Bob Marley aliamini Mungu kweli?

Bob Marley aliamini Mungu kweli?

Ukweli si lazima uendane na kujua.

Uummm.....

Unaweza kuniuliza "Moja jumlisha moja ni ngapi" . Nikakwambia sijui ni ngapi, nikawa sijui, lakini mkweli.

Sasa kama unajua hujui na ukasema hujui huoni utakuwa umesema ukweli kwa kusema hujui? Kujua hujui nao ni ukweli vilevile.

Au hata nikakwambia naamini ni mbili, lakini sijui kwa uhakika, na zaidi wala sijui kwamba sijui kwa uhakika, nikabaki mkweli.

Enhee hapo sasa lakini angalau kutakuwa na namna au njia ya kuusaka huo ukweli. Unamtafuta mtu ajuaye hesabu anakuonyesha jinsi ya kujua moja jumlisha moja.

Kwa hiyo, ukweli hauendani na kujua mara zote, unaweza kuwa mkweli hata usipojua.

Kujua kuwa hujui kitu nako ni kujua ukweli na ukweli hapo ni wewe kutojua.

Hivi unajua kuna watu wengine hawajui hata kama hawajui?

Uummm.....

Sasa kama unajua hujui na ukasema hujui huoni utakuwa umesema ukweli kwa kusema hujui? Kujua hujui nao ni ukweli vilevile.

Enhee hapo sasa lakini angalau kutakuwa na namna au njia ya kuusaka huo ukweli. Unamtafuta mtu ajuaye hesabu anakuonyesha jinsi ya kujua moja jumlisha moja.

Kujua kuwa hujui kitu nako ni kujua ukweli na ukweli hapo ni wewe kutojua.

Hivi unajua kuna watu wengine hawajui hata kama hawajui?

Kuna wengine hawajui kama wanajua, hawajui, au hawako katika kujua au kutokujua, lakini wanaweza kuwa wakweli bado.

Kuna wengine hawajui kama wanajua, hawajui, au hawako katika kujua au kutokujua, lakini wanaweza kuwa wakweli bado.

Duh! Sasa kama mtu hajui kuwa hajui kama anajua basi huyo atahitaji intervention.

.....Rastafarian,kuna wengine wanaita kuwa ni religion,wengine wanasema kuwa ni ideology,na kuna wengine miongoni mwao watakwambia kuwa ni just a way of living,through righteousness and loving in one another.The question of God,whether in believing in HiIM or not nadhani ni very private thing,na nadhani na marastafarians wanali-treat hili swala as such.Kwa ujumla katika imani ya kirastafari (kama mimi ninavyopenda kuiita),imani zimetofautiana.Kuna wengine watakwambia kuwa Haile Sellasie is the Almighty na rightful ruler,na wengine watakwambia kuwa ni messiah na kuna only one God,sasa kama huyu God ndie huyu ambaye wote wanayemuaamini(na katika imani nyingine),I am not sure.

Tukirudi kwa Bob Marley,sidhani kama anamwamini na kumwona Mungu kama macho na imani za wengine zimwonavyo.Bob believes in Haile Sellasie I,sasa kwa what extent,sijui,nadhani hiyo ni kati yake yeye na Mungu wake.Lakini hii ndio hasa iliyofanya waseme pamoja na Tosh "we know while we understand,Almighty God is a living man",wakimaanisha Haile Sellasie.Kama unakumbuka pia katika wimbo huo huo wanasema kuwa,"somemost people think,Great God will come from the sky",kwa wao Mungu yupo hapahapa miongoni mwetu.

Kikubwa ni kuwa Bob alichukia "the system",with all that it represent and stand for,na hapa utaingiza kuanzia religion na politics,kwani hizi ndizo zimekuwa nyanja kuu za kuwatenganisha watu.Ukimuuliza Bob religion yake atakwambia kuwa,I am a Rastaman,bila kumaanisha kuwa rastafarianism ni religion,lakini kuwa yeye hayo ndio maisha yake,since creation.

Kwa kumalizia tu,sidhani kwamba marastafarian wanaishi kwa kumuangalia Bob peke yake kwa kuwa ni icon ya Rastafarianism.Bob ni mmojawapo tu kati ya maicon wengi sana katika rastafarianism.Si kila alichokifanya Bob basi ni norm,na hii ni mojawapo ya vitu vizuri vya rastafarianism,uhuru wa kuishi unavyotaka,as long as you have love in you and ready to spready that love.Na ndio maana hujawahi ona "kanisa" la marastafarins.

Hivyo ndivyo alivyokuwa akiji
Express .... ukweli ni kwamba
Wote hatujui ...

