Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Kwa Watanzania na Wanamageuzi wenye mapenzi mema na CHADEMA na Taifa letu. Kwa vijana wanaotamani kufanya siasa za Upinzani kwa miongo kadhaa ijayo. Lissu is the way! Hawezi kuwa mkamilifu kama Binadamu, lakini ana sifa muhimu kwa maslahi ya CHADEMA na Taifa. Kwa kizazi hiki watu wa aina yake ni wachache sana. Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chadema, haiwezi kuwa habari njema kwa Watawala. Huyu ndiye mtu sahihi.
Tutakuwa na wakati mgumu sana katika kufanya siasa kama atashinda mtu mwingine zaidi ya Lissu. Mfano, ikitokea Mhe Mbowe ametetea kiti chake, kule Bungeni kesho kutwa kina Kibajaji wakipeleka Muswada wa kuondoa ukomo wa Urais tutakuwa na hoja gani za kutetea ukomo? Zipo hoja nyingi ambazo tutakosa uhalali wa kuzisemea. Tuwaunge mkono tunaowapenda lakini tufikirie pia uendelevu wa chama (sustainability) baada ya Uchaguzi.
Natambua uwezo na mchango mkubwa wa Mhe. Mbowe na nikiri tu tumekuwa na ukaribu kuliko ukaribu wangu na Mhe. Lissu lakini kwa maslahi mapana ya Chama ambacho amekijenga kwa gharama kubwa, naona Lissu anatosha kabisa kumpokea kijiti cha Uenyekiti hasa kwa wakati huu ambao tuko kwenye matatizo makubwa ya Kidemokrasia. Morali za watu wetu iko chini hasa baada ya kuumizwa na mifumo ya Uchaguzi. Kwa mazingira haya, mabadiliko ni muhimu ili kuirejesha.
Lissu akishinda tutakuwa na timu kamili (Mwenyekiti Mbowe atabaki kuwa Mzee wa Chama mjumbe wa kudumu wa Kamati kuu ya Chama). Hivyo, bado atakuwa na nafasi ya kujenga Chama. Waliorudi nyuma kisiasa naamini watarudi kazini na wasioitakia mema CHADEMA wataona aibu sana.
Habari ya kuwa ‘neutral’ ni unafiki! Mimi niko na Lissu! Tufanye kampeni za Kistaarabu wote hawa ni viongozi wetu ili tuendelee kutoa somo kuwa chama chetu ni cha Kidemokrasia.