BOCCA DELLA VERITÁ: Sanamu ambayo ukiongea uwongo hukukata vidole

BOCCA DELLA VERITÁ: Sanamu ambayo ukiongea uwongo hukukata vidole

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
BOCCA DELLA VERITA:

Inaitwa MOUTH OF TRUTH

Screenshot_20210205-191539.png

Ipo na inakaa nje ya mlango wa Santa Maria katika Kanisa la Cosmedin Rome Italia

Ni sanamu kubwa iliyo katika hadithi nyingi, inafanana na uso wenye ndevu wa kiume na mashimo ya macho, pua na mdomo.

Kulingana Hadithi nyingi
Mume ambaye alimwamini mkewe alimpeleka kwenye sanamu hiyo "Kinywa cha Ukweli'' ili kujaribu uaminifu wa mkewe. Baada ya hapo, mwanamke huyo aliapa mbele ya Kinywa cha Ukweli kwamba alikuwa tu chini ya mumewe na hajawahi kuwa na mwanaume mwingine tofauti mumewe.

Screenshot_20210205-191527.png

Hadithi zinasema ukifika katika Sanamu hii ukaweka mkono ndani ya kinywa hicho na ukazungumza uwongo basi mdomo huo hujifunga na kukukata vidole.

Watu wengi wamehofia kuapa katika Kinywa cha Ukweli.

Kuna visa vingi kuhusu Sanamu hii.

Screenshot_20210205-191610.png

Sanamu hiyo iliwahi kuwa katika Piazza della Bocca della Veritá hadi 1632.

Halafu ikahamishiwa nje ya moja ya kuta za kanisa la Santa María huko Cosmedin, mahali ambapo ipo mpaka leo.

Screenshot_20210205-191624.png

Ni kawaida sana kuona idadi kubwa ya watu wakijipanga kupiga picha kwa kuweka mkono wao ndani ya Kinywa cha Ukweli na kuapa.

Screenshot_20210205-191552.png

DA'VINCI XV
 
Mungu hajawahi kuumba sanamu, hilo ni shetani lenyewe.

Kutoka : Mlango 20
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
 
sawa sawa mkuu litakuwa jini hilo😂😂
Mungu hajawahi kuumba sanamu, hilo ni shetani lenyewe.

Kutoka : Mlango 20​

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
 
Back
Top Bottom