Nilifikiri kuna sehemu Bob Marley kasema haamini Mungu. Kumbe Peter Tosh?

"In the beginning there was the word. The word was Jah. The word is in I, Jah is in I. I make what is good, better, and what is better, best. I follow this in every aspect of life."

- Peter Tosh

But read it in Revelation
You'll find your redemption
And then you give us the teachings of His Majesty,
For we no want no devil philosophy;
A you fe give us the teachings of His Majesty,
A we no want no devil philosophy:
Feel it in the one drop;

Kijamaika Jah ni Mungu - Mungu wa Ibrahimu, Isaka na yakobo. To the rastafarians Yesu is just a prophet lakini Haile Selasie is regarded as Messiah.

Though nao pia (marasta) wanatofautiana sana (madhehebu mengi ya kirasts) though wanafuata sheria ya Musa, wanaamini wao ni kondoo wa Mungu ndiyo maana wanafuga nywele dread. watu wengi wameingia kwenye urasta na wala hawajui maana yake. wakidhani ni kufuga nywele na kula natural foods, Rastafarians ni dini kama zilvyo dini zingine na ina madhehebu yake.

Wengine wanaamini Haile selasie ni Mesiah, wengine ni Yesu aliyerudi na Wengine wanaamin ni Mfalme wao hapa duniani. Na adui yao ni Western World - The Babylon!

about haile selasie, gonga hapa-- Haile Selassie I - Wikipedia, the free encyclopedia

Kuna ma cardinal na maaskofu wanasema wanamuamini mungu, lakini ukisoma vizuri maandishi yao, unaona kwamba kuna tofauti kubwa ya huyu mungu anayeaminiwa na watu kwamba mdingi fulani kakaa juu anawaangalia watu, ataadhibu watundu na kureward wazuri, na huyu wanayemuamini hawa mabingwa wa theolojiai

Wengine wanasema wazi kabisa kwamba "If god does not exist, it is necessary to invent him" primarily to keep people in check..

Kuna wasomi wa theolojia wanaamini mungu lakini mungu kama idea ya "greatest good" wala si kama force fulani, au kitu fulani.

Ndiyo maana nikauliza hili swali.

Kuna watu katika hiyo link ya yahoo wanaongelea kwamba pengine Bob aliamini kwamba "Almighty god is a living man" kwa maana ya kwamba mungu ni wewe na mimi, mungu ni Selassie.

Kwa hiyo, badala ya kukaa chini na kuomba mungu mvua inyeshe, tuanze kuangalia jinsi gani ya kutumia maji ya mito vizuri katika irrigation.

Ndiyo maana unaambiwa "If you know what life is worth, you will look for yours on earth". Hakuna haja ya kungoja "pie in the sky" siku ya hukumu upewe zawadi, mungu hayupo na hukumu ipo hapa hapa duniani kwa mujibu wa jitihada zako.

Usifikiri kila mtu anayesema yeye rasta anaamini kila kitu katika Rastafarianism.

Juzi tumemuona Buju Banton anajiita Rasta kwa miaka kibao, kumbe anauza unga Miami.

Don't believe everything you read. Analyze.

thanx bro. Ni kweli kabisa. But Bob alishasema, hayupo upande wa mweusi wala mweupe ila yupo kwa Jah! Kwa ishu ya Bob ni ya kuiacha kwani ipo kiimani zaidi na yeye ndie anayejua roho yake ipo wapi. Quotes za inspiration huwa zinahitaji ufafanuzi wa mwenyewe kuliko kuamini tu. Kumbuka kuna dini duniani inamuamini Bob kama mtume wao na hawatakuelewa ukisema alikuwa haamini na katk interview bob hakulisema hilo, nina video yake anazungumzia Jah na msimamo wake. Ki ukweli ninaamini kuwa alimwamini Jah na quotes zake watu wanazitafsiri vibaya kupotosha mob ya watu kama mimi wanaomuamini.

Ukweli ni kitu gani.?

Hata kwa wale wanaoamini mafundisho ya bible kuna sehemu Yesu kala ya kusulubiwa naye aliuliza UKWELI ni kitu gani.?????

Kiingereza kiliwapiga chenga sina uhakika lakini kama kuna lugha au mtu anayeweza kumuelezea Mungu kwa lugha ya kibinadamu kwa ufasaha huyo atakua siyo Mungu.Yaani kiumbe kijue kumuelezea kwa lugha ya kibinadamu Muumba(MIMI NIKO)? Na hiyo ndo maana akaitwa Mungu.
I guess "man" here is used in the old fashion sense of "mankind"

Lakini swali langu halijajibiwa, waliposema "Almighty god is a living man" walimaanisha kwamba god is just a con designed by living men? Ukiangalia context kwa mstari unaofuata kuhusu "You can fool some people for some time, but you can't fool all the people all the time" na mistari ya mwanzo "Preacher man don't tell me" utaona jamaa wanasagia religion na habari ya mungu.

