PreGE2025 Bodaboda, Bajaji na Wajasiriamali Dar wagomea maandamano CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waendeshaji Bajaji, Bodaboda na Wajasiriamali Jijini Dar es Salaam wametangaza kutoshiriki maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yaliyopangwa kufanyika Aprili 24, 2025, kuelekea Mahakama ya Kisutu, ambako kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, inatarajiwa kusikilizwa.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Ilala, Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wadogo nchini, Steven Lusinde, amesema wanachama wao wameamua kutumia siku hiyo kwa shughuli za kiuchumi badala ya kushiriki maandamano.

"Hatuko tayari kupoteza muda kwenye maandamano. Tunajitambua na tunathamini kazi zetu za kila siku ambazo zinatuletea riziki na maendeleo," amesema Lusinde.

Lusinde ameongeza kuwa wanapinga vitendo vya uchochezi, na badala yake wanahamasisha amani na utulivu. Pia amekumbusha kauli ya zamani ya mmoja wa viongozi wa CHADEMA aliyewahi kudharau kazi ya bodaboda kwa kusema ni 'kazi ya laana, jambo ambalo bado halijapokewa vizuri na wahusika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Maofisa Wasafirishaji nchini, Said Kagomba, amethibitisha kuwa wamepata taarifa za maandamano kupitia vyombo vya habari, lakini hawatashiriki. Ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha amani inadumishwa.
View attachment 3311057
Wanaccm bodaboda, kwani chadema wametangaza maandamano?
 
Hao ni chawa halafu ndiyo majambazi wa kesho umeshawahi kujiuliza wachezaji huwa wanapata umaarufu na wakatundika daruga zao wasiwe na kitu chochote kile sababu ya umri mkubwa
Je huyo bodaboda wa leo ambaye mwanaye anasoma shule za kata ataendesha bodaboda mpaka akiwa na miaka 70?
Yaani tutakuwa na kinababu mabodaboda,mimi mwenyewe nikiona mtu mzima anaendesha bodaboda huwa sipandi
Naamini kipindi hicho wataenda kula wanakopeleka mboga sasa hivi
 
Kwani Chadema wametangaza maandamano tarehe 24?

Halafu siku hizi bodaboda koti zao zao zinakuwa na picha ya Samia?
 
Wewe na huyo Lema mlisema bodaboda wamelaaniwa. Nyumbu kwa usahaulifu hovyo sana. Leo mnawaona wanafaa kuandamana.
Sasa kama hao akina kajulamimba unaachaje kusema kua wamelaaniwa, Chadema ipi iliyoitisha maandamano?
 
Obviously wametumwa na sisiemu kwa vijiposho vya siku 1, hakuna maandamano yaliyoitishwa na mtu yeyote, wametoa wapi haya?
 
Waache kutafuta riziki wanye kumsikiliza kichaa Lema na Mdude
Kwani hawo uvccm wameambiwa kuna maandamano au ni ujinga wao tu wa kupewa buku na kulipiwa hiyo sehem kuja kuongea hayo mavi ya bata.
 
Wewe na huyo Lema mlisema bodaboda wamelaaniwa. Nyumbu kwa usahaulifu hovyo sana. Leo mnawaona wanafaa kuandamana.
Kwani ni nani aliyewambiwa waende kusikiliza kesi au ni utaahira wao tu.
 
Back
Top Bottom