Aliyekuwa anajiita rais wa masharobaro au ukipenda muite Mr Chocolate Flavor, Bob Junior hatimaye amlilia Diamond Platnumz na kumlaumu kwa nini amemtupa?
Bob Junior roho inamuuma kwa kuwa yeye ndiye aliyemuibua Diamond na kumfanya ang'ae
Sasa anashangaa kwa nini na yeye diamond asimsaidie kunyanyuka kimuziki kama yeye alivyofanya hapo awali?
Bob Junior aliwahi kutamba na nyimbo kama Nichumu, Oyoyo, na Kimbiji
View attachment 575559
View attachment 575560
Miaka ya nyuma kidogo bob junior alikuwa na ugomvi mkubwa na diamond na mara kwa mara alikuwa anamponda kwenye media, Diamond alijitahidi sana kujishusha ikiwemo kumualika kwenye party mbalimbali lakini bado bob Junior akazidi kumvimbia diamond, na mbaya zaidi akawa team kiba na kumkandia vilivyo Diamond.
Diamond akaona sio kesi akaamua kumpotezea mazima matokeo yake jamaa akasahauilika kabisa kwenye anga ya muziki mpaka sasa ambapo anamlilia Diamond amsaidie kumnyanyua na akumbuke walipotoka.