Au wanasema "Almighty god is a living man" kwa kum glorify mungu kwamba he is a living force, ila kiingereza kiliwapiga chenga wakashindwa kujieleza vizuri?

isn't creation part of giving birth? in that case God is also a woman if you insist that God is Man (he)?

..GOD is God. Deficult to define in our humanity context ndiyo maana he came to moses with a complicated ID...I AM WHO I AM. God didn't say I am he or she.

Excellent Argument!!

I guess "man" here is used in the old fashion sense of "mankind"

Lakini swali langu halijajibiwa, waliposema "Almighty god is a living man" walimaanisha kwamba god is just a con designed by living men? Ukiangalia context kwa mstari unaofuata kuhusu "You can fool some people for some time, but you can't fool all the people all the time" na mistari ya mwanzo "Preacher man don't tell me" utaona jamaa wanasagia religion na habari ya mungu.

Au wanasema "Almighty god is a living man" kwa kum glorify mungu kwamba he is a living force, ila kiingereza kiliwapiga chenga wakashindwa kujieleza vizuri?

Hapana,upo sawa Mkuu,Kwa Muktadha wao huo wimbo,pamoja na Mambo mengine ni kutakabari kwamba Maisha yetu ni HAKI na siyo zawadi kutoka kwa Mungu na dhihaka kwa Yesu ndiyo maana hapo amesema "in a Jesus'name",hiyo ni tofauti na mtu akisema "In Jesus name",hii ya Mwisho inaleta utukufu,ya mwanzo ni kum-demote Christ!!

Ni kama vile anajaribu kutusadikisha kuhusu kutokukumbatia kwamba kuna Maisha Mengine baada ya haya!! Kwamba Mungu yupo juu as far as he is concerned is a fallacy,that u can fool some people sometimes but u cnt fool ol the people all the time!!

It is a song specifically meant inspire mankind to consider LIFE is a RIGHT rather than a GIFT frm God to be cherished and received with thanksgiving!!

Kwani "nyie" mnaaminimungu gani bro!!!!!!!?

Mie siamini mungu yeyote aliye supernatural.Hakuna mungu.

Bob kashakwambia "if you know what life is worth, you will look for yours on earth", hamna "pie in the sky", hiyo ilikuwa ni trick ya bullies of the old katika jitihada za kukunyang'anya chako katika maisha haya huku wakikwambia "mungu atakulipa mbinguni"

Mungu mwenye nguvu zote na upendo wote angekuwepo maisha yasingekuwa mabaya hivi, watu wengine wanatumia maelfu ya lita kwa siku kumwagilia lawns, huko Afrika kinamama wanatembea kilomita 20 kutafuta maji kwa siku. Huku wengine wanapeleka mbwa kwa vet wakati huko kwetu hata wazee tunashindwa kuwahudumia. I can go on and on.

Kwa nini niamini kwamba mungu yupo? Kama mimi ningekuwa na nguvu hata nusu tu za huyu mungu dunia ingekuwa nzuri sana.

Mie siamini mungu yeyote aliye supernatural.Hakuna mungu.

Bob kashakwambia "if you know what life is worth, you will look for yours on earth", hamna "pie in the sky", hiyo ilikuwa ni trick ya bullies of the old katika jitihada za kukunyang'anya chako katika maisha haya huku wakikwambia "mungu atakulipa mbinguni"

Mungu mwenye nguvu zote na upendo wote angekuwepo maisha yasingekuwa mabaya hivi, watu wengine wanatumia maelfu ya lita kwa siku kumwagilia lawns, huko Afrika kinamama wanatembea kilomita 20 kutafuta maji kwa siku. Huku wengine wanapeleka mbwa kwa vet wakati huko kwetu hata wazee tunashindwa kuwahudumia. I can go on and on.

Kwa nini niamini kwamba mungu yupo? Kama mimi ningekuwa na nguvu hata nusu tu za huyu mungu dunia ingekuwa nzuri sana.

tatizo lako mara zote unamchukua huyo mungu unaysema ana super natural alafu untaka apeform kwa vigezo na standard zako za kibinadamu. Hata wewe ungekuwa mungu bado "binadamu" tungeona flaw hata hayo matatizo yote yasingekuwepo.

