Bob Junior ampigia magoti Diamond Platnumz na kumlilia kama mtoto

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Aliyekuwa anajiita rais wa masharobaro au ukipenda muite Mr Chocolate Flavor, Bob Junior hatimaye amlilia Diamond Platnumz na kumlaumu kwa nini amemtupa?

Bob Junior roho inamuuma kwa kuwa yeye ndiye aliyemuibua Diamond na kumfanya ang'ae


Sasa anashangaa kwa nini na yeye diamond asimsaidie kunyanyuka kimuziki kama yeye alivyofanya hapo awali?


Bob Junior aliwahi kutamba na nyimbo kama Nichumu, Oyoyo, na Kimbiji








Miaka ya nyuma kidogo bob junior alikuwa na ugomvi mkubwa na diamond na mara kwa mara alikuwa anamponda kwenye media, Diamond alijitahidi sana kujishusha ikiwemo kumualika kwenye party mbalimbali lakini bado bob Junior akazidi kumvimbia diamond, na mbaya zaidi akawa team kiba na kumkandia vilivyo Diamond.


Diamond akaona sio kesi akaamua kumpotezea mazima matokeo yake jamaa akasahauilika kabisa kwenye anga ya muziki mpaka sasa ambapo anamlilia Diamond amsaidie kumnyanyua na akumbuke walipotoka.
 
Naona hili litakuwa funzo kwa Ommy Dimpoz.

Ommy na Dai walikuwa marafiki wa kubwa sana ila tangu walipotofautiana kidogo wamekuwa maadui wakubwa kiasi kwamba Ommy amemtusi diamond kwa kumvimbia na kudai amelala na mama yake.


Diamond miaka ya nyuma alijitahidi kuondoa tofauti kati yao lakini Ommy akaendelea kuvimba.

Na Diamond walipokutana na Ommy South Africa kwenye Tuzo, Diamond alimsalimia Ommy ila Ommy akamvimbia Dai na kukataa mkono wake.


Dai tangu siku hiyo akampotezea mazima na Ommy akapotea ila naona anataka kurudi kupitia bifu la kimuziki kati ya Mondi na Kiba.
 

Hii story yako inatusaidia nini???


Maana mi najionea utumbo mtupu , wote mapunga
 
Sio kuwa bob anazungumzia soka maana leo simba wamecheza ila kama ni tofaut apambane na hali yake iliopo kwa sasa
 
Kwani alimpandisha bure? Si alilipwa pesa stahiki kwa wakati ule??
 
Wengine wanajiita simba* kumbe paka nyau.
Wanadiss kwa kuimba* ati baba fulani na mistari ya dharau.
Tozi25 naongoza kula bata* simba ananuka mavi ya paka.
Unamdiss Ali kiba* na wimbo wako fresh.
Huku mtaani wasema* wanapakazia simba analiwa ile nyepes. [emoji51] oops[emoji111]



Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nikajua nitakuta mtu analia huku anagalagala kumbe kichwa cha habari na uzi haviendani hata kidogo.
Maripota wa Bongo ni shida
 
anataka apewe promo
Afanye mziki mzuri tu! Tatizo hawana vipaji kama walivyokuwa navyo hawa mafahali wawili,wanataka kunyanyuka harakaharaka kupitia migongo ya watu,bila kufanya kazi nzuri,hata huyo diamond au kiba hawakunyanyuliwa na promo,promo ilikuja baada ya wao kuonesha uwezo wao.Au naye anataka kuwa kama harmorapa mwenye "artificial"kipaji alivyopotea? Hahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…