wanasoma watoto hata harufu ya maziwa haijawatoka sio sekondari tu hata baadhi ya vyuo wanapelekwa pelekwa .
 
Maisha magumu nilikumbana nayo Geita Secondary School. Siku moja ambayo maninja walinichapa kwa nyaya kitandani. Mmoja nikamfahamu na nikaripoti kwa baunsa mmoja ambaye nilitokea kumheshimu na yeye kunichukulia kama ndugu. Asubuhi akanipitisha kila bweni nimtambue maana ilikuwa jumapili. Mungu mkubwa akatokea anatoka kuoga bafuni, alipigwa gwala akadodokea sakafu, nikapewa fimbo mbili kwa sharti hadi ziishe akataja aliyekuwa amewatuma (kuwakodi), alipoletwa nikamtambua jamaa aliniomba nimpe hela nikagoma..............
Wengi wa hayo matendo nilikuja kujua walikuwa ni wale wasio na akili darasani
 
Back
Top Bottom