LGE2024 Bob Wangwe aiomba Mahakama Kuu iizuie TAMISEMI kusimamia shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Maombi yanayoombwa na Waleta maombi ni pamoja na;

1. Mahakama Kutoa ruhusa kwa Waleta maombi kuwasilisha maombi ya kufuta Sheria Ndogo zilizotolewa kupitia matangazo ya serikali Na. 571, 572, 573, na 574 ya tarehe 12/7/2024;

2. Mahakama kutoa ruhusa kwa waleta maombi kuwasilisha maombi ya kuizuia TAMISEMI kuratibu, kuandaa, na kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024;

3. Mahakama kuweka zuio kwa TAMISEMI, mawakala wake, wawakilishi au wafanyakazi wake kuratibu, kuandaa, na kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024.



 
All stars team ya mawakili
 
Dadeeeeeeeeeeeeki hawa sasa ndio wanasheria
 
Niko tayari kuchangia mil 10 taslimu ili kurahisizha mchakato
 

jambo hili ni rahisi mno na hasa ukizingatia waleta maombi ni wazalendo lakini pia ni mawakili wangwana sana humu nchini,

maombi yote yatajibiwa kwa kuzingatia gharama za maandalizi ya uchaguzi zilizotumika, athari na hasara za kutofanyika uchaguzi huo na hatua ya maandalizi ya uchaguzi huo iliyofikiwa,

nadhani uamuzi wenye maelezo ya kina utatolewa baada ya uchaguzi wenyewe November,2024...
na wito wa mapendekezo ya marekebisho utaambatanishwa kwajili ya maandalizi ya chaguzi zijazo....
 
Wana-Group wote mliopo hapa jukwaani na raia wengine tunawaalika kesho kwenye Kesi ya Kupinga Uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kusimamiwa na Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), iliyopangwa kwa mara ya kwanza kutajwa kesho saa 8 mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Kesi itakuwa mbele ya Jaji Dyansobera.

KARIBUNI WOTE
 
Una zani tamisemi inazuia usishinde tuwaangalie mawakala wa nao wekwa na kila chama wengine wanakuwa wananjaa wempaka ijioni wanna chupa ya maji tu chukula awaja nunuliwa sasa apo una semaje
Swala siyo wakala acha kuhalalisha wizi wa kura! Kura zinatakiwa zipigwe lakini taratibu kanuni na Sheria vizingatiwe. Wasimizi wasimamie wahesabu watoe taarifa sahihi siyo lazima wakala awepo. Acheni mawazo ya wizi,wizi,wizi,......
 
Mungu awe pamoja nawe Bob Chacha Wangwe.

God Bless you and the Womb that Reared you.
 
Ngoja tusikia na kuona weledi wa Jaji.

Bob Wangwe tayari yuko supported na Uamzi wa Mahakama ya Afrika iliyoagiza Mamlaka za Tanzania kubadili vifungu vya sheria ya uchaguzi ikiwemo kufuta Wazimamizi kuwa Wanachama wa ccm au wateule wa Rais ambaye naye ni mgombea.

Tunahitaji vijana wenye weledi kama hawa.
 
Mabadikiko yanawezekana ni kukosa utayari tu wa chama cha kijani.

Mbona mambo mengine wanayafanya usiku kuamkia mchana tu.
 
Huko sahihi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…