Bobi Wine: Katiba Mpya pekee si suluhisho

Bora kawachana,unajua Chadomo wanadhani Katiba mpya itawasukumiza Ikulu kama mlevi huku ccm ikihofia kivuli tuu..

Hapa Tzn ukiwaambia wamama kwamba wapinzani wanahatarisha amani,hapo tayari kula zote wanazoa..
 
Huwezi kuandika katiba mpya bila ya kugusa muungano kitu ambacho CCM hawataki hata kukisikia. Nyerere aliwaonya wasiuguse na mpaka leo wako tayari kuulinda kwa gharama yoyote.
 
S
Sebo MACHEDMA hayawezi kukuelewa
 
Huu ndio ukweli. Mfano zipo sheria nzuri nyingi tu lakini hazifuatwi. Kuna sheria inayotaka vyama kuitaarifu Polisi kabla ya mikutano yao? Lakini hii imekuwa fimbo ya kudumu kwa wapinzani na wameshindwa hadi sasa kupinga hilo hata kimahakama.

..Katiba mpya na bora ni muhimu ili kuondoa hayo makandokando yanayotusumbua sasa hivi.

..Katiba mpya ndiyo itakayokuwa dira yetu ya kuelimishana, kuelekezana, na kujengana, ktk misingi ya usawa, haki, na demokrasia.

..Ni kweli miongoni mwetu wako waliopinda, lakini ili kuwarekebisha ni lazima uwe na muongozo mzuri ambao ni katiba bora tofauti na hii iliyopo sasa hivi.

..Kwa upande wangu mtu anayejaribu kudogosha umuhimu wa Katiba mpya bora hapa Tanzania namfananisha na Imamu anayetaka kueneza Uislamu bila msahafu, au Mchungaji anayedai anaweza kueneza Ukristo bila rejea ya Biblia.

..Baada ya ukatili na mabavu ya awamu ya 5 sijui ni kwanini bado kuna baadhi yetu hawaoni ulazima wa Katiba mpya au hatari iliyo mbele yetu kijamii na kisiasa tukiendelea na Katiba hii ya sasa hivi.
 
Afrika ni bara changa kivipi? Kama halijakua badi limedumaa!
 
Kuna Vijana wa matusi watajazana hapa Muda si mrefu


B

Ni kama unalazimisha utukanwe ili upate mahali pa kubeba hoja zako za kizushi. Piga kimya kama huna jipya mzee.
 
Yupo sahihi, ni kweli hata kama Nchi ikiwa na Katiba nzuri Bado inaweza isiheshimiwe na Viongozi wetu.

Bora iwepo kisha isiheshimiwe ili tuone. Kinachofanya katiba yetu isiheshimiwe ni hiki kitendo cha rais kuwa na madaraka makubwa kupita inavyotakiwa, kisha kupata kinga ya kikatiba asishitakiwe akiwa madarakani au akiwa ametoka. Hapo ndio matatizo yote yanapoanzia. Mimi huu mjadala wa katiba mpya bila kuwa na machafuko, najua fika itapatikana katiba ambayo haitaheshimiwa. Machafuko tu ndio sahihi ya kupata katiba itakayoheshimiwa na wote.
 
Kyagulanyi ameongea 💪

Hata katiba iandikwe na malaika....haitokuwa na tija itakiwayo ikiwa inashindwa KUSIMAMIWA VYEMA......

#KATIBA YETU NI BORA NA INATUTOSHA🙏
 
Kyagulanyi ameongea 💪

Hata katiba iandikwe na malaika....haitokuwa na tija itakiwayo ikiwa inashindwa KUSIMAMIWA VYEMA......

#KATIBA YETU NI BORA NA INATUTOSHA🙏
Inakutosha ww na wenzio walamba asali pamoja na machawa.
Mm na wenzangu tunataka katiba mpya.
 
Hakuwa mgeni rasimi, alikua mgeni mwalikwa. Shukrani kwa taarifa.
 
Bob wine ni mpinzani wa kweli anajua tatizoliko wapi

Sawa Chadema watamtukana whatever lakin ana hoja

Katiba pekee sio kila kitu
Kama katiba bora siyo kila kitu, tufanyeje sasa? Tutulie na hii iliyopo na kuacha maisha yaendelee? Au tuipate hiyo bora na kuweka misingi ya kuhakikisha inafuatwa?
 
Chadema hawapend kuambiwa ukwel utashangaa watakavyo mnanga mgeni wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…