Bodaboda, Bajaji, Daladala, Taxi sasa marufuku.

Bodaboda, Bajaji, Daladala, Taxi sasa marufuku.

RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013

IBARA YA 25 ( 2 )



"Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano."



Dukuduku langu: Wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma wanaotegemea sekta hii adhimu na
wananchi tusio na vyombo binafsi vya usafiri tutaishije katika enzi za Katiba mpya?

Dah, nimecheka kweli; kwa hali hiyo basi hata biashara ya meli, mabasi na ndege itakuwa marufuku!!!

Dah!! Mzee wewe unajua kugeuza ukweli wa maneno kweli kweli tena kwa kutumia mantiki ya hali ya juu sana.
 
Wow! Kweli au ni Utani??

Hivi ndivyo vijana wa Kitanzania wanavyo itafsiri katiba????
 
Hivi ndivyo vijana wa Kitanzania wanavyo itafsiri katiba????
Hivi ndivyo wazee wa Kitanzania wanavyoandika katiba?


The guy has a point Kwameh, kama rasimu ya katiba ilimaanisha 'human traficking' wangesema 'biashara ya ulanguzi wa binadamu' na ku-define neno 'ulanguzi' . Otherwise kwameh is right
Thank you!

Mimi nimeelewa kama ilivyoandikwa, wao wanasema mimi sikwenda shule. Sawa, lakini nawauliza, huko shuleni kwao hawakufundishwa kwamba, unapotafsiri kitu kutoka lugha moja kwenda nyingine, kama Tume ya Katiba ilivyotufanyia hapa, hivi huangalii kama inaleta maana kwenye hiyo lugha yako?

The president's wife spoke the naked truth. Hawa watasema mke wa rais aliongea ukweli uchi.
 
Biashara ya kusafirisha binadamu( binadamu anahusishwa lakini katika hali ya mzigo.Hasafiri bali anasafirishwa bilautashi na hiari yake na hali ya kawaida anamilikiwa na msafirishaji. Anakuwa binadamu lakini utu wake unaondolewa kabisa na kuvishwa daraja la UTUMWA)
Biashara ya kusafirisha BINADAMU ni tofauti kabisa na Biashara ya kusafirisha ABIRIA.

Neno binadamu limetumika kwa mkazo mkubwa wenye kubeba uzito wa tendo zima la kusafirisha. Kusafiriha binadamu, linasisitiza uharamia dhidi ya binadamu. Kwa kawaida na katika mazungumzo ya kawaida, usafiri wa daladala ndege au bodaboda unaitwa kusafirisha watu na katika kiswahili fasaha huitwa kusafirisha abiria.)
Katiba ingetoa marufuku ya kusafirisha abiria nchini Tanzania ingekuwa na maana hiyo uisemayo) Neno abiria ndilo neno mahususi katika biashara halali ya kusafirisha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Biashara ya kusafirisha mizigo( hapo binadamu hahusishwi)
Biashara ya kusafirisha viumbe hai(hapo binadamu hahusishwi, wamo Twiga simba ndege, nyoka,smaki na hata bacteria))

Biashara ya kusafirisha abiria(Hii inahusisha watu na mizigo yao wasafiripo kwa hiari yao na kwa gharama yao wenyewe wakiwa watu huru)

Hii ni Tafsiri yangu na baadhi ya Wazee wenzangu na vijana nilioongea nao.
Lakini kwa vile kiswahili kinabadilika kila siku huenda siko sahihihi kabisa. Kiswahili changu enzi Zile 1983 za kuwasoma akina Chonge Maugwaju- wakitamanishwa tende na halua za Oman, pia Lyanda na Wafakiri katika Ubwana na utwana SHULE- Tosamaganga Walimu-Dhambi na Mgunya.
 
kwa hali hiyo basi hata biashara ya meli, mabasi na ndege itakuwa marufuku!!!
Si zote.

Meli za mizigo hazikatazwi, mabasi ya kusafirisha watu ambayo yanamilikiwa na anaesafiri ( kama timu ya mpira) hayajakatazwa, ndege itategemea, zile za mizigo hazijapigwa marufuku. Kilichokatazwa kina pande mbili, ni lazima awe mtu, na pilu yawe yamefanyika malipo.

Hasafiri bali anasafirishwa bilautashi na hiari yake
Sasa huyo katekwa, kidnapped! Hawaongelei kuteka hapa, wangesema.

Anakuwa binadamu lakini utu wake unaondolewa kabisa na kuvishwa daraja la UTUMWA
Hiyo sasa Slave Trade, biashara ya utumwa! Hawajasema biashara ya utumwa marufuku, ila biashara ya kusafirisha binadamu.

Biashara ya kusafirisha viumbe hai(hapo binadamu hahusishwi, wamo Twiga simba ndege, nyoka,smaki na hata bacteria)
Hiyo ni biashara ya kusafirisha wanyama! Kwa swala la Twiga, ni usafirishaji wa nyara za serikali.

linasisitiza uharamia dhidi ya binadamu.
Uharamia unaongeza wewe. Wangetaka wangesema uharamia, hawajasema wamekataza uharamia dhidi ya binadamu, wamesema tatizo ni biashara ya kusafirisha binadamu!

Biashara ya kusafirisha BINADAMU ni tofauti kabisa na Biashara ya kusafirisha ABIRIA..... Kwa kawaida na katika mazungumzo ya kawaida, usafiri wa daladala ndege au bodaboda unaitwa kusafirisha watu na katika kiswahili fasaha huitwa kusafirisha abiria.
Huwezi kusema "kusafirisha abiria."

Abiria ni mtu anaesafirishwa, kwa hiyo ni kiswahili kibovu kusema "kusafirisha mtu anaesafirishwa"! Ndio maana hawakusema wanapiga marufuku biashara ya kusafirisha abiria, bali binadamu.

Neno abiria ndilo neno mahususi katika biashara halali ya kusafirisha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Abiria haihusiani na biashara. Unapompa jirani yako hisani ya kumbeba kwenye gari lako mkielekea eneo moja moja huyo ni abiria wako! Daladala halisafirishi abiria, linapandisha abiria, lakini halisafirishi abiria, linasafirisha umma.

Kama rasimu itapita kama ilivyo utakuwa wakati mgumu sana kwa wengi. Wanaotegemea shughuli za biashara hii na pia wananchi tusio na vyombo vyetu vya usafiri tupeleke vilio vyetu kwa watunga katiba.
 
Kama nilivyosema kiswahili kimekua

Daladala halisafirishi abiria, linapandisha abiria na linasafirisha umma.

Wajuzi wa kiswahili, hasa vijana saidieni hapa.

Abiria chunga mzigo wako.
Umma chunga mzigo wako
 
Back
Top Bottom