tatizo lako mara zote unamchukua huyo mungu unaysema ana super natural alafu untaka apeform kwa vigezo na standard zako za kibinadamu. Hata wewe ungekuwa mungu bado "binadamu" tungeona flaw hata hayo matatizo yote yasingekuwepo.
Tatizo lako huelewi kwamba, standards za binadamu zinatakiwa kuwa ndogo ukizilinganisha na standards za mungu.
Kwa mfano, binadamu hana upendo mkuu kama anaotakiwa kuwa nao mungu, na wala hana uwezo usio kikomo, na wala hajaumba mtu, lakini anaweza kulisha watoto in most cases. Kwa upendo na uwezo wa kibinadamu tu.
Sasa wale watoo masikini wa Somalia wanaokufa kwa njaa, ina maana mungu hana uwezo wa kuwalisha? Au anao uwezo ila hajali?
Mimi nilifikiri mungu mwenye uwezo mkubwa zaidi na upendo mkubwa zaidi, na asiye na mpinzani wa kumzuia kufanya chochote anachotaka, angeweza kumba ulimwengu bora zaidi ya huu.
Unless of course unakuja na defense ya "god works in mysterious ways", which is no defense at all, but rather an admission that you do not have answers to tough questions. I can equally say, if you believe "go works in mysterious ways", that may be a self fulfilling prophecy in that the mystery here is that you profess knowing the existence ofn something you have absolutely neither idea nor empirical proof about it's existence at all.
Na kama unasema mungu si kazi yake, katupa akili tujikimu wenyewe, kwa nini kapendelea wengine na kuwapa akili wanaiendesha dunia, tatizo lao si kukosa chakula, tatizo lao chakula kingi, na wengine kawanyima akili kila siku wanapigana vita, hata ukija kuwapa msaada wanataka kukuua?
Hivi mungu mwenye uwezo mkuu anaweza kuumba kiumbe akakinyima akili? Wanaozaliwa na mtindio wa ubongo wamemkosea nini? Viziwi? Vipofu? Kwa nini wengine wanazaliwa na viungo vyote na wengine wanazaliwa kama vinyangarika vya ajabu? Hii ndiyo kazi ya mungu mwenye upendo wa juu kabisa na uwezo usio kifani?
Matatizo yote unayoyaleza wala hayaitaji msaada na intevention za mungu. Mungu alimaliza kumpa binadamu ubongo amboa ni better na wanyama wengine.
Kwa nini kampa binadamu ubongo ambao ni better kuliko wanyama? Ina maana upendo wake umefikia kikomo kwa binadamu na wanyama hawapendi? Inamaana hawa animal right activists wanaotetea haki za wanyama wana upendo kuliko mungu?
Kwa nini hata katika binadamu kuna wengine kawapa akili zaidi ya wengine? Hawa aliowanyima akili anawapenda sawa na wale aliowapa? Kama ndiyo, kwa nini hakuwapa akili nao? Alishindwa au hakutaka tu?
Ukizidi kuchunguza sana haya maswali, kwa nia ya kutafuta ukweli kabisa bila bias ya historia ya kuwa influenced na dini na culture, utagundua kwamba mungu anayeweza yote kujua yote na aliye na upendo usio ikomo hayupo.