Matatizo yote unayoyaleza wala hayaitaji msaada na intevention za mungu. Mungu alimaliza kumpa binadamu ubongo amboa ni better na wanyama wengine.

Understanding ya Bob Marley kuhusu Mungu na spirituality in general ni challenging.
Alikua akiamini kua "Christ" ni hali ya mtu na wala sio mtu specific. E.g: Wakristu wengi wanaamini Yesu ni Kristo. Yeye anaamini Yesu ni mtu ila alifikia hali ya ukristo kwa Divine transcendence. Mtu wa kawaida pia anaweza fikia hali hio kwa kupitia mafunzo ya Yesu na wengine walio weza kufikia hali hio. Salassie wa Ethiopia ni moja wapo katika watu walio weza kufikia hali hio na kwa hiyo pia ni Kristo na Divine part of him ni Mungu tayari kajitokeza kwa "gamba" la binadam.
God is in Us, we all have the Divine part in us. Ni vigumu kutambua hio Divine part sababu ya mambo ya dinua ila uki concentrate unaweza kugusia hali hio. Kama utashindwa ku-concentrate unaweza kuvuta majani (Bang, msuba) na ikakusaidia kupoteza connexion na vitu vya duniani ukawa in sync na Divine part inside of you.
Kwa kweli sijui kama nimeeleweka maana maneno mengi nimeshindwa kuyasema kwa kiswahili ila kwa kifupi hiyo ndio msingi ya imani ya Bor Marley.

tatizo lako mara zote unamchukua huyo mungu unaysema ana super natural alafu untaka apeform kwa vigezo na standard zako za kibinadamu. Hata wewe ungekuwa mungu bado "binadamu" tungeona flaw hata hayo matatizo yote yasingekuwepo.

Tatizo lako huelewi kwamba, standards za binadamu zinatakiwa kuwa ndogo ukizilinganisha na standards za mungu.

Kwa mfano, binadamu hana upendo mkuu kama anaotakiwa kuwa nao mungu, na wala hana uwezo usio kikomo, na wala hajaumba mtu, lakini anaweza kulisha watoto in most cases. Kwa upendo na uwezo wa kibinadamu tu.

Sasa wale watoo masikini wa Somalia wanaokufa kwa njaa, ina maana mungu hana uwezo wa kuwalisha? Au anao uwezo ila hajali?

Mimi nilifikiri mungu mwenye uwezo mkubwa zaidi na upendo mkubwa zaidi, na asiye na mpinzani wa kumzuia kufanya chochote anachotaka, angeweza kumba ulimwengu bora zaidi ya huu.

Unless of course unakuja na defense ya "god works in mysterious ways", which is no defense at all, but rather an admission that you do not have answers to tough questions. I can equally say, if you believe "go works in mysterious ways", that may be a self fulfilling prophecy in that the mystery here is that you profess knowing the existence ofn something you have absolutely neither idea nor empirical proof about it's existence at all.

Na kama unasema mungu si kazi yake, katupa akili tujikimu wenyewe, kwa nini kapendelea wengine na kuwapa akili wanaiendesha dunia, tatizo lao si kukosa chakula, tatizo lao chakula kingi, na wengine kawanyima akili kila siku wanapigana vita, hata ukija kuwapa msaada wanataka kukuua?

Hivi mungu mwenye uwezo mkuu anaweza kuumba kiumbe akakinyima akili? Wanaozaliwa na mtindio wa ubongo wamemkosea nini? Viziwi? Vipofu? Kwa nini wengine wanazaliwa na viungo vyote na wengine wanazaliwa kama vinyangarika vya ajabu? Hii ndiyo kazi ya mungu mwenye upendo wa juu kabisa na uwezo usio kifani?

Matatizo yote unayoyaleza wala hayaitaji msaada na intevention za mungu. Mungu alimaliza kumpa binadamu ubongo amboa ni better na wanyama wengine.

Kwa nini kampa binadamu ubongo ambao ni better kuliko wanyama? Ina maana upendo wake umefikia kikomo kwa binadamu na wanyama hawapendi? Inamaana hawa animal right activists wanaotetea haki za wanyama wana upendo kuliko mungu?

Kwa nini hata katika binadamu kuna wengine kawapa akili zaidi ya wengine? Hawa aliowanyima akili anawapenda sawa na wale aliowapa? Kama ndiyo, kwa nini hakuwapa akili nao? Alishindwa au hakutaka tu?

Ukizidi kuchunguza sana haya maswali, kwa nia ya kutafuta ukweli kabisa bila bias ya historia ya kuwa influenced na dini na culture, utagundua kwamba mungu anayeweza yote kujua yote na aliye na upendo usio ikomo hayupo.

Back
Top Bottom