KERO Bodaboda kuvamia barabara za mwendokasi imekuwa kero, wanafanya ajali zisiishe

KERO Bodaboda kuvamia barabara za mwendokasi imekuwa kero, wanafanya ajali zisiishe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

heartbeats

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
8,042
Reaction score
13,383
Hivi mamlaka hazioni au ndo zimeshindwa kuwa-manage maana imekuwa kero kero, wanasababisha ajali tena katika zebra wameigeuza barababara ya mwendokasi kama yao special

Kama Serikali inashindwa kusimamia utaratibu mdogo kama hivi wataweza kusimamia kipi sasa,?

Kikawaida tokea chini katika mambo madogo unaona ni jinsi gani serikali ilivyofeli kitu kidogo kama hiki inashindwa kusimamia vipi kuhusu nyanja zingine

Mamlaka zinazohusika hamtendi kazi ipasavyo boda boda zinazidi kuwa nyingi mjini mkishindwa kuzipangilia kwa sasa basi hamtoweza tena, mnafanya uzembe.
 
Tatizo ni wanasiasa wa pande zote kila mmoja ananufaika nao

Ikitokea CCM kupitia Wakurugenzi wa Jiji waseme Boda Boda hazitakiwi fika mjini, Vyama vingine vitapiga kelele kuwa wanaonewa.
Hivyo CCM inaonena liwalo na liwe ila boda boda ni tatizo sugu litalosumbua sana miaka ijayo
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hao siyo bodaboda, hao ni Bolt, baba yao ameshaingia mikataba na wakulungwa, safar ziwe za haraka, ila wameuchuna wasioneshe uzwazwa wao...
 
Tatizo pia barabara zenyewe za mwendokasi hazina hata hayo magari ya mwendokasi, kwanini zisitumike ipasavyo kurahisisha usafiri na kutoa huduma wakati wote?
 
Tatizo pia barabara zenyewe za mwendokasi hazina hata hayo magari ya mwendokasi, kwanini zisitumike ipasavyo kurahisisha usafiri na kutoa huduma wakati wote?
Kwaiyo boda boda tu ndo zinawahi basi ata bajaji na dalaldala zipite umo
 
mwendokasi ya gerezani - mbagala updates zake zimeishia wapi mbona kimya sana, walishauriwa waanze mazoezi ya kuzuia pikipiki zisipite mwendokasi na kuanza matumizi ya taa za barabarani sjui kama wamepokea ushauri
 
Miafrika na ustaarabu ni vitu viwili tofauti from the top to the bottom. Miviongozi inapita hapo hapo. Polisi hapo hapo hata kama hawana emergency, it's only right bodaboda nao wapite ukizingatia mwendokasi zenyewe hazipo.
 
Mwendokasi zenyewe hazipo ni bora tu wakitumia hizo barabara mpaka pale mwendokasi zitakapoletwa. Haiwezekani barabara zibaki bila matumizi na foleni ni kubwa sana
 
Kwaiyo boda boda tu ndo zinawahi basi ata bajaji na dalaldala zipite umo
Naona bora hivyo kuliko kuwa na wastage of resources, yaani barabara ijengwe halafu isitumike to the maximum sasa imejengwa ya nini?
 
Hatua zikichukuliwa mtaanza kupinga na kusema serikali haiwajali watu.
 
Back
Top Bottom