Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wakati msimu wa Ligi Kuu Tanzania na Ligi ya Mabingwa Afrika inaanza, Mashabiki wa Simba wa Dar es salaam walikuwa wanaona Bocco uwezo wake ni mdogo sana na hivyo wakawa wanamzomea kwenye mechi alizocheza kwa Mchina. Leo Bocco ndiyo nguzo ya ushindi wa Simba.
Okwi aliposajiliwa kwa mara nyingine tena na simba, baadhi ya Mashabiki wa Simba waliilaumu simba kusajili "Mzee". Leo hii ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Simba.
Kila wakati Chama anapoonekana na Mashabiki wa simba kwamba anacheza chini ya kiwango na anatakiwa kutoka, ndipo chama hufanya yasiyotarajiwa. Chama amefunga magoli muhimu sana kwa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa.
Wakati anasajiliwa na kuanza kucheza kwenye Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar, Zana Coulibaly alisababisha mashabiki wa Simba wahoji ni kwa nini kasajiliwa. Kwenye Mechi za Zanzibar mpaka wachezaji wenzake walikuwa wanakwepa kumpasia kwa kutomwamini. Leo Zana mbali ya mbwembwe zake baada ya mechi, amebeba imani ya watu wa Msimbazi kwenye eneo la Ulinzi.
Hawa wachezaji wametufunza Simba msemo wa Kiingereza usemao "Think before you leap".