Bocco,Okwi,Zana na Chama wametutia adabu Simba

Bocco,Okwi,Zana na Chama wametutia adabu Simba

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Wakati msimu wa Ligi Kuu Tanzania na Ligi ya Mabingwa Afrika inaanza, Mashabiki wa Simba wa Dar es salaam walikuwa wanaona Bocco uwezo wake ni mdogo sana na hivyo wakawa wanamzomea kwenye mechi alizocheza kwa Mchina. Leo Bocco ndiyo nguzo ya ushindi wa Simba.

Okwi aliposajiliwa kwa mara nyingine tena na simba, baadhi ya Mashabiki wa Simba waliilaumu simba kusajili "Mzee". Leo hii ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Simba.

Kila wakati Chama anapoonekana na Mashabiki wa simba kwamba anacheza chini ya kiwango na anatakiwa kutoka, ndipo chama hufanya yasiyotarajiwa. Chama amefunga magoli muhimu sana kwa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa.

Wakati anasajiliwa na kuanza kucheza kwenye Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar, Zana Coulibaly alisababisha mashabiki wa Simba wahoji ni kwa nini kasajiliwa. Kwenye Mechi za Zanzibar mpaka wachezaji wenzake walikuwa wanakwepa kumpasia kwa kutomwamini. Leo Zana mbali ya mbwembwe zake baada ya mechi, amebeba imani ya watu wa Msimbazi kwenye eneo la Ulinzi.

Hawa wachezaji wametufunza Simba msemo wa Kiingereza usemao "Think before you leap".
 
Mimi siyo mtaalam wa mpira lakini huwa sielewi ni kwa nini Niyonzima huwa anaingizwa kipindi cha pili!! Jamaa namkubali sana!

Ni maamuzi ya kocha. Niyonzima uchezaji wake anagombania namba na Chama. Wote hawa ni wazuri wakiwa na mpira mguuni, Niyonzima ni mwepesi zaidi na ana nguvu kuliko Chama, ila Chama ana madhara zaidi kwa timu pinzani. Anatoa pasi za mwisho zaidi kuliko Niyonzima lakini pia anafunga mwenyewe inapobidi. Takwimu hazidanganyi
 
Mpira mkubwa aliyeonyesha Simba si wa nchi hii. Zana na Niyonzima they were in the best peak
Ila nina wasiwasi pale Simba kama wanapigana misumari ya moto, wachezaji ni talented lakini sio continuously... Yaani kuna kipindi haya majembe yanakuwa floppy ndani ya msimu, tofauti na wachezaji wa Ulaya.
 
Mimi siyo mtaalam wa mpira lakini huwa sielewi ni kwa nini Niyonzima huwa anaingizwa kipindi cha pili!! Jamaa namkubali sana!
Hata mm huwa sielewi, lakini tulibishana na mtu mmoja why Mzamiru aanze badala ya Niyonzima? Nikaambiwa eti Mzamiru anasaidia kukaba, Nikajiuliza Niyonzima hakabi?? Lakini mechi dhidi ya Soura & Na Vita nadhani Mwalimu ampe priority Niyonzima!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukaba hata Messi anakaba,lakini je Messi ni Mkabaji??nafasi ya kiungo mkabaji unatakiwa uwe Mkabaji,Mkude mwenyewe anapungukiwa ukabaji,ukabaji unafanywa na Kotei,ndio maana Mkude anapata taabu sana timu ya Taifa hakuna Kotei kule

Hadi hapo mm huwa sielewi ila kwa sasa nahisi watu wameona mpira wa Niyonzima na kocha kaona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom